Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Watu wawili wafariki dunia kwa mafuriko

Watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha na wengine kupoteza mali zenye thamani jijini Mwanza kufuatia mafuriko yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha majira ya saa kumi na mbili alfajiri ya leo.

Waliopoteza maisha ni pamoja na aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha nne aliyekuwa akiwahi shule kwa ajili ya kufanya mtihani wake wa mwisho na mmoja wa waendesha pikipiki aliyekuwa akiwawahisha wanafunzi wengine wa kidato cha nne kufanya mtihani wao wa mwisho.

Majira ya saa tatu asubuhi jijini Mwanza...

StarTV

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

StarTV

Watu wawili wafariki mkoani Kagera kwa Ugonjwa Wa Kipindupindu

Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dokta Thomas Rutachunzibwa amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu wawili kutokana na ugonjwa wa kipindupindu mkoani humo.

Aidha Mganga huyo amesema hadi hivi sasa jumla ya wagonjwa kumi na wawili waliokutwa na vimelea vya ugonjwa huo,wanaendelea na matibabu katika kambi maalum iliyopo katika hospitali ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Baada ya kuzuka kwa ugonjwa wa kutapika na kuharisha na kuthibitika kuwa si kipindupindu sasa imebainika wazi kuwa wagonjwa...

 

9 years ago

Mtanzania

Watu 19 wafariki dunia kwa kipindupindu

magesa-mulongoNa Benjamin Masese, Mwanza

SERIKALI imesema watu 631 mkoani Mwanza wameugua ugonjwa wa kipindupindu kati ya Januari  hadi Desemba 15, mwaka huu ambapo kati yao 19 wamefariki dunia.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo wakati akizungumza na madiwani pamoja watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu wiki iliyopita.

Wakati Mulongo akitoa takwimu hizo,  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Lwakyendera Onesmo  aliliambia MTANZNAIA jana kwamba wagonjwa wapya wameendelea...

 

5 years ago

Michuzi

Raia wawili wa Iran wafariki dunia mjini Qom kwa maradhi ya virusi vya Corona

Mkuu wa Kituo cha Mawasiliano ya Umma na Upashaji Habari cha Wizara ya Afya nchini Iran, amethibitisha habari ya kufariki dunia watu wawili kutokana na maambukizi ya virusi vya Corona mjini Qom nchini hapa.

Kiyanush Jahanpur aliyasema hayo jana Jumatano na kubainisha kwamba kufuatia ongezeko la matatizo ya kupumua lililoshuhudiwa katika siku za hivi karibuuni mjini Qom, uchunguzi wa vipimo ulithibitisha kesi mbili za maambukizi ya virusi vya Corona.  Ameongeza kwa kusema: "Kwa bahati mbaya...

 

11 years ago

CloudsFM

WATU SABA WAFARIKI DUNIA KWA KUTEKETEZWA NA MOTO

Watu saba wameuawa kwa kuchomwa moto ndani ya nyumba katika tukio ambalo nyumba 18 ziliteketezwa na mbili kubomolewa na wananchi waliodai wanawaua wachawi katika Kijiji cha Murufiti, Kasulu, mkoani Kigoma.

Polisi wameeleza kuwa tayari watu 17 wamekamatwa kwa kuhusika kwenye tukio hilo.
Miongoni mwa waliouawa katika tukio hilo lililotokea Jumatatu iliyopita ni John Mavumba (68) na mkewe Elizabeth Kaje 55 ambao pamoja na wenzao walikuwa wakituhumiwa kuwa ni washirikina.

Akizungumza na...

 

10 years ago

Mwananchi

Wanahabari wawili wafariki dunia

Tasnia ya habari imepata simanzi baada ya waandishi wawili wa habari, Innocent Munyuku na Baraka Karashani kufariki dunia jana jijini Dar es Salaam.

 

9 years ago

Global Publishers

Watu 8 akiwemo Msaidizi wa IGP Wafariki Dunia Kwa Kusombwa na Maji Dodoma

Polisi Eneo la tukio, maaskari wakiukagua mwili wa marehemu.polisiii 1Gari walilopata nalo ajali

WATU 8 wamefariki dunia katika ajali iliyosababishwa na gari kusombwa na maji huku watu 6 wakiwa wa  familia moja.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Davidi Misime amesema majira ya saa tatu usiku Jumapili, wananchi wa Kibaigwa walitoa taarifa jeshi la polisi kwa madai kwamba kuna gari limesombwa na maji na limetumbukia katika mkondo wa maji.

Amesema baada ya jeshi kupata taarifa hizo polisi...

 

9 years ago

Michuzi

WATU SABA WAFARIKI DUNIA KWA KUUNGUA NA MOTO NA WENGINE KUMI WAJERUHIWA

 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma Ferdnand Mtui  akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya ajali ya moto iliyotokea Mkoani Kigoma. Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma katika wodi namba saba hospitali ya Mkoa wa Kigoma. Majeruhi wakiendelea kupatiwa huduma ya matibabu katika wodi namba saba hospitali ya Mkoa wa Kigoma.
                                               Na Editha Karlo wa blog wa jamii,Kigoma
WATU saba wamefariki duniani na wengine kumi wamejeruhiwa katika ajali...

 

5 years ago

Michuzi

BREAKING NEWZZZZZ: WATU 18 WAFARIKI DUNIA NA WENGINE 15 WAJERUHIWA KWA AJALI WILAYANI MKURANGA.


Watu 18 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Kamanda Lyanga amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo Jumatano Aprili 15, 2020 na kwamba imehusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster.“Ni Kweli tuko kwenye eneo la tukio, ajali imetokea na imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15,” amebainisha...

 

5 years ago

Michuzi

WAWILI WAFARIKI DUNIA ARUMERU KUFUATIA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

Na Woinde Shizza, ArushaWATU wawili wamefariki dunia kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha kwa siku tatu mfululizo katika wilaya ya Arumeru huku nyumba zaidi ya 50 kuharibika kutokana na mvua hizo.
Akitoa taarifa za hali ya mwendendo wa mvua hizo mara baada ya kufanya ziara na kushiriki shughuli za uokoaji, Mkuu wa wilaya ya Arumeru  Jery Muro amesema kuwa mvua hizo  zimeleta madhara makubwa kwani zimesababisha vifo vya watu wawili ambao wamefariki dunia leo Alhamisi   April 23 Katika...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani