Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Kesi ya Mwale yaanza kunguruma Arusha

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha juzi, ilianza kusikiliza kesi ya utakatishaji fedha, kula njama na kugushi inayomkabili wakili maarufu nchini, Medium Mwale na wenzake watatu.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Mtanzania

Kesi kupinga ubunge Longido yaanza kunguruma

MMGL2750NA ELIYA MBONEA, ARUSHA

KESI ya kupinga matokeo ya ubunge wa Longido yaliyompa ushindi Onesmo Ole Nangole (Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Stephen Kiruswa, imeanza kusikilizwa.

Nangole ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha, ambaye alitangaza kukihama chama hicho na kujiunga na upinzani, aligombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu na kufanikiwa kushinda.

Kesi hiyo iliyopo mbele ya Jaji Methew Mwaimu, jana  ilianza kusikilizwa...

 

11 years ago

Tanzania Daima

Mawakili kesi ya Mwale waja juu

MAWAKILI wa utetezi kwenye shauri la utakatishaji fedha linalowakabili washitakiwa wanne akiwemo wakili maarufu, jijini hapa, Median Mwale, wameibua hoja juu ya uhalali wa kutumika kwa sheria ya kuzuia utakatishaji...

 

9 years ago

Habarileo

Malumbano ya kisheria yatawala kesi ya Mwale

MALUMBANO ya kisheria yameibuka jana baina ya mawakili upande wa Serikali na utetezi katika kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili washtakiwa wanne akiwemo wakili maarufu wa jijini Arusha, Median Mwale hali iliyosababisha Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kuendesha kesi ndani ya kesi.

 

11 years ago

Habarileo

Wakili: Kesi ya Mwale ilifunguliwa kimakosa

UPANDE wa utetezi kwenye kesi ya wakili maarufu jijini hapa, Median Mwale na wenzake watatu ya kutakatisha fedha haramu, umedai mashitaka hayo dhidi ya washitakiwa, yalifunguliwa kimakosa kabla ya sheria iliyowashitaki kutungwa.

 

9 years ago

Habarileo

Serikali yakata rufaa kesi ya wakili Mwale

 MAWAKILI wa serikali wamekata rufaa Mahakama ya Rufaa baada ya Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Gadi Mjemas anayesikiliza kesi ya wakili maarufu Median Mwale na wenzake watatu, kukataa baadhi ya vielelezo vya ushahidi kutoka nchini Marekani ikiwamo hati saba za viapo.

 

9 years ago

Mtanzania

Kesi ya Wakili Mwale yahamia Mahakama Kuu

NA JANETH MUSHI, ARUSHA

MAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Kanda ya Arusha, inatarajia kuanza kusikiliza kesi ya utakatishaji fedha haramu inayomkabili wakili maarufu jijini hapa, Median Mwale na wenzake watatu.

Hatua hiyo ilikuja jana baada ya upande wa Jamhuri unaowakilishwa na Wakili Oswald Tibabyakomya, kudai kuwa umekamilisha upelelezi wa kesi hiyo.

Watuhumiwa wengine katika shauri hilo ni Don Bosco Gichana, Boniface Mwimbwa na Elias Ndejembi.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi Mkazi wa Mahakama ya Hakimu...

 

10 years ago

Mtanzania

Jaji Msengi Kusikiliza kesi ya Wakili Mwale

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

KESI ya utakatishaji fedha haramu inayomkabili wakili maarufu jijini Arusha, Medium Mwale na wenzake watatu, imeanza kusikilizwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha mbele ya Jaji Fatuma Masengi.
Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwishoni mwa wiki baada ya Jamhuri kwa kuongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Oswald Tibabyekomya, kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali ya mashtaka 42 yanayowakabili.
Tibabyekomya alidai washtakiwa wote walikubali majina yao kuwa Median Mwale, Don...

 

10 years ago

Habarileo

Kesi ya Ponda kunguruma Februari 16

KESI inayomkabili kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini Shehe Ponda Issa Ponda jana imeahirishwa hadi Februari 16, mwaka huu kwa mashahidi wa upande wa mashitaka kuendelea kutoa ushahidi mahakamani.

 

10 years ago

Mwananchi

Kesi ya Badwell kunguruma tena Feb 24

Mbunge wa Bahi, Dodoma, Omary Badwel anayekabiliwa na kesi ya kuomba na kupokea rushwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, Februari 24 mwaka huu, anatarajiwa kuhojiwa na upande wa mashtaka dhidi ya utetezi wake alioutoa mahakamani hapo.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani