Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Kesi ya mita 200 kuanza leo

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

JOPO la majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo linatarajia kuanza kusikiliza kesi ya kikatiba kuhusu haki ya mpigakura kukaa umbali wa mita 200 kama ni sahihi au la.

Jopo hilo la majaji Seleman Kihiyo, Aliyisius Mujuluzi na Lugano Mwandambo, liliteuliwa baada ya mgombea ubunge wa Viti Maalumu Jimbo la Kilombero kupitia Chadema, Amy Kibatala, kufungua kesi hiyo kupitia kwa wakili Peter Kibatala.

Katika maombi yake, anaomba Mahakama Kuu ya...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Habarileo

Kesi ya kukaa mita 200 leo

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, jana imeshindwa kusikiliza kesi kikatiba kuhusu uhalali wa kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupiga kura, kwa kuwa upande wa Jamhuri haujawasilisha utetezi wao.

 

9 years ago

Vijimambo

Mahakama leo kusikiliza hoja kesi mita 200 vituoni.

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo itasikiza hoja za upande wa mashtaka na utetezi katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na mgombea ubunge Viti Maalum kupitia Chadema, Amy Kibatala, baada ya upande wa Jamhuri kuwasilisha majibu ya kesi hiyo.

Katika kesi hiyo namba 37 ya mwaka huu, mlalamikaji anaiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo vyao....

 

9 years ago

Vijimambo

Kesi mita 200 moto.

Mvutano mkali wa hoja za kisheria ulitikisa kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana wakati Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Tulia Ackson alipoiomba mahakama itupilie mbali maombi ya walalamikaji katika kesi inayohusiana na umbali wa mita 200 za kusimama kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.

Dk. Ackson alidai mahakamani hapo kuwa maombi ya kesi ya kikatiba ya kutaka tafsiri ya kifungu cha 104 cha Sheria ya Uchaguzi yamewasilishwa na walalamikaji kwa kutumia sheria isiyostahili...

 

9 years ago

StarTV

 Uamuzi kesi wa mita 200  iliyofunguliwa kutolewa Oktoba 23

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam imetoa maelekezo  kuwa Oktoba 23 mwaka huu itatoa Uamuzi dhidi ya Kesi iliyofunguliwa ya Kikatiba kuhusu Tafsiri sahihi ya Umbali anaotakiwa kusimama Mpiga kura baada ya kupiga kura.

Kesi hiyo Namba 37 ya Mwaka 2015 iliyofunguliwa na Amy Kibatala anayeongozwa na Wakili Peter Kibatala, ambaye anataka Tafsiri ya kifungu 104 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu kukaa umbali wa mita mia 200 baada ya kupiga kura

 Kesi hiyo imeanza kuunguruma mapema Wiki...

 

9 years ago

Mtanzania

Mvutano mkali waibuka kortini kesi ya mita 200

Pg 4 oct 22NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MVUTANO mkali wa zaidi ya saa sita umeibuka katika kesi ya kutaka kujua uhalali wa wananchi ama wapigakura kukaa nje ya mita 200 kutoka katika vituo vya kupigia kura na kutaka tafsiri ya mahakama kuhusu kifungu cha sheria ya uchaguzi namba 104(1).

Mvutano huo uliibuka kati ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wakili wa mleta maombi katika shauri hilo wakati Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilipoanza kusikiliza kesi hiyo jana.

Kesi hiyo inayosikilizwa na...

 

9 years ago

GPL

KESI YA WAPIGA KURA KUKAA MITA 200 YAAHIRISHWA

Wakili Peter Kibatala. MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, imehairisha kesi namba 37 ya mwaka huu, ya mlalamikaji kuiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu cha 104 kidogo cha (1) cha Sheria ya Uchaguzi kama kinazuia ama la wananchi kukaa umbali wa mita 200 baada ya kupiga kura katika vituo. Kesi hiyo sasa itasikilizwa kesho saa 3 asubuhi baada ya upande wa serikali kudai kuwa walikuwa hawajamaliza kujibu hoja au kuweka pingamizi sababu...

 

9 years ago

Mtanzania

Uamuzi mita 200 kutolewa leo

mtz4NA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

JOPO la majaji watatu wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo watatoa uamuzi wa mvutano mkali kuhusu kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura.

Mwenyekiti wa jopo hilo, Sekieti Kihiyo, alisema hayo jana akiwa pamoja na majaji wenzake, Aloycius Mujuluzi na Lugano Mwandambo.

“Jana (juzi) tuliwaambia leo tutatoa maelekezo muhimu, kesho(leo) saa nne tutatoa uamuzi,”alisema Jaji
Kihiyo.

Majaji hao walifikia hatua ya kutoa uamuzi huo baada ya kusikiliza hoja...

 

9 years ago

Habarileo

Hatma ya kesi ya meta 200 kutolewa leo

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo itatoa uamuzi kuhusu shauri la kikatiba lililofunguliwa na Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Amy Kibatala likihoji uhalali wa wapigakura kukaa mita 200 kutoka kwenye vituo vya kupigia kura.

 

10 years ago

BBCSwahili

Bolt ashinda mita 200

Mwanariadha raia wa Jamaica Usain Bolt ameshinda kwa urahis katika shindano lake la kwanza mwaka huu huko barani Ulaya.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani