Mzee Moyo afukuzwa CCM
NA SARAH MOSSI, ZANZIBAR
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimemfukuza uanachama mmoja wa waasisi wa chama hicho Visiwani, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Hatua hiyo ilitangazwa jana na Katibu wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja, Aziza Iddi Mapuri katika taarifa aliyoitoa kwa vyombo vya habari mjini hapa.
Mapuri alisema Mzee Moyo anadaiwa kukisaliti chama hicho kwa kukiuka maadili na kutoa matamshi yasiyokubaliana na sera za chama chao.
Alisema Mzee Moyo alitumia majukwaa ya siasa katika mikutano...
Mtanzania
Habari Zinazoendana
10 years ago
Habarileo20 Apr
Nassor Moyo afukuzwa CCM
MWANASIASA mkongwe na kada wa CCM aliyepata kushika nyadhifa mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwaziri, Mzee Hassan Nassor Moyo amefukuzwa uanachama wa chama hicho ambacho yeye ni mmoja wa waasisi wake, akiwa mwanachama namba 7.
10 years ago
Vijimambo20 Apr
Zanzibar yatibuka.CUF wafurushwa kwa mabomu, Nassoro Moyo afukuzwa CCM.
![](http://www.ippmedia.com/media/picture/large/Idd-20April2015.jpg)
Jeshi la Polisi Zanzibar, limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) waliokuwa wakikaidi amri ya kutotoka wilaya moja kwenda nyingine kuhudhuria mkutano wa hadhara. Inakumbukwa kwamba baada ya wafuasi wa CUF kushambuliwa mwishoni wa mwezi uliopita wakitoka katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Makunduchi, Mkoa wa Kusini Unguja, polisi waliitisha mkutano nabaadhi ya vyama vya siasa na...
11 years ago
Mwananchi25 Apr
Mzee Moyo awataka CCM wajipime
10 years ago
Mtanzania21 Apr
Mzee Moyo: Sijutii kufukuzwa CCM
Na Is-haka Omar, Zanzibar
WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Ndani mstaafu, Mzee Nassor Moyo, amesema hajutii kufukuzwa uanachama ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na hatarajii kukata rufaa.
Akizungumza na MTANZANIA mjini hapa jana, Moyo alisema ataendelea kuwa muumini wa Serikali tatu na kudai mamlaka kamili ya Zanzibar hadi mwisho wa maisha yake.
Alisema anaamini kile anachosimamia ndani ya moyo wake, hivyo hakuna chama wala taasisi yoyote yenye uwezo wa kubadilisha kile anachokiamini kusimamia...
5 years ago
Michuzi![](https://1.bp.blogspot.com/-LXQV7xrGDUY/XlkmyrboPkI/AAAAAAALf6M/xB4uQ_8dtdAoicveNoK1EQ85-Q0BiKHLACLcBGAsYHQ/s72-c/Benard.jpg)
MEMBE AFUKUZWA CCM
![](https://1.bp.blogspot.com/-LXQV7xrGDUY/XlkmyrboPkI/AAAAAAALf6M/xB4uQ_8dtdAoicveNoK1EQ85-Q0BiKHLACLcBGAsYHQ/s640/Benard.jpg)
WAZIRI wa zamani wa Mambo ya Nje, Bernard Membe amevuliwa uanachama pamoja na madaraka na kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) hapa nchini
Hayo ameyasema, Katibu mwenezi wa chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole leo Februari 28, 2020 wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi ndogo za Chama cha Mapinduzi (CCM),Lumumba jijini Dar es Salaam, wakati Membe akivuliwa uanachama, katibu mkuu wa zamani wa chama cha CCM, Abdulrahman Kinana amepewa onyo na kutokugombea nafasi...
9 years ago
Mzalendo Zanzibar18 Oct
Kama mzee Moyo, ameyaona Kingunge
Jabir Idrissa NANI katika CCM waliopo sasa, akiwemo Mwenyekiti wao Jakaya Mrisho Kikwete, makamu Philip Mangula na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana, anayekijua kwa ufasaha chama hiki – asili yake, itikadi yake, sera yake, malengo yake – […]
The post Kama mzee Moyo, ameyaona Kingunge appeared first on Mzalendo.net.
10 years ago
Mwananchi23 Apr
Mzee Moyo: Walionifukuza ni watoto wasiojua kitu
10 years ago
Vijimambo![](http://img.youtube.com/vi/goTXSRxDNEI/default.jpg)
10 years ago
Mtanzania24 Apr
Mzee Moyo: Sina mpango kujiunga chama chochote
Na Elizabeth Hombo, aliyekuwa Tanga
MWASISI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mapinduzi ya Zanzibar, Nassor Hassan Moyo amesema hafikirii kujiunga na chama chochote cha siasa, baada ya kuvuliwa uanachama wa CCM.
Wiki iliyopita, Katibu wa CCM Mkoa wa Magharibi Unguja, Aziza Iddi Mapuri alitangaza kumfukuza mwanasiasa huyo mkongwe kwa madai ya kukisaliti kwa kukiuka maadili na kutoa matamshi yasiyokubaliana na sera za chama chake.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na MTANZANIA nyumbani kwake...