Watu 34 hoi kwa kipindupindu Dar
NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM
UGONJWA wa kipindupindu umezidi kushika kasi mkoani Dar es Salaam, baada ya idadi ya wagonjwa kuongezeka kutoka 27 hadi 34.
Akizungumza na MTANZANIA mjini Dar es Salaama jana, Mratibu wa Huduma za Dharura, Mkoa wa Dar es Salaam, Victoria Bura alisema kumekuwapo na ongezeko la ugonjwa huo katika Wilaya ya Kinondoni.
Alitaja maeneo yaliyoathirika na ugonjwa huo kuwa ni Kijitonyama, Makumbusho, Saranga, Manzese, Tandale, Kimara na Mwananyamala.
Kwa mujibu wa Bura,...
Mtanzania
Habari Zinazoendana
9 years ago
Habarileo26 Aug
Dar, Moro watu 262 wana kipindupindu
WATU nane wamethibitishwa kufariki kwa ugonjwa wa kipindupindu na wengine 262 wameambukizwa maradhi hayo katika mkoa wa Dar es Salaam na Morogoro. Waziri wa Afya na Usatwi wa Jamii, Dk Seif Rashid akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa maradhi ya ugonjwa huo uliozuka hivi karibuni alisema hadi kufikia jana, kwa mkoa wa Dar es Salaam, watu saba wamefariki na wengine wapatao 230 tayari wameambukizwa ugonjwa huo.
9 years ago
Mtanzania28 Dec
Watu 19 wafariki dunia kwa kipindupindu
Na Benjamin Masese, Mwanza
SERIKALI imesema watu 631 mkoani Mwanza wameugua ugonjwa wa kipindupindu kati ya Januari hadi Desemba 15, mwaka huu ambapo kati yao 19 wamefariki dunia.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo wakati akizungumza na madiwani pamoja watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu wiki iliyopita.
Wakati Mulongo akitoa takwimu hizo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. Lwakyendera Onesmo aliliambia MTANZNAIA jana kwamba wagonjwa wapya wameendelea...
9 years ago
Michuzi![](http://1.bp.blogspot.com/-QN27tZAGe5k/VoFbmDEOdQI/AAAAAAAIPDE/rVVjl0Qc4D4/s72-c/IMG_9430.jpg)
WATU 196 WAMEFARIKI DUNIA KWA UGONJWA WA KIPINDUPINDU
![](http://1.bp.blogspot.com/-QN27tZAGe5k/VoFbmDEOdQI/AAAAAAAIPDE/rVVjl0Qc4D4/s640/IMG_9430.jpg)
![](http://3.bp.blogspot.com/-l5LDq8w8Dr4/VoFdsB8D0OI/AAAAAAAIPD4/cBQfqujfTHY/s640/IMG_9436.jpg)
Na Zainabu Hamis wa Globu ya Jamii.JUMLA ya...
9 years ago
StarTV21 Nov
Watu wawili wafariki mkoani Kagera kwa Ugonjwa Wa Kipindupindu
Mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dokta Thomas Rutachunzibwa amethibitisha kutokea kwa vifo vya watu wawili kutokana na ugonjwa wa kipindupindu mkoani humo.
Aidha Mganga huyo amesema hadi hivi sasa jumla ya wagonjwa kumi na wawili waliokutwa na vimelea vya ugonjwa huo,wanaendelea na matibabu katika kambi maalum iliyopo katika hospitali ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Baada ya kuzuka kwa ugonjwa wa kutapika na kuharisha na kuthibitika kuwa si kipindupindu sasa imebainika wazi kuwa wagonjwa...
9 years ago
Michuzi![](http://1.bp.blogspot.com/-PflB1vDnTuc/VnjzLG10PHI/AAAAAAAINzM/06Q-IcujenE/s72-c/USAFI.jpg)
MAKALA KUHUSU UGONJWA WA KIPINDUPINDU: Tujilaumu Watanzania kwa kuugua Kipindupindu
Kipindupindu ni ugonjwa wa kuharisha na kutapika unaosababishwa na vimelea vya bacteria vinavyoitwa kwa lugha ya kitaalam “vibro cholera”. Chanzo cha kikubwa cha ugonjwa huu huletwa na vimelea vilivyomo kwenye kinyesi na matapishi ya mgonjwa wa kipindupindu.
Kwa miaka mingi sasa wananchi wa Tanzania tumekumbwa na magonjwa ya aina mbalimbali ya mlipuko ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu ambao umeenea kwa kasi kubwa sana kutokana na kuwepo kwa mazingira hatarishi...
9 years ago
Mwananchi20 Aug
Ni aibu Dar kuwa sugu kwa kipindupindu
10 years ago
GPLSIMBA HOI KWA POLISI MORO UWANJA WA TAIFA DAR
9 years ago
BBCSwahili18 Aug
Mlipuko wa kipindupindu waua watu 3 TZ
9 years ago
Habarileo10 Dec
Watu milioni 10 kuelimishwa kipindupindu
WATANZANIA zaidi ya milioni 10 wanaotumia mitandao ya simu nchini, wanatarajia kunufaika kupata elimu kuhusu ugonjwa wa kipindupindu.