Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


KESI YA WAPIGA KURA KUKAA MITA 200 YAAHIRISHWA

Wakili Peter Kibatala. MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, imehairisha kesi namba 37 ya mwaka huu, ya mlalamikaji kuiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo. Kesi hiyo sasa itasikilizwa kesho saa 3 asubuhi baada ya upande wa serikali kudai kuwa walikuwa hawajamaliza kujibu hoja au kuweka pingamizi sababu...

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Habarileo

Kesi ya kukaa mita 200 leo

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana imeshindwa kusikiliza kesi kikatiba kuhusu uhalali wa kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupiga kura, kwa kuwa upande wa Jamhuri haujawasilisha utetezi wao.

 

9 years ago

Vijimambo

Kesi mita 200 moto.

Mvutano mkali wa hoja za kisheria ulitikisa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana wakati Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson alipoiomba mahakama itupilie mbali maombi ya walalamikaji katika kesi inayohusiana na umbali wa mita 200 za kusimama kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.

Dk. Ackson alidai mahakamani hapo kuwa maombi ya kesi ya kikatiba ya kutaka tafsiri ya kifungu cha 104 cha Sheria ya Uchaguzi yamewasilishwa na walalamikaji kwa kutumia sheria isiyostahili...

 

9 years ago

Mtanzania

Kesi ya mita 200 kuanza leo

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

JOPO la majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo linatarajia kuanza kusikiliza kesi ya kikatiba kuhusu haki ya mpigakura kukaa umbali wa mita 200 kama ni sahihi au la.

Jopo hilo la majaji Seleman Kihiyo, Aliyisius Mujuluzi na Lugano Mwandambo, liliteuliwa baada ya mgombea ubunge wa Viti Maalumu Jimbo la Kilombero kupitia Chadema, Amy Kibatala, kufungua kesi hiyo kupitia kwa wakili Peter Kibatala.

Katika maombi yake, anaomba Mahakama Kuu ya...

 

9 years ago

StarTV

 Uamuzi kesi wa mita 200  iliyofunguliwa kutolewa Oktoba 23

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imetoa maelekezo  kuwa Oktoba 23 mwaka huu itatoa Uamuzi dhidi ya Kesi iliyofunguliwa ya Kikatiba kuhusu Tafsiri sahihi ya Umbali anaotakiwa kusimama Mpiga kura baada ya kupiga kura.

Kesi hiyo Namba 37 ya Mwaka 2015 iliyofunguliwa na Amy Kibatala anayeongozwa na Wakili Peter Kibatala, ambaye anataka Tafsiri ya kifungu 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu kukaa umbali wa mita mia 200 baada ya kupiga kura

 Kesi hiyo imeanza kuunguruma mapema Wiki...

 

9 years ago

Mtanzania

Mvutano mkali waibuka kortini kesi ya mita 200

Pg 4 oct 22NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MVUTANO mkali wa zaidi ya saa sita umeibuka katika kesi ya kutaka kujua uhalali wa wananchi ama wapigakura kukaa nje ya mita 200 kutoka katika vituo vya kupigia kura na kutaka tafsiri ya mahakama kuhusu kifungu cha sheria ya uchaguzi namba 104(1).

Mvutano huo uliibuka kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wakili wa mleta maombi katika shauri hilo wakati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilipoanza kusikiliza kesi hiyo jana.

Kesi hiyo inayosikilizwa na...

 

9 years ago

Vijimambo

Mahakama leo kusikiliza hoja kesi mita 200 vituoni.

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo itasikiza hoja za upande wa mashtaka na utetezi katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mgombea ubunge Viti Maalum kupitia Chadema, Amy Kibatala, baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha majibu ya kesi hiyo.

Katika kesi hiyo namba 37 ya mwaka huu, mlalamikaji anaiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo vyao....

 

9 years ago

Vijimambo

ESHI LA POLISI MKOANI MWANZA LATOA MSIMAMO WAKE JUU YA SUALA LA MITA 200 BAADA YA KUPIGA KURA

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana ambapo alitoa msimamo wa jeshi hilo juu ya suala la wananchi kubaki mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura siku ya jumapili Octoba 25,2015 ikiwa ni siku ambayo Watanzania watashiriki katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Kuwachagua Wawakilishi wao kuanzia ngazi ya Madiwani, Wabunge na Rais.Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza,...

 

9 years ago

Dewji Blog

Jeshi la Polisi mkoani Mwanza latoa msimamo wake juu ya suala la mita 200 baada ya kupiga kura

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Polisi Charles Mkumbo akiongea na Waandishi wa Habari Ofisini kwake jana ambapo alitoa msimamo wa jeshi hilo juu ya suala la wananchi kubaki mita 200 kutoka vilipo vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura siku ya jumapili Octoba 25,2015 ikiwa ni siku ambayo Watanzania watashiriki katika zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Kuwachagua Wawakilishi wao kuanzia ngazi ya Madiwani, Wabunge na Rais.

Na:George Binagi-GB Pazzo, BMG

Kamanda...

 

5 years ago

Michuzi

WAPIGA KURA WAFIKIA MIL. 30 UBORESHAJI DAFTARI WAPIGA KURA NEC

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu, Semistocles Kaijage akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusu mafanikio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Nec, Dkt.  Wilson Charles Mahera Baadhi ya viongozi  wa Vyama vya Siasa na wadau wengine wakisikiliza kwa makini wakati Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Kaijage akihutubia katika mkutano...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani