Huduma Muhimbili yasimama tena, Wananchi washangaa
Mashine ya MRI iliyoko katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, iliyoanza kazi siku chache zilizopita imeharibika na kushindwa kufanya kazi tena na kusababisha kusimama kwa huduma za vipimo kwa wagonjwa wanaopaswa kupimwa na mashine hiyo.
Mashine hiyo ilianza kufanya kazi Baada ya tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Magufuli alilolitoa siku chache baada ya kuapishwa na kuutaka uongozi wa Hospitali hiyo uhakikishe mashine za CT-SCAN na MRI zinafanya kazi jambo ambalo...
StarTV
Habari Zinazoendana
9 years ago
Mwananchi16 Nov
Muhimbili wasitisha tena huduma za MRI
9 years ago
Habarileo17 Nov
MRI yaharibika tena Muhimbili
UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umesimamisha kwa muda huduma za uchunguzi kupitia mashine ya MRI kuanzia mwishoni mwa wiki, kwa ajili ya matengenezo zaidi ya mashine hiyo.
9 years ago
Mwananchi19 Nov
Mbu wavamia tena Muhimbili
9 years ago
Mtanzania17 Dec
MRI, CT-Scan zaharibika tena Muhimbili
NA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM
MASHINE ya MRI na CT-Scan zilizoko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) zimeharibika tena, licha ya kufanyiwa matengenezo siku kadhaa zilizopita baada ya Rais Dk. John Magufuli kuamuru zitengenezwe haraka.
Hii ni mara ya tatu sasa tangu mashine hizo zilipoanza kuharibika mapema mwishoni mwa Agosti, mwaka huu.
R a i s Magufuli alitoa amri ya kutengenezwa kwa m a s h i n e hizo Novemba 9, mwaka huu alipofanya ziara ya
kushtukiza hospitalini hapo,...
9 years ago
Mtanzania17 Nov
Mashine ya MRI Muhimbili yaharibika tena
Veronica Romwald na Allen Msapi (GHI), Dar es Salaam
MASHINE ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ijulikanayo kama Magnetic Reasonance Imaging (MRI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, imeharibika tena baada ya kufanya kazi kwa siku mbili, tangu ilipofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Philips.
Mashine hiyo ilifanyiwa matengenezo kutokana na shinikizo la Rais Dk. John Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo na kuamuru zifanyiwe marekebisho haraka.
Katika ziara yake hiyo,...
10 years ago
Habarileo14 Jan
Huduma za uzazi Muhimbili hoi
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi, huduma mbovu za rufaa na upungufu wa vitendea kazi, hali inayochangia kuwepo kwa huduma hafifu katika masuala ya uzazi.
10 years ago
Mtanzania04 Jun
Wagonjwa Muhimbili wasotea huduma ya CT -Scan
Hadia Khamis na Johanes Respichius (RCT), Dar es Salaam
BAADHI ya wagonjwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wamelalamikia hatua ya uongozi wa hospitali hiyo kushindwa kuchukua hatua za dharura za kutoa huduma za CT-Scan, ambayo imeharibika kwa kipindi cha miezi miwili sasa.
Wakizungumza na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, wagonjwa hao walisema wamekuwa wakiteseka kwa kipindi cha miezi miwili sasa bila kupata huduma hiyo.
Mmoja wa wagonjwa hao aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Omari,...
9 years ago
StarTV03 Dec
Huduma zaimarika hospitali ya Taifa Muhimbili
Hali ya utoaji wa huduma ya upimaji kwa mionzi ya CT Scan na MRI kwenye hospitali ya Taifa ya Muhimbili hivi sasa imeimarika baada ya uongozi wa kitengo hicho kuthibitisha kuwa mashine za vipimo zimeendelea kufanya kazi bila ya tatizo lolote.
Hatua hii inafikiwa baada ya Rais Dr. John Magufuli kuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha kuwa vipimo hivyo ambavyo vilikuwa vibovu kwa muda mrefu vinafanyiwa marekebisho na kuanza kazi mara moja.
Siku chache tu zimepita tangu mashine ya mionzi...
10 years ago
Mwananchi30 Oct
Wananchi walizwa kupanda kwa gharama Muhimbili