KILICHOMPONZA ASKOFU GWAJIMA CHAJULIKANA
![](http://api.ning.com:80/files/Z-JJSpQIZ68nflh*yi*KOkfEZovvvUmYktR6Vd4*dRitkb*zQqvHoae7HYp4Iq2Xfu5inz5-F4V6UVwhCnPnOaBlWRT20H-9/Gwajima.jpg?width=650)
Na Waandishi Wetu Imejulikana kwamba kilichomponza Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (pichani) pamoja na madai ya kutumia maneno yenye kuudhi kwa Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycap Kadinali Pengo mambo ya kisiasa yametajwa kuwa ndiyo msingi wa kushughulikiwa kwake. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima. Gwajima anadaiwa kushabikia upande mmoja wa kisiasa katika...
GPL
Habari Zinazoendana
10 years ago
Mtanzania03 Apr
Askofu Gwajima taabani polisi
NA ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM
HALI ya afya ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imebadilika ghafla baada ya kushindwa kupanda ngazi katika ofisi za Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana.
Askofu Gwajima alifika kituoni hapo saa 2 asubuhi akiwa ameongozana na maaskofu zaidi ya watano.
Katika hali ya kushangaza, wakati akipanda ngazi kuelekea kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alifanikiwa kupanda mbili, lakini alipojaribu ya...
10 years ago
Habarileo12 Apr
Askofu Gwajima ajipalia makaa
HATUA ya mawakili wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kutengeneza ubishi wa kisheria katika agizo la Polisi la kuwasilisha nyaraka za mali za Askofu huyo, imeelezwa kuwa ni ukaidi ambao hautamsaidia kisheria.
10 years ago
Mtanzania31 Mar
Sura mbili za Askofu Gwajima
NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
SIKU chache baada ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukamatwa na kuhojiwa na polisi na hatimaye kuzimia, utata mpya umeibuka juu ya kiongozi huyo wa kiroho.
Utata huo unahusu uraia, historia yake, utajiri na umiliki wa silaha ambayo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadai haina kibali huku yeye akidai ana vibali vyote.
Hali hiyo imeibuka huku nyuma ya pazia kukiwa na sintofahamu juu ya hatima yake.
Ingawa Askofu Gwajima,...
10 years ago
Habarileo27 Mar
Polisi wamsaka Askofu Gwajima
POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wamefungua jalada la uchunguzi dhidi ya tuhuma za Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima za tuhuma za kumkashifu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki, Mwadhamana Polycarp Kardinali Pengo.
9 years ago
Mwananchi08 Sep
Dk Slaa asubiri majibu ya Askofu Gwajima
10 years ago
Mtanzania30 Mar
Askofu Gwajima ataka kutoroshwa Kimafia
Na Waandishi Wetu,Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia wafuasi 15 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa tuhuma za kutaka kumtorosha Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Josephat Gwajima.
Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam, baada ya kupata mshituko wakati akihojiwa na makachero wa Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu...
9 years ago
Mzalendo Zanzibar05 Sep
Tenesco yamshtaki Askofu Gwajima Polisi
Askofu Josephat Gwajima Imeandikwa na Theopista Nsanzugwanko Imechapishwa: 04 Septemba 2015 Askofu Josephat Gwajima SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limelishtaki Polisi Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kutokana na kuharibu miundombinu ya […]
The post Tenesco yamshtaki Askofu Gwajima Polisi appeared first on Mzalendo.net.
9 years ago
Habarileo04 Sep
Tanesco yamshtaki Askofu Gwajima Polisi
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeishtaki polisi Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kutokana na kuharibu miundombinu ya umeme katika maeneo ya shirika hilo Jumamosi iliyopita na kusababisha umeme kukatika kwa baadhi ya mikoa na Jiji la Dar es Salaam.
10 years ago
Mtanzania08 Apr
Askofu Gwajima aligomea Shirika la Nyumba
Na Asifiwe George, Dar es Salaam
MCHUNGAJI Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwandu Mwangasa, amesema kamwe hawawezi kuhamisha kanisa lao lililopo katika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya gazeti moja la kila siku (si MTANZANIA) kumnukuu Meneja Uhusiano wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Yahaya Charahani akisema wametoa notisi ya mwezi mmoja kwa kanisa hilo linaloongozwa na Mchungaji Josephat Gwajima kuhama katika viwanja...