Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Waathirika wa mafuriko mkoani Lindi wapata msaada wa thamani wa Sh.Milioni 30

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya China inayofanya kazi nchini  (Over Seas Chinese  Services Center) imetoa msaada kwa Wananchi waliopata maafa ya mafuriko mkoani Lindi.

Msaada huo umekabidhiwa kwa Chama cha Msalaba Mwekwendu Tanzania Red Cross wenye thamani ya sh.milioni 30.Akizungumza na waandishi wa Habari wakati wa akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa Taasisi ya China Aston Yi amesema kuwa Tanzania ni China ni familia moja hivyo wanajibu wa kutoa msaada...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

5 years ago

Michuzi

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MBEGU ZA MAHINDI KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO LINDI

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa, sehemu ya mbegu za mahindi tani nne zenye thamani ya shilingi milioni 20 zilizotolewa na Benki hiyo kupitia ombi maalum la Mbunge wa Kuteuliwa anayewakilisha mikoa ya Lindi na Pwani na Mwenyekiti wa mfuko Wanawake na Maendeleo Foundation (WAMA), Mama Salma Kikwete kwa ajili ya kuwasaidia wananchi wa mkoa huo ambao mashamba yao yaliathiwa na mafuriko mapema mwaka huu....

 

5 years ago

Michuzi

ARIFU ABRI ATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO MBINGAMA PAWAGA,MKOANI IRINGA


Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Vijijini Arifu Abri akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi msaada kwa ajili ya wahanga wa kitongoji cha Mbingama tarafa ya Pawaga.



NA FREDY MGUNDA, IRINGA.

MJUMBE wa mkutano mkuu wa CCM Taifa kupitia Wilaya ya Iringa Vijijini Arifu Abri ametoa msaada wa chakula tani tatu kwa ajili ya wahanga wa mafuriko wa kijiji cha  Isele kilichoko tarafa ya Pawaga wilaya ya Iringa vijijini mkoanbi Iringa kwa kuwa wanakabiliwa na...

 

5 years ago

Michuzi

RC MAKONDA ATOA MSAADA WA MABATI YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 476 KWAAJILI YA KUEZEKA NYUMBA 1,000 ZA WAJANE WALIOKUMBWA NA ADHA YA MAFURIKO DAR.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ametoa msaada wa Mabati yenye Thamani ya shilingi Milioni 476 kwaajili ya Kuezeka Nyumba 1,000 za Wajane mkoani humo ambao nyumba zao zimeathiriwa na mafuriko yanayotokana na Mvua zinazoendelea kunyesha ambapo amewataka Wananchi waliojenga mabondeni kuondoka.

RC Makonda amesema hayo wakati wa Ziara ya Kukagua athari za Mvua  na kubaini uwepo wa familia za Wajane ambao Nyumba zao zimechukuliwa na Mafuriko na sasa wanapitia changamoto ya...

 

10 years ago

Mwananchi

Waathirika wa mafuriko waomba msaada

Wananchi wa Kata ya Arusha chini, Wilaya ya Moshi wamewaomba viongozi wa Serikali kuwapatia msaada wa chakula na mavazi kutokana na  vitu vyao kusombwa na maji ya mvua inayoendelea kunyesha.

 

11 years ago

Tanzania Daima

Wahanga wa mafuriko wapata msaada

WAHANGA wa mafuriko katika Manispaa ya Tabora wamekabidhiwa msaada wa chakula tani 1.4 za unga wenye thamani ya zaidi ya sh milioni 1.2 baada ya nyumba zao kubomoka kutokana na...

 

11 years ago

Michuzi

WAATHIRIKA WA MAFURIKO MBEYA BADO WANAHITAJI MSAADA - MKUU WA WILAYA

Mkuu wa Wilaya Kyela Margareth Esther Malenga(katika)akiongozana na Mkuu wa Vodacom Foundation,Yessaya Mwakifulefule na Mwenyekiti wa chama cha Msalaba Mwekundu"Red Cross"Mkoa wa Mbeya Bw.Ulimboka Mwakilili,wakikagua maeneo yaliyoathirika na Mafuriko wakati walipokwenda kukabidhi msaada wenye thamani ya Shilingi Milion 10 kwa wahanga wa mafuriko wilayani humo. Mkuu wa Wilaya Kyela Margareth Esther Malenga(kulia)akipokea msaada wa vyandarua kupitia chama cha Msalaba Mwekundu"Redcross"kwa...

 

11 years ago

Habarileo

Milioni 100/- zahitajika Lindi kwa waathirika wa mvua, upepo

JUMLA ya Sh milioni 100 zinahitajika kufanya ukarabati wa shule za msingi, sekondari na zahanati wilayani Kilwa mkoani Lindi zilizoezuliwa bati na majengo kuharibiwa kutokana na mvua kali zilizoambatana na upepo mwezi huu.

 

10 years ago

Michuzi

BENKI YA NMB YATOA MSAADA KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO WILAYANI HAI

Meneja wa Benki ya NMB kanda ya kaskazini Vicky Bishubo akizungumza wakati wa kukabidhi msaada wa kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea hivi karibuni ukanda wa chini wilayani Hai.Msaada wa magodoro uliotolewa na Benki ya NMB kwa waathirika wa mafuriko yaliyotkea hivi karibuni wilayani Hai.Meneaja wa NMB kanda ya kasakazini Vicky Bishubo akikabidhi msaada kwa mkuu wa wilya ya Hai,Anthony Mtaka huku zoezi hilo likishuhudiwa na mbunge wa jimbo hilo Freeman Mbowe.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

 

11 years ago

Michuzi

Ubalozi wa China watoa msaada kwa waathirika wa mafuriko mkaoni Morogoro

Balozi wa China nchini Tanzania, Mhe. Lu Youping akikabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa Mkurugenzi wa Idara ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Leteni Jenerali Sylivester Rioba. msaada huo ambao unathamani ya Shilingi milioni 32 umetolewa kwa ajili ya watu walioathirika na mafuriko mkoani Morogoro. Balozi wa China (katikati) akishikana mikono na Luteni Generali Rioba na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Mhe. Athony Mtaka wakati wa hafla ya...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani