Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


SADC yaishukuru Tanzania kwa mchango wa ukombozi na kumpongeza Mzee Hashim Mbita


Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Rais Robert Gabriel Mugabe wa Zimbabwe akimkabidhi Bi. Sheila Hashim Mbita, binti yake Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita Tuzo ya Juu ya Taifa la Zimbabwe ya Nishani ya Royal Order Of Mwanamutapa kwa kutambua mchango wake katika ukombozi wa Taifa la Zimbabwe na nchi nyingine kusini mwa Afrika. Rais Mugabe alikabidhi tuzo hiyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

Mwanafunzi wa Tanzania Aibuka mshindi wa Kwanza Tuzo ya Isha SADC, Rais Mugabe amtunuku Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza mwanafunzi wa kidato cha nne Neema Steven Mtwanga(16) anayesoma katika shule ya sekondari Naboti Makambako,Njombe baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika utunzi wa insha katika shindano lililoandaliwa na Jumuiya ya uchumi ya maendeleo kusini mwa Afrika(SADC).Rais Kikwete alimpongeza mwanafunzi huyo wakati wa hafla ya ufunguzi wa mkutano wa 34 wa wakuu wa nchi za SADC unaofanyika katika mji wa kitalii wa Victoria Falls, nchini Zimbabwe ambapo...

 

10 years ago

Michuzi

JUST IN: gwiji la ukombozi wa afrika kusini brigedia jenerali hashim mbita afariki dunia leo dar es salam


Habari zilizotujia hivi punde zinasema Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), amefariki dunia asubuhi hii katika hospitali kuu ya jeshi ya Lugalo jijini Dar es salaam. 
Mzee Mbita atakumbukwa Tanzania,  bara zima la Afrika na dunia kwa jumla kama kamanda mahiri aliyeshiriki kikamilifu katika uondoshaji wa utawala wa ukoloni  barani Afrika, hususan utawala kidhalimu wa makaburu  Zimbabwe na  Afrika...

 

11 years ago

Michuzi

Rais Kikwete awajulia hali Mzee Hashim Mbita na Mbunge Donald Max

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Mbunge wa Geita Donald Max aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili leo jioni.Rais Kikwete akiwa hospitalini hapo alimjulia hali pia Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita aliyelazwa hospitalini hapo(picha na Freddy Maro).

 

10 years ago

New Kerala

Tanzania's liberation icon Hashim Mbita dies at 74


Economy Lead
Tanzania's liberation icon Hashim Mbita dies at 74
New Kerala
Hashim Mbita, a Tanzanian army general and the icon of the southern Africa liberation struggle, died at the age of 74 on Sunday after a long illness. The East African nation's State House in the commercial capital Dar es Salaam said in a statement that Mbita, ...
Hashim Mbita is no moreDaily News

all 7

 

10 years ago

Michuzi

Rais Kikwete atoa heshima za Mwisho kwa Brigedia Jenerali Hashim Mbita

Amiri Jeshi Mkuu, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Katibu Mkuu mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Afrika (OAU) marehemu Brigedia Jenerali(Mstaafu) Hashim Mbita katika hospitali kuu ya Jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo. Rais Kikwete akiifariji familia ya Marehemu muda mfupi baada ya kutoa heshima za mwisho(picha na Freddy Maro).

 

10 years ago

Dewji Blog

Tanzania yampoteza mtu muhimu, ni Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita aliyefariki dunia mapema leo

Marehemu Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita

Taifa likiwa katika maadhimisho ya miaka 51 ya Muungano wa Tanzania Bar na Zanzibar, mapema leo limepata pigo baada ya kuondokewa na mtu muhimu na aliyewahi kuwa Katibu Mtendaji wa Kamati ya Ukombozi ya uliokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Brigedia Jenerali Mstaafu Hashim Mbita aliyefariki katika dunia majira ya asubuhi katika hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo,  jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa duru za habari kutoka familia ya...

 

10 years ago

Michuzi

Salam za Rambirambi kutoka kwa Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi kwa Familia ya Marehemu Brigedia Hashim Mbita

 Nimeshtushwa sana na kifo cha Kiongozi huyu mashuhuri aliyechangia kwa dhati harakati za ukombozi wa Bara la Afrika. Nimehuzunishwa mno, mimi Binafsi, Familia yangu na nina imani msiba huu mzito sio wa Watanzania peke yao, bali ni wa Bara zima la Afrika kwa ujumla. Katika harakati za kumzika kiongozi huyo, sitokuwepo kwa kuwa niko safarini lakini nitawakilishwa na wanangu wakiongozwa na Dkt Hussein. Kwa Mola tumetoka na kwake Mola sote tutarejea. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya...

 

10 years ago

Michuzi

MH. MEMBE AKABIDHI HUNDI YA DOLA LAKI 1 KWA FAMILIA YA BRIGEDIA JENERALI HASHIM MBITA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard K. Membe (Mb) (katikati) akikabidhi hundi yenye thamani ya Dola za Marekani laki moja kwa mtoto wa Brigedia Jen. Mstaafu Hashim Mbita, Bibi Shella Mbita. Bibi Mbita alipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Baba yake ambayo imetolewa na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Robert Mugabe kutokana mchango mkubwa alioutoa Brig. Jen. Mbita katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika. Mwingine katika picha ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe....

 

10 years ago

Vijimambo

MHE. BERNARD MEMBE AKABIDHI HUNDI YA $ 100,000 KWA MTOTO WA BRIGEDIA JEN. MSTAAFU HASHIM MBITA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard K. Membe (Mb) (katikati) akikabidhi hundi yenye thamani ya Dola za Marekani laki moja kwa mtoto wa Brigedia Jen. Mstaafu Hashim Mbita, Bibi Shella Mbita. Bibi Mbita alipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Baba yake ambayo imetolewa na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Robert Mugabe kutokana mchango mkubwa alioutoa Brig. Jen. Mbita katika harakati za ukombozi Kuisini mwa Afrika. Mwingine katika picha ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe....

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani