Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Askari wawili wauawa, SMG 10, risasi na mabomu vyaporwa

IGP Mangu

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Mangu

NA PETER MAKUNGA, BUKOMBE

HOFU ya usalama wa raia na mali zao imetanda baada ya askari polisi wawili kuuawa na bunduki 10 aina ya SMG kuporwa katika Kituo Kikuu cha Polisi wilayani hapa.

Uporaji huo umefanywa na watu ambao hawajafahamika baada ya kuvamia kituo hicho saa 9:45 alfajiri na kuwashambulia askari polisi waliokuwa zamu ambapo wawili waliuawa na wengine watatu walijeruhiwa.

Mbali na kupora SMG 10, pia inadaiwa wamefanikiwa kupora risasi...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Majambazi yateka kituo cha polisi, yaua askari wawili, yapora SMG tano

WATU 15 wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za kivita na mabomu ya kurushwa kwa mkono wamevamia kituo cha polisi Ikwiriri  wilayani Rufiji Mkoani Pwani na kuua askari polisi wawili na kupora silaha tano za SMG na mbili za kufyatulia mabomu ya machozi zilizokuwepo kituo hapo na kutokomea kusikojulikana.

 

11 years ago

Tanzania Daima

Wavuvi wawili wauawa kwa risasi

WAVUVI wawili wilayani Mlele, Katavi wameuawa  kwa kupigwa  risasi   na askari wa Game Reserve walipokuwa wakivua samaki  ndani ya  Hifadhi  ya Pori la Akiba la Ugala na mwenzao mmoja kujeruhiwa ...

 

11 years ago

Mwananchi

Raia wawili, askari wauawa Moro, kituo chachomwa moto

Watu watatu, akiwamo askari polisi wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kuzuka mapambano kati ya polisi na raia katika Kijiji cha Igwati, Tarafa ya Malinyi Wilaya ya Ulanga, Morogoro.

 

10 years ago

Dewji Blog

Mkulima anaswa na risasi 271 za SMG

DSC03164

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP.Thobias Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake.

Na Nathaniel Limu, Singida

JESHI la polisi mkoa wa Singida linamshikilia mkulima na mkazi wa Matele-Kasulu mkoani Kigoma,Discon Bavumbi Masombo Kiyungu (45) kwa tuhuma ya kumiliki risasi 271 za bunduki ya kijeshi aina ya SMG kinyume na sheria.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP.Thobias Sedoyeka, alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa Januari 18 mwaka...

 

10 years ago

Mwananchi

Anayedaiwa kuua polisi Bukombe, akamatwa na SMG sita, mabomu 11

Siku moja baada ya kituo cha polisi cha Wilaya ya Bukombe mkoani Geita kuvamiwa na majambazi wakiwa na silaha na kuua polisi wawili, Jeshi la Polisi limemtia mbaroni mtu mmoja akidaiwa kuhusika katika tukio hilo.

 

10 years ago

Michuzi

TAARIFA YA POLISI JIJINI DAR: MAJAMBAZI WAWILI WAUAWA DAR WAKATI WA MAPAMBANO KATI YAO NA ASKARI WA JESHI LA POLISI

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata silaha moja aina ya SMG yenye namba BA172288  na risasi kumi na tatu wakati wa  mapambano makali ya ana kwa ana kati ya majambazi na Jeshi la Polisi.  Aidha katika tukio hilo majambazi wawili waliuawa  kwa risasi wak ati wakijaribu kuwadhuru askari.  
Tukio hilo lilitokea eneo la Kariakoo mtaa wa Mkunguni na Livingstone saa 3.00hrs usiku. Wakati wa tukio hilo umeme ulikuwa hakuna na mlalamikaji alikuwa anatumia taa za...

 

10 years ago

Habarileo

Kanda ya Ziwa wanasa jambazi sugu, SMG, risasi 331

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Valentino MlowolaPOLISI wa mikoa ya Mwanza, Simiyu na Shinyanga wamefanikiwa kusambatarisha mtandao wa ujambazi kwenye mikoa hiyo baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ujambazi sugu, Njile Samweli (46) mkazi wa kijiji cha Lyoma, Bariadi mkoani Simiyu aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu.

 

10 years ago

Michuzi

POLISI WAKAMATA BUNDUKI SMG, RISASI 59 PAMOJA NA WATUHUMIWA KATIKA MATUKIO TOFAUTI JIJINI DAR.

 Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha. Watuhumiwa wamekamakwa katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam kufuatia oparesheni kali inayoendelea ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali.
Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 03/06/2015 majira saa 08:00HRS  maeneo ya Tabata Kinyerezi mtaa wa Kibaga askari wa kikosi kazi (TASK FORCE) walimkamata mtuhumiwa  HEMED S/O...

 

10 years ago

Michuzi

TAARIFA: POLISI WAKAMATA BUNDUKI AINA YA SMG NA JUMLA YA RISASI 59 PAMOJA NA WATUHUMIWA KATIKA MATUKIO TOFAUTI JIJINI DAR

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha. Watuhumiwa wamekamakwa katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam kufuatia oparesheni kali inayoendelea ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali.
Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 03/06/2015 majira saa 08:00HRS  maeneo ya Tabata Kinyerezi mtaa wa Kibaga askari wa kikosi kazi (TASK FORCE) walimkamata mtuhumiwa  HEMED S/O...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani