Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Muhimbili wasitisha tena huduma za MRI

Wiki moja baada ya kutengamaa kwa mashine ya uchunguzi wa magonjwa ya MRI (Magnetic Resonance Imaging), Hospitali ya Taifa Muhimbili imesitisha kutoa huduma hiyo jleo kutokana na kuharibika kwa kifaa  kimojawapo huku mashine ya CT Scan ambayo ni muhimu zaidi ikiwa bado haijatengamaa.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Habarileo

MRI yaharibika tena Muhimbili

UONGOZI wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) umesimamisha kwa muda huduma za uchunguzi kupitia mashine ya MRI kuanzia mwishoni mwa wiki, kwa ajili ya matengenezo zaidi ya mashine hiyo.

 

9 years ago

Mtanzania

MRI, CT-Scan zaharibika tena Muhimbili

mri--1NA VERONICA ROMWALD, DAR ES SALAAM

MASHINE ya MRI na CT-Scan zilizoko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) zimeharibika tena, licha ya kufanyiwa matengenezo siku kadhaa zilizopita baada ya Rais Dk. John Magufuli kuamuru zitengenezwe haraka.

Hii ni mara ya tatu sasa tangu mashine hizo zilipoanza kuharibika mapema mwishoni mwa Agosti, mwaka huu.
R a i s Magufuli alitoa amri ya kutengenezwa kwa m a s h i n e hizo Novemba 9, mwaka huu alipofanya ziara ya
kushtukiza hospitalini hapo,...

 

9 years ago

Mtanzania

Mashine ya MRI Muhimbili yaharibika tena

mictuVeronica Romwald na Allen Msapi (GHI), Dar es Salaam

MASHINE ya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ijulikanayo kama Magnetic Reasonance Imaging (MRI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, imeharibika tena baada ya kufanya kazi kwa siku mbili, tangu ilipofanyiwa matengenezo na Kampuni ya Philips.

Mashine hiyo ilifanyiwa matengenezo kutokana na shinikizo la Rais Dk. John Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo na kuamuru zifanyiwe marekebisho haraka.

Katika ziara yake hiyo,...

 

9 years ago

StarTV

Huduma Muhimbili yasimama tena, Wananchi washangaa

Mashine ya MRI iliyoko katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, iliyoanza kazi siku chache zilizopita imeharibika na kushindwa kufanya kazi tena na kusababisha kusimama kwa huduma za vipimo kwa wagonjwa wanaopaswa kupimwa na mashine hiyo.

Mashine hiyo ilianza kufanya kazi Baada ya tamko la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta John Magufuli alilolitoa siku chache baada ya kuapishwa na kuutaka uongozi wa Hospitali hiyo uhakikishe mashine za CT-SCAN na MRI zinafanya kazi jambo ambalo...

 

9 years ago

BBCSwahili

Kifaa cha MRI charekebishwa Muhimbili

Hospitali kuu ya Muhimbili nchini Tanzania,imesema kwamba mashine ya MRI imeanza kufanya kazi tena baada ya kurekebishwa.

 

9 years ago

Mwananchi

Muhimbili haistahili pongezi kwa MRI kutengemaa

Uongozi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ulitangaza kuwa mashine ya kuchukulia vipimo kwa nguvu ya sumaku (MRI), imepona baada ya kufanyiwa matengenezo na mafundi kutoka kampuni ya Phillips.

 

9 years ago

Michuzi

MAFUNDI WAZISHUGULIKIA MASHINE ZA MRI NA CT-SCAN MUHIMBILI.

MAFUNDI kutoka kampuni ya Philips wanaendelea na matengenezo ya mashine za MRI na CT-SCAN katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili zilizopata hitilafu za kiufundi hivi karibuni.
Akizungumza ofisini kwake leo hii Mkuu wa Idara ya Uhusiano Hospitali ya Taifa Muhimbili Bw. Aminiel Buberwa Aligaesha amesema mafundi wapo katika eneo la kazi wakitengeneza hizo mashine ili ziweze kurudi katika hali yake ya kawaida.
“Tumepewa siku tatu kukamilisha ukarabati wa hizi mashine hivyo wananchi wawe na subira...

 

9 years ago

Mwananchi

Agizo la Rais laponyesha mashine ya MRI Muhimbili

Agizo la Rais John Magufuli la kutaka mashine za uchunguzi wa magonjwa za CT Scan na MRI za Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, limetekelezwa baada ya mashine moja ya MRI kuanza kufanya kazi saa tisa alasili jana.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani