Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


KIKONGWE AUAWA KWA KUCHARANGWA MAPANGA AKIWA NA WAJUKUU ZAKE WAWILI

Matukio ya mauaji ya wanawake vikongwe kutokana na ugomvi wa mashamba yameendelea kujitokeza mkoani Shinyanga ambapo huko katika kitongoji na kijiji cha Magwata kata ya Mwamalili katika manispaa ya Shinyanga,mwanamke aitwaye Sayi Nyenje(75) ameuawa kwa kukatwa mapanga shingoni na kiganjani akiwa amelala na wajukuu zake.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka wa kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SAP Justus Kamugisha tukio hilo limetokea Julai 23,mwaka huu saa 11 alfajiri.

...

CloudsFM

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Tanzania Daima

Auawa kwa kucharangwa mapanga

WATU wasiojulikana wamevamia Kanisa la Pentekoste Assemblies of God ( PAG ) usiku wa kuamkia leo Tawi la Kagemu, Kata ya Kitendaguro Manispaa ya Bukoba na kumuua mwalimu ambaye ni...

 

9 years ago

StarTV

Watu wanne wauawa kwa kucharangwa kwa mapanga.

 

Watu wanne wamekutwa wameuawa katika kijiji cha  Katoma wilayani Bukoba, miili yao ikiwa imecharangwa kwa mapanga na watu wasiofahamika .

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera  Kamishna MSAIDIZI Mwandamizi wa Polisi Augustino Ollomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba hadi sasa watu waliohusika na mauaji hayo bado hawajatiwa mbaroni.

Matukio hayo yametokea katika kijiji cha Katoma wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera ambapo jumla ya watu wanne wameuawa katika maeneo mawili...

 

9 years ago

Mwananchi

Bibi na wajukuu wawili wateketea kwa moto

Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia wilayani Mbarali mkoani hapa baada ya nyumba yao ya nyasi walimokuwa wamelala, kuungua moto.

 

11 years ago

GPL

AUAWA KIKATILI KWA MAPANGA

Stori: Victor Bariety, Geita
HUU ni unyama! Modester Shija, 55, mkazi wa Kitongoji cha Kamlale, Kijiji cha Nyawilimilwa, wilayani Geita, ameuawa kikatili kwa kukatwa mapanga. Tukio hilo la kuhuzunisha, lilitokea Machi 14, mwaka huu ambapo lilifanywa na watu wasiojulikana wakati mama huyo akiwa jikoni kwake akitayarisha chakula cha usiku. Ilielezwa kuwa siku ya tukio, majira ya saa 1:30 usiku, Modester akiwa jikoni,  walifika...

 

11 years ago

Habarileo

Mwendesha bodaboda auawa kwa mapanga

MWENDESHA bodaboda, mkazi wa Kijiji cha Korotambe Kata ya Mwema wilayani Tarime, Nyang'era Kirutu Chacha (40) ameuawa baada ya kupigwa mapanga katika kijiji cha Magena akidaiwa kuwa mwizi wa mifugo.

 

10 years ago

CloudsFM

MGANGA WA KIENYEJI AUAWA KWA RISASI, MAPANGA

Watu wasiofahamika wamemvamia na kumuua mganga wa kienyeji, Salehe Garimoshi (65), mkazi wa Kijiji cha Milala wilayani Mpanda kwa kumpiga risasi kichwani kisha kuukatakata mwili wake kwa mapanga.
Taarifa kutoka eneo la tukio, zilizothibitishwa na Jeshi la Polisi zinadai kuwa baada ya mganga huyo kuvamiwa na watu hao, mmoja wao aliyekuwa na bunduki, alimfyatulia risasi kichwani kisha kuamuru wenzake wamkatekate kwa mapanga.

Kaimu kamanda wa polisi wa Mkoa wa Katavi, Focus Malengo alisema jana...

 

9 years ago

Mwananchi

Mke auawa kwa mapanga, mume akimbia

Mwanamke kazi wa Kijiji cha Mgunga, wilayani Igunga, Gama Jilala ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana.

 

11 years ago

Mwananchi

Aua kikongwe, naye auawa

Kijana mmoja mkazi wa Kijiji cha Mabalanga wilayani Kilindi, Hassani Said (28) amemuua kwa kumkata na jembe kichwani bibi yake, lakini baadaye akauawa na wananchi wa eneo hilo.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani