Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Samia aahidi makubwa wa bodaboda

MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kuanzisha madawati maalumu katika Manispaa za Dar es Salaam kwa ajili ya kusajili madereva wa bodaboda na bajaji, iwapo chama chake kitachaguliwa katika uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mtanzania

Samia aahidi ujenzi wa mabwawa

Pg 2 sept 1Patricia Kimelemeta, Dodoma

CHAMA Cha Mapinduzi(CCM), kimeahidi kujenga mabwawa makubwa ya maji ili kuondoa tatizo la maji lililopo mkoani hapa.

Akizungumza wakati  wa mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Bahi mkoani Dodoma jana, mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan alisema  uamuzi huo unalenga kumaliza kero ya maji ya muda mrefu ambayo imesababisha wananchi kukosa huduma hiyo.

Alisema kutokana na matatizo ya ukame yaliyopo katika mkoa huo, Serikali ya awamu ya tano itakayoongozwa...

 

10 years ago

Mwananchi

Samia aahidi mbadala wa mv Bukoba

Ikiwa imepita miaka 19 tangu meli ya Mv Bukoba ilipozama na kugharimu maisha ya zaidi ya abiria 1,000, wakazi wa Bukoba wamepata matumaini baada ya kuahidiwa meli mpya.

 

10 years ago

Mwananchi

Mgambia aahidi makubwa Simba

Kiungo mshambuliaji mpya wa Simba, Omary Mboom amesema kuwa hatofanya makosa iwapo atasajiliwa na badala yake atahakikisha anawapa raha wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kongwe nchini.

 

11 years ago

Mwananchi

Kiiza aahidi makubwa Yanga

>Mshambuliaji wa Yanga, Hamis Kiiza amejiapiza kuwa atahakikisha mwaka 2014 anavaa medali nyingi kadri inavyowezekana akiwa na kikosi cha timu hiyo.

 

10 years ago

Mtanzania

CAG mpya aahidi makubwa

Profesa Mussa Juma Assad

Profesa Mussa Juma Assad

NA KULWA KAREDIA, DAR ES SALAAM

RAIS Jakaya Kikwete, amemteua Profesa Mussa Juma Assad kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, imesema uteuzi wa Assad ulianza Novemba 5, mwaka huu.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Profesa Assad alisema hatamwangusha Rais Kikwete na Watanzania kutokana na imani iliyoonyeshwa kwake.

“Sitamwangusha...

 

10 years ago

Habarileo

Magufuli aahidi makubwa Moshi

MGOMBEA urais wa Tanzania kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, jana aliuteka mji wa Moshi mkoa wa Kilimanjaro, baada ya kuvuta umati mkubwa wa watu aliowakuna kwa hotuba yake iliyosheheni ahadi nzito, zikiwamo za kuondoa kero zinazowakabili na pia kuahidi kupaisha uchumi wa mkoa kwa ujumla.

 

10 years ago

Habarileo

Samia aahidi kubeba changamoto za walemavu

MGOMBEA Mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kushirikiana na watu wenye ulemavu katika kutatua changamoto zinazowakabili.

 

10 years ago

Habarileo

Samia aahidi ajira kwa 40% ya vijana

MGOMBEA mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassan, amesema katika ilani ya CCM ya awamu ya serikali ya tano, wameahidi kutoa ajira kwa asilimia 40 ya vijana ambazo zitatokana na viwanda, vikubwa na vidogo.

 

10 years ago

Mwananchi

Magufuli aahidi makubwa Tabora na Kigoma

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli ameahidi kushughulikia matatizo yanayowakabili wananchi wa kata ya Nguruka, jimbo la Kigoma Kusini yeye mwenyewe na kusema atakayechaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo amwachie yeye kazi hiyo.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani