Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


CCM: KUJITOA SLAA, LIPUMBA UKAWA WATANYOOKA TU!

Mwandishi wetu WATANYOOKA tu! Hiyo ndiyo kauli waliyoitoa wafuasi wa CCM jijini Dar baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (Cuf), Ibrahim Lipumba kujiweka pembeni katika shughuli za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa). Slaa amedaiwa kujichimbia nyumbani kwake Mbweni jijini Dar na kukataa kuzungumzia hatma yake kisiasa na kuacha shughuli za Ukawa...

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

CUF yakanusha kujitoa Ukawa

>Chama cha Wananchi CUF kimekanusha taarifa zilizoenea kuwa kimejitoa kwenye Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) CUF imesema kuwa haikuhudhuria katika kikao cha Ukawa kilichoendelea jana kwa sababu kwanza hawakupata taarifa na pia walikuwa na kikao cha ndani ya chama kama katiba yao inavyotaka.

 

9 years ago

Mtanzania

Nape awapongeza Dk. Slaa, Lipumba

napeNA EVANS MAGEGE

KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Nape Nnauye, amewafananisha viongozi waliokihama chama hicho na oili chafu.

Pia aliwapongeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu ‘aliyepumzishwa’ wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kuwa wamejitambua kisiasa kwa kujitenga na oili hiyo inayomiminwa ndani ya injini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Akizungumza na waandishi wa...

 

10 years ago

Raia Tanzania

Profesa Lipumba, Dk. Slaa hamjatutendea haki

WAKATI mwingine ni wanasiasa wenyewe wanaosababisha raia wa kawaida kuuamini msemo uliopo mitaani kuwa ‘siasa ni mchezo mchafu’.

Msemo huu wa kawaida kabisa mitaani umesababisha hata mtu akizungumza porojo tu watu hudai kwamba eti; ‘hizo ni siasa tu.’

Kwa hiyo sasa siasa kwa lugha nyingine ya mtaani ni ‘usanii’ tu, kitu ambacho si kweli hata kidogo.

Wasomi wa ‘sayansi ya siasa’ (sina hakika kama ndio tafsiri halisi ya ‘political science’), hudai kuwa siasa ni sayansi ya jamii...

 

10 years ago

Raia Mwema

Kiujiuzulu kwa Prof. Lipumba na sintofahamu ya Dk. Slaa

MAKALA hii ni mwendelezo wa ile iliyochapishwa katika gazeti hili katika toleo la wiki iliyopita.

Evarist Chahali

 

10 years ago

Mwananchi

Prof Lipumba, Zitto DK Slaa, kuvaana kwenye mdahalo

Umoja wa watendaji wakuu wa kampuni wa CEO RoundTable (CEOrt) umeandaa mdahalo wa kuzungumzia mbio za urais utakaowahusisha viongozi wa vyama vya upinzani, Profesa Ibrahim Lipumba, Dk Willibrod Slaa, Zitto Kabwe na Emmanuel Makaidi, lakini Chadema imesema itakuwa tayari kwa midahalo baada ya mchakato wa ndani kukamilika.

 

10 years ago

Raia Mwema

Slaa na sasa Lipumba, nani wengine dhamira zitawasuta?

“KWANGU mimi kuingia Ikulu ni tunda la lengo kuu ambalo ni kurudisha maadili ndani ya nchi hii.

Johnson Mbwambo

 

10 years ago

KwanzaJamii

Lipumba: Moyo wa Ukawa ni Wajumbe 14

Dar es Salaam. Wakati mchakato wa Katiba mpya unaendelea mjini Dodoma na suala la theluthi mbili likisumbua vichwa vya wengi, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameeleza kuwa kura za wajumbe 14 kutoka Zanzibar ndizo zitauokoa au kuukwamisha mchakato huo. Profesa Lipumba alikuwa kwenye mahojiano maalumu na Mwananchi nyumbani kwake, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kuhusu mustakabali wa mchakato wa Katiba baada ya kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia kuhudhuria...

 

10 years ago

Mtanzania

Profesa Lipumba: Nitaibeba Ukawa

lipumbaNA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahimu Lipumba amesema anatosha kugombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) iwapo atapewa nafasi hiyo na vyama washirika.
Amesema anawania nafasi hiyo huku kujiona ni mgombea pekee anayeweza kuwaunganisha Watanzania na kwamba ndiye aliasisi jina la Ukawa wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya kuchukua fomu ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani