Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


news alert: ankal anunua ndege kuondokana na adha ya foleni jijini dar es salaam

Ankal akijiandaa kuingia ndani ya ndege yake ndogo inayoweza kutua popote aliyoinunua hivi karibuni kutoka katika visiwa vya Ushelisheli (Seychelles Islands) ili kuepukana na adha ya foleni jijini Dar es salaam.  Ankal ameiambia Globu ya Jamii kwamba amekuwa akisomea urubani wa ndege hiyo kwa siri kwa mwaka mmoja na sasa ameshatimiza  masaa 450 hewani na tayari ameshapata leseni ya kupaa katika jiji la Dar (mchana tu, kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni) na kutua katika viwanja...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

Michuzi

News Alert: Helkopta ya Polisi yapiga mweleka wakati wa Kuruka kwenye Uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere jijini Dar leo

Helkopta ya Jeshi la Polisi Tanzania ikiwa imepiga mweleka mapema leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere mara baada ya kupatwa na hitilafu ya kiufundi wakati wa ikitaka kuruka.Taarifa za uhakika kabisa zilizoifikia Globu ya Jamii,zinaeleza kuwa Helkopta hiyo ilishindwa kuruka kwa kwenda mbele na badala yake iiliruka kwa kurudi nyuma,hali iliyopelekea Panga la Helkopta hiyo kujipigiza kwenye moja ya Paa la Karakana la Uwanjani hapo na kupiga mweleka.Hakuna aliedhulika...

 

10 years ago

Michuzi

News Alert: membe akutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi jijini Dar es salaam leo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), leo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Laurent Kavakure jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro. Mhe. Kavakure aliwasili nchini tarehe 03 Mei 2015. Wakati huo huo, Mhe. Membe ataongoza ujumbe wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenda Burundi siku ya Jumatano tarehe 06 Mei 2015 kufanya mazungumzo na Serikali ya...

 

11 years ago

Michuzi

news alert: wawili wahukumiwa faini shilingi milioni 15 ama jela miaka 15 kwa ujenzi wa jengo la ghorofa 18 jijini dar es salaam

Watu  wawili wamehukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni 15 au kwenda jela miaka miaka 15 baada ya kupatikana na hatia ya makosa matano ya ujenzi wa jengo la ghorofa 18 lililojengwa jirani na Ikulu lililopo mtaa wa Chimala Kitalu cha 45 na 46, kinyume cha sheria. 
 Washtakiwa hao ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na aliyekuwa Msanifu Mkuu wake Richard Maliyaga (55) wote wakazi wa jijini Dar es Salaam. 
 Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mkazi Sundi...

 

10 years ago

Michuzi

10 years ago

Michuzi

NEWS ALERT: NDEGE YA JWTZ YAPATA AJALI JIJINI MWANZA LEO

Ndegevita moja ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ikiteketea kwa moto huku jitihada za kuuzima zikiendelea katika ajali iliyotokea leo Februari 27, 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa MwanzaJeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kutoa taarifa ya ajali ya Ndegevita moja (1) iliyotokea leo tarehe 27 Februari 2015 katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Mwanza.
Ndegevita za JWTZ zilikuwa katika mazoezi ya kawaida ya kivita,  Wakati rubani wa ndegevita...

 

11 years ago

Michuzi

libeneke la foleni za magari kutoka angani jijini dar es salaam

 Huo msalaba uuonao hapo ni taa za magazri zilizo katika foleni mishale ya saa moja jioni kwenye makutano ya barabara za Morogoro road na Nelson Mandela jijini Dar es salaam. Hakika kuna haja ya kutafuta njia mbadala za kupunguza foleni ya magari katika jiji hili. Ushauri wa bure kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Madiwani wa Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni. Boresheni njia za pembeni ili magari yaweze kupungua katika barabara hizi kuu. 
Picha na Sultani Kipingo wa Globu ya Jamii

 

10 years ago

Michuzi

NEWS ALERT: WATU KADHAA WAUWAWA, SILAHA ZAPORWA BAADA YA MAJAMBAZI KUVAMIA KITUO KIDOGO CHA POLISI CHA SITAKISHARI, UKONGA, JIJINI DAR ES SALAAM USIKU HUU

Habari zilizotufikia chumba cha habari  zinasema kwamba watu kadhaa wameuwawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, baada ya kuvamia kituo kidogo cha Polisi cha Sitakishari, Ukonga jijini Dar es salaam usiku huu.
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kwamba askari polisi kadhaa kituoni hapo pamoja na raia mmoja wameuwawa. Silaha kadhaa pia inasemekana zimeporwa na askari wako eneo la tukio hivi sasa.
Tunaendelea kufuatilia taarifa hii na tutawajuza maendeleo yake kadri tutapopata fununu...

 

9 years ago

Michuzi

NEWS ALERT: Hatimaye Gesi Asilia kutoka Mtwara yafika Dar es salaam

 Mtaalam kutoka Kampuni ya “CPP” (Mkandarasi wa Mradi wa Gesi Asilia) (Kulia) akitoa maelezo ya usalama kabla ya wakuu wa taasisi za TPDC na TANESCO kuingia katika kituo cha kupokea gesi asilia Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, kituo hicho tayari kimeanza kupokea gesi asilia kutoka kiwanda cha kuchakata gesi  Madimba Mkoani Mtwara.

 Mtaalam kutoka Kampuni ya Mhandisi Mshauri Muelekezi (WorleyParsons), Allen Slowe (kulia) akitoa maelezo ya jinsi ya zoezi zima la kupokea gesi asilia...

 

9 years ago

Michuzi

News alert: Gari lateketea kwa moto mchana huu sinza Kumekucha, dar es salaam

 Gari dogo linalosemekana lilikuwa matengenezoni limeshika moto na kuteketea mchana huu eneo la Sinza Kumekucha jijini Dar es salaam. Mashuhuda wameiambia Globu ya Jamii eneo la tukio kwamba huenda chanzo kikawa moto wa kuchomelea ambapo fundi welding alikuwa kazini. Shughuli zikiendelea kama kawaid wakati gari hilo likiwaka motoHadi wakati ripota wetu akiondoka eneo hilo huku gari likizidi kuteketea hakuna dalili ya kuwepo ya juhudi za kuliokoa. Ihukuriwe hakuna mtu aliyepata madhara.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani