Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


HOFU YATANDA, SILAHA ZA KIVITA KUKAMATWA

Silaha zilizokamatwa zikioneshwa kwa wandishi wa habari. Na Timu ya Uwazi, Mkuranga HOFU kubwa imetanda kwenye Kijiji cha Mamndi Mkongo kilichopo Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani kufuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa  kushirikiana na wale wa mkoa huo kunasa silaha  nyingine za kivita zikiwa zimefukiwa kwenye shimo msituni. Tukio hilo  la unasaji wa silaha lilifanikiwa Agosti 29,  mwaka huu ...

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Mwananchi

Silaha za kivita zauzwa mpakani

Wakati Serikali ikihaha kukabiliana na ujangili na uhalifu mwingine wa kutumia silaha ukiwamo ujambazi unaotokea maeneo mbalimbali, imebainika kuwa silaha za kivita zimeendelea kupenyezwa na kuuzwa nchini kutoka nchi jirani.

 

11 years ago

Tanzania Daima

Mbaroni kwa silaha ya kivita

JESHI la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na bunduki ya kivita aina ya G3, namba FMP 061283B367 ikiwa na risasi zake tisa wakati wakisafirisha...

 

11 years ago

Habarileo

Polisi Z’bar wakamata silaha za kivita

POLISI Zanzibar, wamefanikiwa kukamata silaha mbili za vita na risasi 40 zinazosadikiwa kutumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu, likiwemo la mauaji ya askari polisi mmoja lililotokea Machi 2, mwaka huu huko kwenye Hoteli ya Kitalii ya Pongwe Bay mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar.

 

11 years ago

Tanzania Daima

Majambazi waua polisi, wapora silaha za kivita

WATU sita wanaodhaniwa kuwa majambazi, wamemuua askari polisi wa Kituo kidogo cha Polisi kilichopo Mkamba, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani na kuwajeruhi askari mgambo wawili baada ya kuvamia kituo hicho....

 

11 years ago

Mwananchi

Mwakilishi ataka Zanzibar imiliki silaha za kivita

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imeshauriwa kuwa na uraia kwa watu wake pamoja na kuvipa hadhi vikosi vyake maalumu ili viweze kumiliki silaha za kivita chini ya mfumo wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

 

5 years ago

CCM Blog

JWTZ YAKAMATA SILAHA ZA KIVITA MAKAMBI YA WAKIMBIZI KATAVI

  Serikali ya  Mkoa wa Katavi kwa kushirikiana na Jeshi la  Wananchi kikosi cha 202 na 401  wamefanikiwa  kukamata Bunduki 50 zikiwemo 13 za kivita na tatu zilizotengenezewa nchi za ulaya aina ya  G3 kufutia masako uliofanywa kwa muda wa siku 21 katika Makazi ya wakimbizi ya Katumba na Mishamo humo
Operesheni hiyo imefanyika ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli alilolitoa mwezi Oktoba  mwaka jana wakati wa ziara yake  Mkoani Katavi kwa uongozi wa Serikali ambapo aliwataka  ...

 

10 years ago

Mtanzania

Hofu ya Ebola yatanda nchini

20150810_182328NA EDITHA KARLO, KIGOMA

RAIA wa Burundi aliyetambulika kwa jina la Buchumi Joel (39), amefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa wenye dalili sawa na Ebola, ikiwa ni pamoja na kutokwa na damu sehemu mbalimbali za mwili wake.

Madaktari, wauguzi na ndugu waliomuhudumia mgonjwa huyo, wamewekwa chini ya uangalizi maalumu kwa siku 21 kama hatua ya tahadhari, huku wakisubiri kupokea majibu ya sampuli za vipimo ili kubaini iwapo kweli ni ugonjwa wa Ebola ama la.

Akizungumza na waandishi wa habari...

 

9 years ago

Raia Tanzania

Hofu Ukawa kuvunjika yatanda

MWENYEKITI mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia, amewataka viongozi na wanachama wa umoja huo kuheshimu makubaliano yaliyomo kwenye mwongozo waliotiliana saini mwaka jana.

Mbatia alitoa angalizo hilo baada ya kuwepo kwa viashiria kwa baadhi ya vyama ndani ya umoja huo kwenda kinyume na walichokubaliana hasa kuachiana majimbo kwa wagombea wabunge na udiwani.

Wiki hii kumekuwapo taarifa katika baadhi ya majimbo kwamba kuna vyama ndani ya Ukawa vimeweka wagombea...

 

10 years ago

Mwananchi

Hofu ya mabomu yatanda Njombe

Njombe. Wakazi wa Mji wa Njombe, jana walikumbwa na taharuki kutokana na mabomu ya machozi yaliyopigwa na Polisi kwa lengo la kutawanya waandamanaji waliokuwa wanapinga mauaji ya mkazi mmoja anayedaiwa kupigwa risasi na askari na mwingine kujeruhiwa.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani