Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Majambazi waua 7 kituo cha Polisi

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na waandishi wa habari alipowasili kukagua Kituo cha Polisi Sitaki Shari Ukonga, Dar es Salaam jana baada ya kuvamiwa na majambazi wanaodaiwa kupora silaha kituoni hapo juzi usiku. Askari wanne na raia watatu waliuawa katika tukio hilo. Kulia kwake ni Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova. (Na Mpigapicha Wetu).ASKARI wanne na raia watatu wameuawa baada ya watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kuvamia Kituo cha Polisi cha Sitakishari kilichopo Ukonga katika Manispaa ya Ilala, Dar es Salaam.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

CloudsFM

Majambazi wavamia kituo, waua polisi wawili

ASKARI wawili wa Jeshi la Polisi katika Kituo cha Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani Pwani, wameuawa baada ya kushambuliwa kwa silaha na majambazi, waliovamia kituo hicho na kuiba silaha baada ya kufanikisha mauaji.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi liko katika msako mkali, huku Mkuu wa jeshi hilo, IGP, Ernest Mangu akitangaza donge nono la Sh milioni 20 kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo na silaha.

Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu kutoka eneo la...

 

10 years ago

Habarileo

Majambazi waua polisi 2 kizuizi cha Dar, Pwani

Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman KovaASKARI wawili wa Jeshi la Polisi waliokuwa kazini eneo la kizuizi cha polisi cha kijiji cha Kipara Mpakani Vikindu wilayani Mkuranga mkoani Pwani, wameuawa na majambazi na kuporwa silaha.

 

10 years ago

Vijimambo

MAJAMBAZI WALIOVAMIA KITUO CHA POLISI CHA STAKISHARI, WAKAMATWA

Jeshi la polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limefanikiwa kuwakamata majambazi watano wanaodaiwa kuhusika na tukio la uvamizi katika kituo cha polisi cha Stakishari kilichopo Ukonga.Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema Majambazi hao wamekamatwa Mbagala ambapo katika tukio hilo pia wamekamata pia fedha shilingi milioni 170 na bunduki 16 miongoni mwao ni zile zilizoibiwa katika kituo cha Stakishari.

 

11 years ago

Mwananchi

Majambazi yateka kituo cha polisi, yaua

Hili linawezekana kuwa ni tukio la kwanza na la aina yake. Majambazi wanaokisiwa kuwa sita, wakiwa na pikipiki tatu, juzi walivamia Kituo Kidogo cha Polisi Mkamba kilichopo Kimanzichana, Wilaya ya Mkuranga, Pwani na kuua askari mmoja na mgambo na kujeruhi mgambo mwingine na kisha kupora bunduki tano na risasi 60 usiku wa kuamkia juzi.

 

10 years ago

GPL

KITUO CHA POLISI IKWIRIRI CHAVAMIWA NA MAJAMBAZI, ASKARI WAWILI WAUWAWA

MAJAMBAZI yaliyojihamu kwa silaha yamevamia Kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua askari wawili na kupora silaha zilizokuwepo kituoni hapo. Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar aliyekatwa mapanga na WP Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto. Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku...

 

10 years ago

Michuzi

MWILI WA MMOJA WA ASKARI WALIOUAWA NA MAJAMBAZI KITUO CHA POLISI STAKISHARI WAAGWA

Jeneza lenye mwili wa marehemu Koplo Gaudin Kakoko, likiwa  nyumbani kwa marehemu, Majohe, Ilala Jijini Dar es Salaam tayari kwa mwili wa marehemu kuagwa na wapendwa wake,Mwili huo ulisafirishwa jana kupelekwa kwao wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera kwa mazishi.Marehemu ni mmoja wa askari wanne waliouawa na majambazi hivi majuzi baada ya kukivamia kituo cha polisi Stakishari, Ukonga, Ilala Jijini Dar es Salaam, Mungu ailaze roho ya marehemu wote mahali pema peponi.Baadhi ya waombolezaji wakiwa...

 

11 years ago

Michuzi

News Alert: Majambazi wavamia kituo cha Polisi Kimanzichana na kuua Askari

Mnamo tarehe 11/06/14 majira ya 0100hrs huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani,watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kimanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada. 
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha aina ya SMG ikiwa na risasi 30.
Ndipo...

 

10 years ago

Mwananchi

Majambazi yateka kituo cha polisi, yaua askari wawili, yapora SMG tano

WATU 15 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za kivita na mabomu ya kurushwa kwa mkono wamevamia kituo cha polisi Ikwiriri  wilayani Rufiji Mkoani Pwani na kuua askari polisi wawili na kupora silaha tano za SMG na mbili za kufyatulia mabomu ya machozi zilizokuwepo kituo hapo na kutokomea kusikojulikana.

 

10 years ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZZ.....: KITUO CHA POLISI IKWIRIRI,RUFIJI CHAVAMIWA NA MAJAMBAZI,ASKARI WAWILI WAUWAWA

Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii asubuhi hii,inaeleza kuwa majambazi yamevamia kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji mkoani Pwani na kuua Askari wawili na kupora silaha (bunduki) zilizokuwepo kituoni hapo.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo,huku askari wanaodaiwa kupotenza maisha ni Cop. Edgar  aliyekatwa mapanga na Wp Judith aliyepigwa risasi ubavuni upande wa kulia na kutokea upande wa kushoto.
 Hivi sasa hali ni tete katika eneo hilo na watu wamekusanyika huku polisi wakiongeza...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani