Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


IPTL yamdai Zitto fidia bil.500/-

KAMPUNI ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), imefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakimtaka Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe awalipe fidia ya Sh bilioni 500 kutokana na kutoa kashfa dhidi yao.

habarileo

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

KwanzaJamii

IPTL yamdai Zitto bilioni 500/- kortini

Na Karama Kenyunko Wiki chache baada ya kumshtaki Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, Kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na wenzake wawili, sasa imemgeukia Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe kwa kumfungulia kesi ya madai ya fidia ya Sh. bilioni 500  Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam. IPTL pamoja na wadai wenzake wanaiomba mahakama imwamuru Zitto kulipa fidia hiyo kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao...

 

11 years ago

Habarileo

Bil.6.8/-kutumika kulipa fidia Makambako hadi Songea

SERIKALI imetenga zaidi ya Sh bilioni 6.8 kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi walioko kandokando mwa barabara kuu kutoka Makambako hadi Songea.

 

11 years ago

Mwananchi

IPTL yamtaka Kafulila kulipa fidia ya Sh310 bilioni

Sakata la tuhuma za wizi wa pesa katika Akaunti ya Escrow ndani ya Benki Kuu (BoT) sasa limehamia mahakamani baada ya Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kumfungulia mashtaka Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR- Mageuzi), David Kafulila.

 

11 years ago

Habarileo

Gazeti la Mawio na mwandishi wake Jabir wadaiwa fidia bil.2/-

MKURUGENZI Mtendaji wa kampuni ya AP Media and Consultant Limited, Peter Keasi, amefungulia shauri la madai dhidi ya Mhariri wa gazeti la kila wiki la Mawio na mwandishi wa gazeti hilo, Jabir Idrissa, akidai fidia ya Sh billioni mbili kwa madai ya kukashifiwa.

 

11 years ago

Tanzania Daima

Miradi ya BRN yatafuna bil. 500/-

SERIKALI imetumia zaidi ya sh bilioni 500 kwa ajili ya utekeleaji wa miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2013. Hayo yalisemwa jana na kiongozi...

 

10 years ago

Mtanzania

Saa za waliochota Sh bil 321 IPTL zahesabika

Abdulrahman Kinana

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kila aliyehusika katika kashfa ya uchotwaji wa Sh bilioni 321 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), abebe msalaba wake bila kujali cheo chake na kwamba muda wa kulindana umekwisha.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye walipokuwa wakihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Ilulu...

 

11 years ago

Habarileo

Serikali yatumia bil. 500/- miradi ya Matokeo Makubwa

SERIKALI imetumia zaidi ya Sh bilioni 500 katika utekelezaji wa miradi ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) katika kipindi cha miezi sita, kati ya Julai na Desemba mwaka jana.

 

11 years ago

Michuzi

IPTL, Al-Madinah washerehekea sikukuu ya Eid na mayatima 500


Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL Bw. Aidan Kaune (mwenye suti ya kijivu) akijumuika pamoja na baadhi ya watoto 500 mayatima kusherehekea sikukuu ya Eid wakati wa karamu ya chakula iliyoandaliwa na taasisi ya Al-Madina na kufadhiliwa na IPTL. Kulia ni meneja maswala ya kampuni ya IPTL (Company Affairs Manager) Bw. Kulwinder Singh Jheeta na wa tatu kulia ni Mkurugenzi wa taasisi ya Al-Madinah Sheikh Ally Mubarak.  Meneja rasilimali watu wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL...

 

10 years ago

Mtanzania

IPTL yamshtaki Zitto

Zitto Kabwe

Zitto Kabwe

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na wadai wengine wawili, wamefungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini,  Zitto Kabwe (Chadema).

Pia IPTL imewafungulia kesi watu wengine wawili, huku wakitaka kulipwa fidia ya Sh. bilioni 500.

Mbali na IPTL, wengine waliofungua kesi hiyo  Septemba 4, mwaka huu kupitia wakili Melchisedeck Lutema wa Asyla Attorneys na  Kay Felician Mwesiga...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani