Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Profesa Tibaijuka atetewa mgawo wa escrow

Wakati Watanzania wakisubiri utekelezaji wa maazimio ya Bunge juu ya ufisadi wa Akaunti ya Tegeta Escrow, Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Barbro Johansson Girls’ Education Trust, imemtetea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kuwa hastahili kuwajibishwa.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Vijimambo

Mgawo Escrow wamchanganya Prof. Tibaijuka

Juhudi za Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka, kujisafisha dhidi ya kashfa ya kunufaika na mgao wa zaidi ya Sh. bilioni 300 zilizochotwa katika akaunti ya Tegeta Escrow, zimechukua sura mpya na sasa anaitumia shule ya wasichana ya Barbro Johansso, bodi yake, wanafunzi na wazazi kujinasua.

Prof. Tibaijuka ambaye aligawiwa Sh. bilioni 1.6 katika fedha hizo, tangu juzi ulianza mkakati wa kutoa matangazo katika magazeti na jana uliitishwa mkutano wa waandishi wa...

 

10 years ago

Mwananchi

Mgawo wa escrow wazidi kumtesa Tibaijuka

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana waliendeleza mvutano kuhusu mgawo uliofanywa na Mkurugenzi wa VIP Engeering, James Rugemalira kwenda kwa watu mbalimbali.

 

10 years ago

Mwananchi

Escrow yamfukuzisha kazi Profesa Tibaijuka

Rais wa Jamhuri wa Tanzania Jakaya Kikwete ametangaza kumfukuza kazi  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka baada ya vyombo vya Serikali kubaini na kijiridhisha kuwa amekiuka maadili ya utumishi wa Umma kwa kuingiziwa fedha kiasi cha Sh1.65bilioni kwenye akaunti yake binafsi.

 

10 years ago

Mtanzania

Askofu asimulia mgawo wa Escrow

Nzigilwa-bishopNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

HATIMAYE Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Eusebius Nzigilwa, amevunja ukimya na kusimulia namna alivyopokea Sh milioni 40.4 kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engireering & Marketing Ltd, James Rugemalila.
Fedha hizo, ni sehemu ya kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Askofu Nzigilwa ni mmoja wa watu waliotajwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), mwaka jana kuwa alipokea...

 

10 years ago

Habarileo

‘Maaskofu mgawo Escrow wabanwa’

MWENYEKITI wa Ushirika wa Wachungaji wa Kipentekoste Tanzania (PPFT), Askofu Pius Ikongo ameibuka na kutaka Jukwaa la Kikristo (TCF) kutoa tamko juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya maaskofu waliotuhumiwa kupokea mgawo wa fedha za Escrow.

 

10 years ago

Mtanzania

Vigogo kizimbani mgawo Escrow

2Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
SAKATA la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, limeanza kuchukua sura mpya baada ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), kuwafikisha mahakamani vigogo wawili wa Serikali.
Vigogo hao, waliofikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana, ni Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA), Theophillo Bwakea na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa...

 

10 years ago

Mwananchi

Waliopata mgawo Escrow kutozwa mamilioni

Watu waliopokea mgawo wa fedha zilizochotwa kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) huenda wakalazimika kulipa mamilioni ya Shilingi ambayo ni kodi ya mapato ya fedha walizopewa, imefahamika.

 

11 years ago

Mwananchi

Profesa Tibaijuka azomewa

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka alipata wakati mgumu juzi jioni baada ya kuzomewa na wananchi waliokerwa na kitendo chake cha kubadilika na kumruhusu mwekezaji kuendelea kumiliki eneo la ardhi katika Shamba la Kapunga, Wilaya ya Mbarali, Mbeya.

 

11 years ago

Mwananchi

Moto wamwakia Profesa Tibaijuka

 Viongozi wa vyama vya siasa na wanaharakati wa masuala ya ardhi, wamesema kuzomewa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka ni matokeo ya makosa yanayowafanywa na Serikali kuwapendelea wawekezaji wa nje na kuwapuuza wananchi.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani