Eto’o ateuliwa kuwa kocha Uturuki
Mchezaji wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Chelsea Samuel Eto’o ameteuliwa kuwa kocha msaidizi wa klabu ya Antalyaspor ya Uturuki.
Eto’o atakuwa anasaidiana na mkufunzi wa timu ya vijana ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi Mehmet Ugurlu.
Atapewa kazi hiyo kwa mkataba wa muda mrefu iwapo klabu hiyo itafanya vyema kwenye mechi tatu kabla ya mapumziko mafupi ya majira ya baridi.
Eto’o alijiunga na timu ya Antalyaspor kama mchezaji huru Juni 25 kwa mkataba wa miaka mitatu na alicheza mechi...
Bongo5
Habari Zinazoendana
9 years ago
MillardAyo16 Dec
Hii ndio sababu ya Antalyaspor kumuongezea majukumu Samuel Eto’o ya kuwa kocha mchezaji …
Mshambuliaji wa kimataifa wa Cameroon anayekipiga katika klabu ya Antalyaspor ya Uturuki Samuel Eto’o bado yupo katika kikosi hicho na anapewa nafasi kubwa. Stori zilizotoka December 15 zinaeleza kuwa uongozi wa klabu ya Antalyaspor umempata majukumu mapya Samuel Eto’o ya kuwa kocha wa muda wa kikosi hiko. Stori kutoka mtandao wa cameroononline.com unaeleza kuwa Eto’o atakuwa kocha mchezaji wa […]
The post Hii ndio sababu ya Antalyaspor kumuongezea majukumu Samuel Eto’o ya kuwa kocha...
9 years ago
Dewji Blog10 Nov
Vieira ateuliwa kuwa kocha wa New York City FC
Kocha mpya wa New York City, Patrick Vieira.
Kikosi cha New York City.
Na Rabbi Hume
Mchezaji wa zamani wa Arsenal na kocha wa timu kukuzia vipaji ya vijana ya Manchester City, Patrick Vieira ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya New York City inayoshiriki ligi kuu ya nchini Marekani MSL.
Uteuzi wa Vieira umekuja ikiwa ni siku sita (6) tangu kutimuliwa kazi aliyekuwa kocha wa timu hiyo Jason Kreis.
Vieira ambae anaiongoza timu ya vijana kuangalia maendeleo ya vijana alijiunga na timu hiyo 2013...
9 years ago
Bongo521 Dec
Guus Hiddink ateuliwa kuwa kocha mpya Chelsea
![151219081747_guus_hiddink_file_512x288_pa_nocredit](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/12/151219081747_guus_hiddink_file_512x288_pa_nocredit-300x194.jpg)
Aliyekuwa meneja wa timu ya taifa ya Uholanzi Guus Hiddink ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Chelsea hadi mwisho wa msimu.
Ameteuliwa baada ya Jose Mourinho kufukuzwa kazi Alhamisi.
“Nimefurahia kurejea Stamford Bridge. Chelsea ni moja ya klabu kubwa duniani lakini haimo pale inakofaa kuwa kwa sasa. Hata hivyo nina uhakika tunaweza kubadilisha mambo,” amesema Hiddink baada ya kuteuliwa. “Nasubiri kwa hamu kufanya kazi na wachezaji na wakufunzi wenzangu wapya katika klabu hii kubwa na kufufua...
9 years ago
Dewji Blog02 Dec
Gary Neville ateuliwa kuwa kocha mkuu wa Valencia
Gary Neville.
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Beki wa zamani wa Manchester United na kocha wa kikosi cha kwanza cha timu ya taifa Wingereza, Gary Neville ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Valencia inayoshiriki Ligi kuu ya Hispania.
Gary Neville ameteuliwa kocha mkuu kwa mkataba mfupi na ataongoza timu hiyo mpaka mwishoni mwa msimu huu.
Neville amechukua nafasi hiyo baada ya siku chache zilizopita kutimuliwa kazi kwa aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Nuno Santo na sasa Gary Neville atafanya...
9 years ago
Bongo511 Nov
Abdallah ‘King’ Kibadeni ateuliwa kuwa kocha wa Kilimanjaro Stars
![Abdallah Kibadeni during a training session with Simba SC. TFF sources claim that the former Taifa Stars attacking midfielder will take charge of the Mainland side, Kilimanjaro Stars, for the 2015 Cecafa Challenge Cup. photo | file](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/11/pic-kili-stars-300x194.jpg)
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemteua Abdallah Kibadeni kuwa kocha mkuu wa timu wa Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Star’ atasaidiwa na Juma Mgunda kuelekea katika michuano ya CECAFA Chelenji itakayoanza kutimua vumbi Novemba 21 mjii Addis Ababa, Ethiopia.
Kilimanjaro Stars inashiriki michuano hiyo mikongwe kabisa barani Afrika, ambapo jumla ya nchi 12 wanachama wamedhibitisha kushiriki michuano hiyo itakayomalizika Disemba 6 mwaka huu.
Nchi hizo zinazoshiriki michuano hiyo...
9 years ago
Bongo510 Nov
Patrick Vieira ateuliwa kuwa kocha mpya wa New York City
![patrick-vieira_3238775b](http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2015/11/patrick-vieira_3238775b-300x194.jpg)
Mchezaji na kiungo wa zamani ufaransa na timu za Arsenal na Manchester City, Patrick Vieira ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya New York City.
Vieira mwenye miaka 39 amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Marekani.
Vieira alikuwa kocha wa kikosi cha vijana wa chini ya umri wa 21 cha Manchester City. Vieira ni miongoni mwa nyota wa timu ya taifa ya Ufaransa waliotwaa kombe la dunia mwaka 1998.
Vieira ataanza kazi hiyo rasmi Januari 1,...
9 years ago
Bongo527 Oct
Rigobert Song ateuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Chad
9 years ago
BBCSwahili16 Dec
Eto’o apewa kazi ya ukufunzi Uturuki
9 years ago
Mtanzania18 Dec
Eto’o awa kocha mpya Antalyaspor
ISTANBUL, UTURUKI
NYOTA wa zamani wa klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Cameroon, Samuel Eto’o, ameteuliwa kuwa kocha wa muda wa klabu ya Antalyaspor ambayo inashiriki ligi ya nchini Uturuki.
Nyota huyo alijiunga na klabu hiyo Juni, mwaka huu, akiwa kama mchezaji wa kawaida, lakini kwa sasa amepewa nafasi ya kuwa kocha mkuu wa muda akichukua nafasi ya kocha Yusuf Simsek.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye aliwahi kukipiga katika klabu ya Chelsea, alisaini mkataba wa miaka...