Yanga yaanzia kileleni
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga jana walianza vyema kampeni ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo mkali uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
habarileo
Habari Zinazoendana
9 years ago
Mtanzania17 Dec
Yanga yakwea kileleni
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wamekwea kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo, baada ya kuifunga bao 1-0 timu ya African Sports katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Bao hilo lilifungwa katika dakika 90 ya mchezo huo kupitia kwa Thabani Kamusoko, baada ya kupokea pasi ya Donald Ngoma hivyo kuifanya Yanga kushika usukani wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 27 huku Azam FC wakishika nafasi ya pili kwa kuwa na pointi 26.
Yanga walianza mchezo huo kwa kasi ambapo...
10 years ago
Mtanzania05 Feb
Yanga yajivinjari kileleni
NA SALMA JUMA, TANGA
USHINDI wa bao 1-0 dhidi ya Wagosi wa Kaya wa Tanga, timu ya Coastal Union jana umeifanya Yanga kujivinjari kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa na pointi 22 katika msimamo wa ligi hiyo.
Yanga imejikusanyia pointi hizo baada ya kucheza michezo 12, huku ikibakiza mechi yake ya kiporo dhidi ya Mbeya City, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 21 huku ikiwa imecheza michezo 11, Mtibwa inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 18.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa...
9 years ago
Habarileo17 Dec
Yanga yapaa kileleni
YANGA jana iliishusha Azam na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya African Sports. Ushindi huo unaifanya Yanga ambayo ndio bingwa mtetezi wa ligi hiyo kufikisha pointi 27 na kuishusha Azam yenye pointi 26, lakini ikiwa na mchezo mmoja nyuma.
9 years ago
Mwananchi01 Nov
Yanga kileleni kwa saa 24
10 years ago
Mtanzania12 Feb
Azam yaishusha Yanga kileleni
NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Azam FC, jana walirejea kuongoza ligi kwa kishindo baada ya kuibamiza bila huruma Mtibwa Sugar mabao 5-2 katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Kwa matokeo ya jana, Azam imefikisha pointi 25 sawa na Yanga lakini zikiwa zimetofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.
Azam ilianza kupata karamu hiyo ya mabao kupitia kwa mshambuliaji wake wa kimataifa, Didier Kavumbagu dakika ya 19,...
9 years ago
Habarileo30 Oct
Azam yaitoa Yanga kileleni
AZAM jana ilishika usukani wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya JKT Ruvu. Mchezo huo uliokuwa na ushindani wa hali ya juu ulifanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ambapo hadi mapumziko washindi walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
9 years ago
Mwananchi28 Dec
Azam yaipumulia Yanga kileleni
10 years ago
BBCSwahili10 Feb
Azam kuitoa Yanga kileleni?
9 years ago
Mtanzania31 Dec
Azam yaiporomosha Yanga kileleni
NA JENIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
TIMU ya Azam FC imeitibulia Yanga kwa kuitoa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuifunga Mtibwa Sugar bao 1-0 na kukwea juu yao katika mchezo uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo, Azam wamefikisha pointi 35 wakiishusha Yanga nafasi moja ambao wana pointi 33 katika msimamo wa ligi hiyo.
Lilikua bao la mshambuliaji John Bocco, ambalo lilitosha kuirejesha Azam kileleni, baada ya kufunga bao pekee...