Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Mauaji yazidi kutikisa Kiteto....Waliopoteza uhai Wafikia 7

Mapigano baina ya wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto mkoani Manyara, yameendelea tena, ambapo watu wengine wawili wamefariki dunia jana na kufanya idadi ya waliouawa kuwa saba. Awali, Novemba 11, mkulima Hassan Kondeja mkazi wa Kitongoji cha Bwawani Kijiji cha Matui aliuawa kwa kukatwa shingo na wafugaji na ndipo yakatokea mauaji ya wakulima wawili na wafugaji wawili. Akizungumza na mwandishi wetu, Kamanda wa polisi wa Mkoa Manyara, SACP Deusdedit Nsimeki alisema wakulima wawili wameuawa...

Vijimambo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Mauaji yazidi kutikisa Kiteto

Mapigano baina ya wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto mkoani Manyara, yameendelea tena, ambapo watu wengine wawili wamefariki dunia jana na kufanya idadi ya waliouawa kuwa saba.

 

11 years ago

Mwananchi

Mauaji yazidi kutikisa Tarime

Hali ya usalama Tarime imezidi kutoweka baada ya jambazi lisilofahamika likiwa na bunduki ambayo haijafahamika aina yake kuendelea kuua watu kwa risasi hasa wa jinsi ya kiume, ambapo idadi ya waliouawa imefikia saba hadi sasa na inadaiwa huwaua watu na kupotea bila kutambuliwa.

 

11 years ago

Mwananchi

Mabomu yazidi kutikisa Arusha

>Milipuko ya mabomu nchini inazidi kuongezeka baada ya bomu jingine kulipuka mjini Arusha na kujeruhi vibaya watu wanane wenye asili ya Kiasia katika mgahawa wa Vama Traditional Indian Cuisine ulioko eneo la Arusha Gymkhana.

 

10 years ago

Uhuru Newspaper

Mauaji ya Kiteto yalitikisa Bunge


JESHI Polisi linawashikilia watu watano kuhusiana na mauaji katika mapigano kati ya wafugaji na wakulima katika kijiji cha Matui wilayani Kiteto.
Katika mapigano hayo, watu wanne waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Akitoa kauli ya serikali bungeni jana, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mathias Chikawe, alisema mapigano hayo yalitokea juzi katika wilaya hiyo.
Chikawe alisema Jumanne iliyopita katika kijiji hicho, mkulima Hassan Kondeja, mkazi wa Kijiji cha Bwawani, alikwenda katika Kituo cha...

 

9 years ago

Mtanzania

Magufuli: Nachukia mauaji ya Kiteto

g jpg*Asema hayupo tayari kuongoza Serikali inayovuja damu

 

Na Bakari Kimwanga, Kongwa

MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amesema amechoka kusikia mauaji ya wakulima na wafugaji wilayani Kiteto.

Mgombea huyo alisema akichaguliwa kuwa rais atashughulika na Mkuu wa Mkoa (RC) na Mkuu wa Wilaya (DC), atakaowateua iwapo mauaji hayo yataendelea.

Alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) atakayeteuliwa anapaswa kujipanga vizuri kusimamia amani katika eneo hilo la sivyo...

 

10 years ago

Tanzania Daima

Mauaji ya Kiteto, Siha yakome

KWA muda mrefu kumekuwa na taarifa kwenye vyombo vya habari kuhusu ugomvi kati ya wakulima na wafugaji wanaogombania maeneo hapa nchini Ugomvi wa pande hizo mbili zimekuwa zikisababisha vifo, majeraha,...

 

10 years ago

Tanzania Daima

Mauaji kiteto kujadiliwa Bungeni

BUNGE limepeleka kamati ndogo, chini ya uongozi wa Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, kwenda kuchunguza mauaji ya kutisha yanayoendelea kutokea wilayani Kiteto mkoani Manyara. Hatua hiyo ilitangazwa jana Bungeni...

 

11 years ago

Tanzania Daima

Mauaji ya wakulima tena Kiteto

MAPAMBANO kati ya wakulima na wafugaji katika Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, yanaendelea kushika kasi na kusababisha watu wanne kupoteza maisha. Hali hiyo ilibainishwa na Katibu wa wakulima wilayani hapa,...

 

11 years ago

Tanzania Daima

DC adaiwa kuchochea mauaji Kiteto

MKUU wa Wilaya (DC) ya Kiteto mkoani Manyara, Martha Umbulla, amedaiwa kuwa chanzo cha kuchochea mauaji ya wakulima na wafugaji. Madai hayo yalitolewa na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani