Kesi mita 200 moto.
Mvutano mkali wa hoja za kisheria ulitikisa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana wakati Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson alipoiomba mahakama itupilie mbali maombi ya walalamikaji katika kesi inayohusiana na umbali wa mita 200 za kusimama kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.
Dk. Ackson alidai mahakamani hapo kuwa maombi ya kesi ya kikatiba ya kutaka tafsiri ya kifungu cha 104 cha Sheria ya Uchaguzi yamewasilishwa na walalamikaji kwa kutumia sheria isiyostahili...
Vijimambo
Habari Zinazoendana
9 years ago
Mtanzania20 Oct
Kesi ya mita 200 kuanza leo
Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
JOPO la majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo linatarajia kuanza kusikiliza kesi ya kikatiba kuhusu haki ya mpigakura kukaa umbali wa mita 200 kama ni sahihi au la.
Jopo hilo la majaji Seleman Kihiyo, Aliyisius Mujuluzi na Lugano Mwandambo, liliteuliwa baada ya mgombea ubunge wa Viti Maalumu Jimbo la Kilombero kupitia Chadema, Amy Kibatala, kufungua kesi hiyo kupitia kwa wakili Peter Kibatala.
Katika maombi yake, anaomba Mahakama Kuu ya...
9 years ago
Habarileo21 Oct
Kesi ya kukaa mita 200 leo
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana imeshindwa kusikiliza kesi kikatiba kuhusu uhalali wa kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupiga kura, kwa kuwa upande wa Jamhuri haujawasilisha utetezi wao.
9 years ago
Mtanzania22 Oct
Mvutano mkali waibuka kortini kesi ya mita 200
NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM
MVUTANO mkali wa zaidi ya saa sita umeibuka katika kesi ya kutaka kujua uhalali wa wananchi ama wapigakura kukaa nje ya mita 200 kutoka katika vituo vya kupigia kura na kutaka tafsiri ya mahakama kuhusu kifungu cha sheria ya uchaguzi namba 104(1).
Mvutano huo uliibuka kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wakili wa mleta maombi katika shauri hilo wakati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilipoanza kusikiliza kesi hiyo jana.
Kesi hiyo inayosikilizwa na...
9 years ago
GPL![](http://globalpublishers.co.tz/wp-content/uploads/2015/10/Peter-Kibatala-620x308.jpg)
KESI YA WAPIGA KURA KUKAA MITA 200 YAAHIRISHWA
9 years ago
StarTV23 Oct
 Uamuzi kesi wa mita 200  iliyofunguliwa kutolewa Oktoba 23
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imetoa maelekezo kuwa Oktoba 23 mwaka huu itatoa Uamuzi dhidi ya Kesi iliyofunguliwa ya Kikatiba kuhusu Tafsiri sahihi ya Umbali anaotakiwa kusimama Mpiga kura baada ya kupiga kura.
Kesi hiyo Namba 37 ya Mwaka 2015 iliyofunguliwa na Amy Kibatala anayeongozwa na Wakili Peter Kibatala, ambaye anataka Tafsiri ya kifungu 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu kukaa umbali wa mita mia 200 baada ya kupiga kura
Kesi hiyo imeanza kuunguruma mapema Wiki...
9 years ago
Vijimambo22 Oct
Mahakama leo kusikiliza hoja kesi mita 200 vituoni.
![](http://www.itv.co.tz/media/image/Mahakama.jpg)
Katika kesi hiyo namba 37 ya mwaka huu, mlalamikaji anaiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo vyao....
10 years ago
BBCSwahili27 May
Bolt ashinda mita 200
9 years ago
Mtanzania24 Oct
Mita 200 yapigwa marufuku
Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetamka bayana kwamba hairuhusiwi watu kukutana mahali popote bila kujali umbali wake siku ya uchaguzi kesho.
Uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu waliokuwa wakisikiliza mvutano wa kisheria kuhusu kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura.
Mwenyekiti wa jopo hilo, Sekieti Kihiyo na Jaji Lugano Mwandambo kwa nyakati tofauti walipokuwa wakisoma uamuzi huo, walisema wamezingatia hoja zilizowasilishwa na pande mbili...
9 years ago
Habarileo21 Oct
Tume: Kukusanyika mita 200 ni hujuma
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesisitiza kuwa pamoja na kwamba sheria zote za uchaguzi, zinaruhusu mpigakura kukaa umbali wa mita 200 mpaka 300 kutoka kwenye kituo chake cha kupigiakura, umbali huo, hauruhusu watu kukusanyika kwa kisingizio cha kulinda kura.