Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Mwigulu: auchungulia urais

SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM
KASI ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutangaza nia ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu, imezidi kuongezeka baada ya Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, kuonyesha nia ya kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Mwigulu ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, alionyesha nia hiyo huku akitumia nukuu za mitume, akiwamo Yesu Kristo kupitia kitabu kitakatifu cha Biblia.
Mwigulu alionyesha nia hiyo jana, akiwa...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Mwigulu afunguka urais

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema ameanza kuchangiwa fedha na Watanzania wanaoishi ughaibuni ili zimsaidie iwapo ataamua kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwakani.

 

10 years ago

Habarileo

Mwigulu na Wassira wakoleza mbio za Urais

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, akitangaza nia ya kuomba kuchaguliwa na CCM kugombea urais mwaka huu.MAKADA wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mwigulu Nchemba na Stephen Wassira wametangaza rasmi nia yao ya kutaka kuwania kupitishwa na chama hicho, kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

10 years ago

Michuzi

MWIGULU ACHUKUA FOMU YA KUWANIA URAIS


Mh.Mwigulu akiwasili makao makuu ya CHAMA CHA MAPINDUZI mjini Dodoma kwaajili ya Kuchukua Fomu ya Kuwania Urais wa Tanzania mwaka 2015.

Mh:Mwigulu akisaini kitabu cha Wagombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

 

10 years ago

Mtanzania

Zitto, Mwigulu waungana urais 2015

mwigilu nchembaNa Mwandishi Wetu
WANASIASA wawili vijana ambao wamejijengea umaarufu wa kisiasa ndani ya makundi mbalimbali ya kijamii hapa nchini wameunganisha nguvu zao za kusaka ukuu wa dola katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Wanasiasa hao, Zitto Kabwe ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi na pia Naibu Waziri wa Fedha ambao jana walialikwa kushiriki mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa...

 

10 years ago

GPL

URAIS 2015: JANUARI VS MWIGULU NGOMA NZITO!

Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, January Makamba (41). HOMA ya Uchaguzi Mkuu 2015 inazidi kupanda. Wapo baadhi ya wagombea wa urais ambao tayari wameshatangaza nia hadharani lakini wengine wanaendeleza harakati zao chini kwa chini.
Miongoni mwa makada ambao tayari wameonesha nia ya kutaka kugombea ni pamoja na vijana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba (40) na Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na...

 

10 years ago

Mtanzania

Wasira, Mwigulu nao wajitosa urais CCM

MWIGULUWASIRA muda huuHEKAHEKA za kuwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mgombea urais zinazidi kupamba moto baada ya makada wengine wawili, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba kutangaza kujitosa katika mbio hizo jana.
Wakati Wasira akitangaza kuhakikisha analeta mageuzi mpya kwa taifa, Mwigulu ameahidi Watanzania kuumiliki uchumi.
Wasira ambaye ni Mbunge wa Bunda, amekuwa ni kada wa pili huku Mwigulu akiwa wa tatu kutangaza nia ya kuwania...

 

10 years ago

Mtanzania

Zitto, Mwigulu wang’ara urais 2015

Zitto-KabweNa Asifiwe George, Dar es Salaam
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) ameng’ara katika mbio za urais mwaka 2015 akipata asilimia 18 tofauti na wagombea wengine wanaotajwa kugombea nafasi hiyo kupitia muungano wa vyama vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), utafiti umebaini.
Takwimu hizo zilitolewa na Asasi ya Utafiti wa Elimu Tanzania ( TEDRO) kwa lengo la kutathmini ushiriki wa vijana katika siasa kama wagombea na namna ambavyo vijana wanavyopokewa katika...

 

10 years ago

KwanzaJamii

MWIGULU NCHEMBA: NIMEOMBWA NA WAZEE NIGEMBEE URAIS 2015

Wakati baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea kupigana vikumbo kuwania urais wa 2015, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, amesema ameombwa na watu mbalimbali wakiwamo wazee na wasomi kuwania nafasi hiyo. Hata hivyo, Nchemba amesema kwa sasa hafikirii suala hilo kwani amebanwa na utekelezaji wa jukumu alilokabidhiwa na Rais. Nchemba, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, aliyasema hayo jana wakati akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni...

 

10 years ago

GPL

MWIGULU NCHEMBA NAYE ATANGAZA NIA YA KUWANIA URAIS

Mwigulu Nchemba akitangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea Urais kupitia CCM jioni hii mkoani Dodoma. NAIBU Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ametangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea Urais jioni hii kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiwa katika Ukumbi wa Mwl. Nyerere uliopo kwenye Chuo cha Mipango mkoani Dodoma. Kauli mbiu ya Mwigulu ni ‘Mabadiliko ni Vitendo Wakati ni Sasa.’ Katika hotuba yake Mwigulu ameanza...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani