Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Dar, Moro watu 262 wana kipindupindu

WATU nane wamethibitishwa kufariki kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine 262 wameambukizwa maradhi hayo katika mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro. Waziri wa Afya na Usatwi wa Jamii, Dk Seif Rashid akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa maradhi ya ugonjwa huo uliozuka hivi karibuni alisema hadi kufikia jana, kwa mkoa wa Dar es Salaam, watu saba wamefariki na wengine wapatao 230 tayari wameambukizwa ugonjwa huo.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Mtanzania

Watu 34 hoi kwa kipindupindu Dar

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

UGONJWA wa kipindupindu umezidi kushika kasi mkoani Dar es Salaam, baada ya idadi ya wagonjwa kuongezeka kutoka 27 hadi 34.

Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaama jana, Mratibu wa Huduma za Dharura, Mkoa wa Dar es Salaam, Victoria Bura alisema kumekuwapo na ongezeko la ugonjwa huo katika Wilaya ya Kinondoni.

Alitaja maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo kuwa ni Kijitonyama, Makumbusho, Saranga, Manzese, Tandale, Kimara na Mwananyamala.

Kwa mujibu wa Bura,...

 

9 years ago

Habarileo

Moro wajipanga kudhibiti kipindupindu

MKUU wa mkoa wa Morogoro (RC), Dk Rajab Rutengwe, amewataka watendaji wa kata na mitaa katika halmashauri za mkoa huo kuhakikisha kila mmoja anawajibika ipasavyo kusimamia suala la usafi wa mazingira na kuzuia uuzaji holela wa vyakula na matunda.

 

9 years ago

Mwananchi

Kipindupindu chaingia Moro, Shinyanga, mmoja afariki

Wakazi wa Kata ya Mindu Manispaa ya Morogoro wamekumbwa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu  ambapo hadi sasa mtu mmoja ameripotiwa kufa na hivyo kuzua hofu kwa wakazi  wa eneo hilo na manispaa kwa ujumla.

 

9 years ago

BBCSwahili

Mlipuko wa kipindupindu waua watu 3 TZ

Watu 3 wameaga dunia na wengine 30 wamelazwa hospitalini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu mjini Dar es salaam.

 

9 years ago

Habarileo

Watu milioni 10 kuelimishwa kipindupindu

WATANZANIA zaidi ya milioni 10 wanaotumia mitandao ya simu nchini, wanatarajia kunufaika kupata elimu kuhusu ugonjwa wa kipindupindu.

 

10 years ago

BBCSwahili

Kipindupindu chawaua watu 29 Sudan Kusini

Watu 29 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipundupindu nchini Sudan Kusini huku wengine 1000 wakiwa katika hatari ya maambukizi kulingana na Umoja wa mataifa.

 

9 years ago

Mtanzania

Watu 19 wafariki dunia kwa kipindupindu

magesa-mulongoNa Benjamin Masese, Mwanza

SERIKALI imesema watu 631 mkoani Mwanza wameugua ugonjwa wa kipindupindu kati ya Januari  hadi Desemba 15, mwaka huu ambapo kati yao 19 wamefariki dunia.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo wakati akizungumza na madiwani pamoja watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu wiki iliyopita.

Wakati Mulongo akitoa takwimu hizo,  Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Lwakyendera Onesmo  aliliambia MTANZNAIA jana kwamba wagonjwa wapya wameendelea...

 

9 years ago

Michuzi

WATU 196 WAMEFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIPINDUPINDU

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na ugonjwa wa Kipindupindu ulivyoweza kupungua ikiwa kukiwa na vifo vya watu 196 kwa Tanzania Bara.Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.

Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jamii.JUMLA ya...

 

9 years ago

Dewji Blog

Watu 27 waripotiwa kuwa na ugonjwa Kipindupindu jijini Arusha

2

Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu.

Mahmoud Ahmad Arusha

Jumla ya watu 27 waliripotiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa kipindupindu huku kati yao 6 walithibitishwa kuwa na ugonjwa wa kipindupindu. Na watano wamelazwa katika kituo cha Afya Levolosi.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake Mkuu wa wilaya ya Arusha, Fadhili Nkurlu aliwataka wakazi wa jiji la Arusha kufuata kanuni za ugonjwa huo na kuwa waepuke kula vyakula sehemu zisizofaa.

Nkurlu alisema kuwa kwa zaidi ya miezi miwili sasa...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani