Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Nchi 16 wamzika Brigedia Jenerali Mbita

Na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

VIONGOZI wa nchi mbalimbali za Afrika jana walijitokeza kuaga mwili wa aliyekua katibu mtendaji wa kamati ya ukombozi kusini Afrika, Brigedia Jenerali Hashim Mbita katika Hosipitali ya jeshi ya Lugalo, Dar es salaam.

Mbali na nchi hizo, Rais Jakaya Kikwete aliongoza kuaga mwili wa marehemu Mbita akifuatana na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda pamoja na viongozi waandamizi wa jeshi na vyama vya siasa.
Mwili wa Mbita uliagwa jana...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mtanzania

Brigedia Jenerali Mbita kuzikwa leo

mbitaAdam Mkwepu na Easther Mnyika, Dar es Salaam
ALIYEKUWA Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Brigedia Jenerali mstaafu Hashim Mbita (82), anatarajiwa kuzikwa leo jijini Dar es Salaam.
Mbita aliyefariki dunia Mei 26, mwaka huu katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, anatarajiwa kuzikwa leo alasiri katika makaburi ya Kisutu.
Kifo cha mpigania uhuru huyo wa nchi za Afrika kimewagusa viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali ambapo Katibu Mkuu wa Chama...

 

10 years ago

GPL

HATIMAYE BRIGEDIA JENERALI MBITA AZIKWA

Mwili wa Brigedia Jenerali Hashim Mbita ukiswaliwa Msikitini. Mwili wa Marehemu Mbita ukiingizwa kwenye gari maalum la Jeshi kwa ajili ya kupelekwa makaburi ya Kisutu Dar kwa maziko.…

 

10 years ago

Mtanzania

Brigedia Jenerali Mbita afariki dunia

mbitaJonas Mushi na Patricia Kimelemeta, Dar es Salaam

MMOJA wa Watanzania waliofanikisha ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika,Brigedia Jenerali Hashim Mbita (82), alifariki dunia jana katika Hospitali Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lugalo ambako alikuwa amelazwa kwa muda mrefu.

Akizungumza na MTANZANIA nyumbani kwa marehemu Chang’ombe Madukani Dar es Salaam jana, mtoto wa marehemu Iddi Mbita alisema baba yake alifariki dunia saa 3:30 asubuhi baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu...

 

10 years ago

Mwananchi

JK aongoza mamia kumzika Brigedia Jenerali Mbita

Dar es Salaam. Mamia ya waombolezaji wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete jana walijitokeza katika Makaburi ya Kisutu jijini hapa kuuzika mwili wa Brigedia Jenerali Hashim Mbita aliyefariki dunia mwanzoni mwa wiki hii.

 

10 years ago

Michuzi

Rais Kikwete atoa heshima za Mwisho kwa Brigedia Jenerali Hashim Mbita

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Afrika (OAU) marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo. Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho(picha na Freddy Maro).

 

10 years ago

Vijimambo

BRIGEDIA JENERALI ( MSTAAFU ) HASHIM MBITA AZIKWA MAKABURI YA KISUTU, JIJINI DAR

Viongozi mbali mbali wa Dini ya Kiislam wakishiriki pamoja na waumini wao kwenye Ibada ya kuuswalia mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na baadae kwenda kuuhifadhi kwenye nyumba yake ya milele, Makaburi ya Kisutu, Jijini Dar es Salaam. Picha zote na Hamis Makuka.Maelfu ya waunini wa kiislam wakishiriki kuubeba mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita wakati wakiutoa kwenye Msikiti wa Mtoro, Kariakoo na tayari kwa kwenda...

 

10 years ago

Michuzi

MH. MEMBE AKABIDHI HUNDI YA DOLA LAKI 1 KWA FAMILIA YA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard K. Membe (Mb) (katikati) akikabidhi hundi yenye thamani ya Dola za Marekani laki moja kwa mtoto wa Brigedia Jen. Mstaafu Hashim Mbita, Bibi Shella Mbita. Bibi Mbita alipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Baba yake ambayo imetolewa na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Robert Mugabe kutokana mchango mkubwa alioutoa Brig. Jen. Mbita katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika. Mwingine katika picha ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe....

 

10 years ago

Michuzi

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU HASHIM MBITA LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.  Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro,  baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.  Rais Jakaya Mrisho Kikwete...

 

10 years ago

Vijimambo

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU HASHIM MBITA HOSPITALI YA LUGALO

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita aliyelazwa akipata matibabu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaaam jana.Brigedia Jenerali Hashim Mbita ni mwanasiasa mkongwe ambaye aliwahi kuwa  mmoja wa viongozi waandamizi katika harakati za ukombozi Barani Afrika Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita aliyelazwa akipata matibabu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaaam...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani