Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Watu wanne wauawa kwa kucharangwa kwa mapanga.

 

Watu wanne wamekutwa wameuawa katika kijiji cha  Katoma wilayani Bukoba, miili yao ikiwa imecharangwa kwa mapanga na watu wasiofahamika .

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera  Kamishna MSAIDIZI Mwandamizi wa Polisi Augustino Ollomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa watu waliohusika na mauaji hayo bado hawajatiwa mbaroni.

Matukio hayo yametokea katika kijiji cha Katoma wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ambapo jumla ya watu wanne wameuawa katika maeneo mawili...

StarTV

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

StarTV

Watu wanne wauawa kwa kukatwa mapanga Geita

Watu wanne wameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana katika kijiji cha Bugalama Wilaya ya Geita.

Tukio hilo limetokea disemba moja majira ya saa nne usiku likihusishwa na imani za kishirikina ambapo inadaiwa marehemu Mariamu Lushafisha alimuua mumewe Samuel Masebu ambaye alikuwa akionekana mara kwa mara maeneo ya nyumbani na baadhi ya wanandugu wa upande wa kiume kumtuhumu Mariam amemuua kimazingara.

Watu hao wasiofahamika waliingia na mapanga kwenye mji wa Marehemu Samuel Masebu...

 

10 years ago

Tanzania Daima

Auawa kwa kucharangwa mapanga

WATU wasiojulikana wamevamia Kanisa la Pentekoste Assemblies of God ( PAG ) usiku wa kuamkia leo Tawi la Kagemu, Kata ya Kitendaguro Manispaa ya Bukoba na kumuua mwalimu ambaye ni...

 

9 years ago

Michuzi

WATU WANNE WAMEUWAWA KWA KUKATWA NA MAPANGA MKOANI GEITA

Watu wanne wameuwawa kwa kukatwa na mapanga na watu wasiofahamika mkoani Geita kutokana na imani za kishirikina.

 

11 years ago

CloudsFM

KIKONGWE AUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA AKIWA NA WAJUKUU ZAKE WAWILI

Matukio ya mauaji ya wanawake vikongwe kutokana na ugomvi wa mashamba yameendelea kujitokeza mkoani Shinyanga ambapo huko katika kitongoji na kijiji cha Magwata kata ya Mwamalili katika manispaa ya Shinyanga,mwanamke aitwaye Sayi Nyenje(75) ameuawa kwa kukatwa mapanga shingoni na kiganjani akiwa amelala na wajukuu zake.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SAP Justus Kamugisha tukio hilo limetokea Julai 23,mwaka huu saa 11 alfajiri.

...

 

10 years ago

KwanzaJamii

WATU WANNE WA FAMILIA MOJA WAUAWA KWA KUKUTWA NA BHANGI

Familia ya wanne kuuawa Saudia kwa kupatikana na Hashish Utawala wa Saudi Arabia umeagiza kuuawa kwa watu wanne kutoka kwa familia moja kwa kosa la kumiliki dawa za kulevya. kaka hao waliokuwa katika makundi mawili waliuliwa Jumatatu katika mji wa Najran ulio kusini mashariki baada ya kuhukumiwa kwa kupokea kiasi kikubwa cha hashish. Mahakama ya taifa hilo imetoa adhabu za kifo kwa watu 17 katika wiki mbili zilizopita ikilinganishwa na 17 katika miezi sita ambayo imepita. Mwaka wa 2013...

 

9 years ago

Mwananchi

Mama na mwanawe wauawa kwa mapanga

Mkazi wa Kijiji cha Saragulwa, Kata ya Nyamwilolela mkoani hapa na mwanaye wameuawa kwa kukatwa mapanga na watu ambao hawajajulikana.

 

10 years ago

Tanzania Daima

Wanne wauawa kwa tuhuma za wizi

WATU wanne wameuawa kwa kupigwa marungu, kuchomwa mikuki na miili yao kuteketezwa kwa moto wilayani Sengerema, Mwanza wakituhumiwa kuwa wezi. Watu hao huku wawili kati yao ni ndugu, waliuawa na...

 

10 years ago

Vijimambo

WATU WANNE WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI WAUAWA KATIKA MAPAMBANO YA KURUSHIANA RISASI NA POLISI

Watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wauawa katika mapambano ya kurushiana risasi na polisi wilaya ya Momba. 
Katika tukio hilo watu wanne wanaume wasiofahamika wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliuawa katika majibizano ya kurushiana risasi na Askari Polisi.

Tukio hilo limetokea Agusti 3, 2015 majira ya saa 09.00hrs eneo la Sogea, Kata na Tarafa ya Tunduma Wilaya ya Momba. 
Awali watu hao walivamia dukani kwa Thadeo Sanga (50), mfanyabiashara na wakala wa kuuza/kusambaza bia za TBL ,...

 

9 years ago

GPL

MEXICO YAHALALISHA BANGI ITUMIKE KWA WATU WANNE TU

Mahakama Kuu nchini Mexico. Mwanaharakati anayeunga mkono matumizi ya bangi nchini Mexico, Lucha Libre aliyevaa Maski, akishangilia mara baada ya Mahakama Kuu nchini humo kuruhusu matumizi ya bangi. Mmoja wa wavuta bangi raia wa Mexico akivuta msokoto wa bangi nje ya jengo la Mahakama Kuu ya nchi hiyo jana. Mmoja wa wanaharakati na watumiaji wa zao la mmea wa bangi.… ...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani