Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


SIMBACHAWENE AIASA KAMATI YA PAMOJA YA UENDESHAJI WA MGODI WA TANZANITEONE

WAZIRI wa Nishati na Madini, George Simbachawene ameiasa Kamati ya Pamoja ya Uendeshaji wa Mgodi wa TanzaniteOne, “Joint Operating Committee”-JOC kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa ili kuwanufaisha wadau wa Tanzanite katika uvunaji wa madini hayo, huku wakilinda maslahi ya mgodi huo kwa  Taifa.


 Simbachawene ametoa rai hiyo hivi karibuni wakati akizindua Kamati ya hiyo ya JOC, katika hafla iliyofanyika kwenye eneo la mgodi wa TanzaniteOne uliopo Mirerani, katika Wilaya ya Simanjiro...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

TanzaniteOne yachongewa kwa Kamati ya Bunge

Wachimbaji wadogo wa madini ya tanzanite katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro wameishtaki kampuni ya TanzaniteOne kwa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wakidai kuwa imevamia na kupora baadhi ya migodi na zana za kufanyia kazi na kuharibu miundombinu yake.

 

11 years ago

Michuzi

KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE YAKUTANA NA SERIKALI PAMOJA NA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI MJINI DODOMA LEO

 Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza kikao cha pamoja baina ya Serikali, Kamati ya Uongozi pamoja na Kamati ya Bunge ya Bajeti ikiwa ni kikao cha maridhiano kuhusu Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2014/2014. kikao hicho kiliudhuriwa pia na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Kayanza Pinda, Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya. Picha kwa hisani ya Bunge  Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza kikao cha pamoja baina ya Serikali, Kamati ya Uongozi pamoja na Kamati ya...

 

10 years ago

Michuzi

Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira yaumwagia sifa Mgodi wa Buzwagi

Migodi ya dhahabu nchini imetakiwa kuiga mfano wa mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama katika kutunza na kuweka mazingira ya uzalishaji salama kwa binadamu na viumbe wengine.
 Rai hiyo imetolewa  na mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili  na Mazingira Mheshimiwa James Lembeli, wakati kamati hiyo ilipotembelea mgodi huo tarehe 30 Oktoba 2014 . 
Mhe.Lembeli alisema kuwa kamati yake ilifuatilia kwa kina utekelezaji wa maagizo na maelekezo ya Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC)  kwa migodi...

 

5 years ago

Michuzi

SIMBACHAWENE AWAONGOZA WATENDAJI WAKUU ZIMAMOTO KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati), akizungumza na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Victor Mwambalaswa wakati wakitoka kukagua Jengo la Makao makuu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, jijini Dodoma leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima....

 

5 years ago

Michuzi

WAZIRI SIMBACHAWENE AWAONGOZA WATENDAJI WA WIZARA KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE KUWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI, BUNGENI JIJINI DODOMA, LEO

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma, leo. Wizara iliwasilisha katika kikao hicho Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2020/21. Katikati ni Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Salim Mwinyi Rehani, na kulia ni Katibu wa Kamati hiyo, Ramadhani Abdalla. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya...

 

5 years ago

Michuzi

MWILI WA BABA MZAZI WA GEORGE SIMBACHAWENE , MAREHEMU BONIFACE SIMBACHAWENE WAZIKWA KIJIJINI PWAGA, JIMBO LA KIBAKWE WILAYANI MPWAPWA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene na Mkewe Mariana Simbachawene, wakiweka picha ya Baba Mzazi wa waziri huyo Marehemu Boniface Simbachawene wakati wa ibada ya mazishi yaliyofanyika katika Kijiji cha Pwaga kilichopo Jimbo la Kibakwe , wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Spika wa Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lililohifadhi mwili wa Baba Mzazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George...

 

11 years ago

Mwananchi

Mkapa aiasa Afrika Mashariki

>Rais Mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amewataka wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuacha kuoneana haya kwenye vikao vyao, badala yake waulizane yanayotokea kwenye nchi zao ili kuiepusha jumuiya na mauaji mengine ya kimbari kama ilivyotokea nchini Rwanda mwaka 1994.

 

11 years ago

Habarileo

Waziri Mkuu Finland aiasa Tanzania

WAZIRI Mkuu wa Finland, Jyrki Katainen, ameitaka Tanzania kutumia nafasi pekee iliyonayo kijiografia, kunufaika na ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Afrika kwa ujumla. Alisema hayo jana wakati wa majadiliano kuhusu uhusiano wa kiuchumi kati ya Bara la Ulaya na Afrika na jinsi ya kuongeza manufaa katika uhusiano huo. Katainen alisema ukanda wa Afrika Mashariki ni eneo ambalo uchumi wake unaendelea kukua kwa haraka na nchi yake imekuwa ikiendelea kusaidia nchi za ukanda huo...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani