Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


MH. ANGELA KAIRUKI AFUNGA RASMI MKUTANO WA KIKANDA WA UKUAJI WA MAISHA YA BAADAE KWA MIJI YA AFRIKA MASHARIKI

Mkutano wa kikanda juu ya ukuaji na maisha ya baadae ya miji ya Afrika mashariki ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI INSTITUTE) umefungwa rasmi leo na Naibu waziri wa Nyumba na maendeleo ya makazi Mhe.  Angela Kairuki katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es salaam.
Mkutano huo wa siku mbili uliohudhuriwa na wawakilishi wa ngazi za juu kutoka serikalini, mashirika ya kikanda na kimataifa, miji mikubwa, wasomi, sekta binafsi na asasi za kiraia...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

WAZIRI MKUU KUFUNGUA MKUTANO WA KIKANDA JUU YA UKUAJI NA MAISHA YA BAADAE YA MIJI YA AFRIKA

Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) imeandaa  mkutano  wa kikanda  utakaokutanisha viongozi na watunga sera  kutoka  nchi  za Afrika mashariki kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadaye ya miji ya Afrika.
Mkutano huu uliopewa jina la, ‘Maisha ya baadae ya nchi za Afrika Mashariki: Jinsi gani tunataka kuishi mwaka 2050’, utafanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, Kilimanjaro Hotel tarehe 19 na 20 Februari ambapo...

 

10 years ago

Michuzi

Balozi Seif Ali Idd afungua mkutano wa kikanda wa Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,jijini Dar leo

 Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd (wa pili kushoto) akiwa katika meza kuu pamoja na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI,Mh. Hawa Ghasia (kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Mh. Said Meck Sadick (wa pili kulia),Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi,Prof. Joseph Sembojo (katikati) pamoja na Dkt. Remy Sietchiping kutoka UN-Habitat wakati wa Mkutano wa Kikanda uliojadili Ukuaji wa maisha ya baadae kwa miji ya Afrika,uliofanyika leo kwenye...

 

10 years ago

Dewji Blog

Waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda kufungua mkutano wa kikanda juu ya ukuaji na maisha ya baadae ya miji ya Afrika

Mizengo-Pinda

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda (Mb).

Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) imeandaa  mkutano  wa kikanda  utakaokutanisha viongozi na watunga sera  kutoka  nchi  za Afrika mashariki kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadaye ya miji ya Afrika.

Mkutano huu uliopewa jina la, ‘Maisha ya baadae ya nchi za Afrika Mashariki: Jinsi gani tunataka kuishi mwaka 2050’, utafanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam,...

 

10 years ago

Dewji Blog

Kairuki afunga mkutano wa ukuaji wa miji Afrika Mashariki

1

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya makazi,Mhe:Angela Kairuki, akiongea na Viongozi na watunga Sera kutoka Nchi za Afrika Mashariki wakati wa kufunga Mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI INSTITUTE) uliozungumzia changamoto za ukuaji wa miji na jinsi gani tungependa kuishi ifikapo 2050. Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Hyatt Regency zamani Kilimanjaro-jijini Dar es Salaam.

2

3

Afisa mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi...

 

10 years ago

Dewji Blog

Balozi Iddi afungua rasmi mkutano wa kikanda juu ya ukuaji wa miji ya Afrika Mashariki

1

Afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uongozi wa Afrika kwa Maendeleo Endelevu (UONGOZI Institute) Prof. Joseph Semboja, (Kulia) akimkaribisha Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mh. Balozi Seif Ali Iddi, (kushoto) kufungua rasmi Mkutano wa kikanda uliokutanisha viongozi na watunga sera kutoka nchi za Afrika mashariki, kuzungumzia changamoto za ukuaji wa miji na kushughulikia hali ya baadae ya miji ya Afrika mpaka ifikapo 2050, katikati ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick....

 

10 years ago

Michuzi

Waziri Membe afunga rasmi kongamano la wadau wa habari ukanda wa Afrika Mashariki.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akisisitiza jambo kwa wadau mbalimbali wa habari toka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki mapema hii leo wakati akifunga kongamano la siku mbili la wadau wa habari liloandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki lenye lengo la kuangalia mchango wa vyombo vya habari katika kukuza demokrasia katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki. Mhariri wa gazeti la Hoja toka nchini Tanzania Bw. Yassin Sadik  akichangia mada wakati wa kufunga...

 

10 years ago

Michuzi

Naibu Waziri wa Ardhi Mh. Angela Kairuki afungua mkutano wa 'Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia'

 Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. Angela Kairuki ambaye alikuwa mgeni rasmi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa ‘Viongozi Wanawake Vijana Wanaochipukia’ uliondaliwa na Taasisi ya UONGOZI kwa kushirikiana na Mfuko wa Wanawake Tanzania mapema leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulilenga kuzungumzia suala la wanawake na uongozi, na namna ya kutatua changamoto wanazozipata katika kufanikisha ndoto zao za kiuongozi katika sekta mbali mbali nchini.
 Afisa Mtendaji...

 

9 years ago

Dewji Blog

Albamu ya nyimbo za Injili ya Sogea na Baraka za Bwana zazinduliwa rasmi jijini Dar na Mhe. Angela Kairuki

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi, Angela Kairuki (kushoto), akionesha DVD ya nyimbo za injili iitwayo Sogea wakati wa uzinduzi wa albamu mbili za nyimbo hizo ikiwepo na ya Baraka za Bwana zilizoimbwa na muimbaji Anna Shayo Dar es Salaam juzi. Kulia ni Mwanaharakati Hoyce Temu na mwimbaji na mmiliki wa albam hizo, Anna Shayo. Kairuki alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo.

2

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi, Angela Kairuki...

 

10 years ago

Vijimambo

WAZIRI MEMBE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akifungua rasmi Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam tarehe 30 Mei, 2015. Mkutano huo ambao ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC utakaofanyika tarehe 31 Mei, 2015, pamoja na mambo mengine utapokea na kujadili taarifa zitakazowasilishwa na Jopo la Watu Maalum wanaofuatilia...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani