Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Askofu Gwajima ataka kutoroshwa Kimafia

gwajimaNa Waandishi Wetu,Dar es Salaam
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia wafuasi 15 wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kwa tuhuma za kutaka kumtorosha Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Josephat Gwajima.
Gwajima ambaye amelazwa katika Hospitali ya TMJ, Mikocheni Dar es Salaam, baada ya kupata mshituko wakati akihojiwa na makachero wa Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

Lowassa azindua helkopta ya kanisa la ufufuo na uzima, Askofu Gwajima ataka apewe eneo la Tanganyika Parkers

Joseph Zablon, Kawe Dar es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ameahidi kumsaidiana kwa maombi na njia zingine, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ili aweze kulipata eneo la Tanganyika Pakers analolitumia kwa mahubiri ili ajenge kanisa kwa ajili ya waumini wake. Kauli ya Lowassa imefuatia ombi la askofu huyo wakati wa uzinduzi wa helkopta ya kanisa hilo ambayo ameahidi kuitumia kwa ajili ya kusaidia majanga yanapotokea na pia kusambaza neno la Mungu ambako alidai...

 

10 years ago

Habarileo

Polisi wamsaka Askofu Gwajima

Josephat GwajimaPOLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam wamefungua jalada la uchunguzi dhidi ya tuhuma za Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima za tuhuma za kumkashifu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki, Mwadhamana Polycarp Kardinali Pengo.

 

10 years ago

Habarileo

Askofu Gwajima ajipalia makaa

Josephat GwajimaHATUA ya mawakili wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kutengeneza ubishi wa kisheria katika agizo la Polisi la kuwasilisha nyaraka za mali za Askofu huyo, imeelezwa kuwa ni ukaidi ambao hautamsaidia kisheria.

 

10 years ago

GPL

KILICHOMPONZA ASKOFU GWAJIMA CHAJULIKANA

Na Waandishi Wetu
Imejulikana kwamba kilichomponza Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (pichani) pamoja na madai ya kutumia maneno yenye kuudhi kwa Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Polycap Kadinali Pengo mambo ya kisiasa yametajwa kuwa ndiyo msingi wa kushughulikiwa kwake. Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima. Gwajima anadaiwa kushabikia upande mmoja wa kisiasa katika...

 

10 years ago

Mtanzania

Sura mbili za Askofu Gwajima

NA WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
SIKU chache baada ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kukamatwa na kuhojiwa na polisi na hatimaye kuzimia, utata mpya umeibuka juu ya kiongozi huyo wa kiroho.
Utata huo unahusu uraia, historia yake, utajiri na umiliki wa silaha ambayo Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linadai haina kibali huku yeye akidai ana vibali vyote.
Hali hiyo imeibuka huku nyuma ya pazia kukiwa na sintofahamu juu ya hatima yake.
Ingawa Askofu Gwajima,...

 

10 years ago

Mtanzania

Askofu Gwajima taabani polisi

NA ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM

HALI ya afya ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, imebadilika ghafla baada ya kushindwa kupanda ngazi katika ofisi za Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam jana.

Askofu Gwajima alifika kituoni hapo saa 2 asubuhi akiwa ameongozana na maaskofu zaidi ya watano.

Katika hali ya kushangaza, wakati akipanda ngazi kuelekea kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alifanikiwa kupanda mbili, lakini alipojaribu ya...

 

10 years ago

Mwananchi

Askofu Gwajima sasa aja kivingine

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameliombea Taifa ili liepukane na ajali za barabarani, akisema nyingi zinasababishwa na kafara zinazofanywa na baadhi ya watu aliowaita wabaya.

 

10 years ago

Mwananchi

Kardinali Pengo amjibu Askofu Gwajima

>Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema, amemsamehe Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye hivi karibuni alimtolea maneno makali kutokana na kutofautiana naye juu ya msimamo wa viongozi wa Kikristo kuhusu Katiba Inayopendekezwa.

 

9 years ago

Habarileo

Tanesco yamshtaki Askofu Gwajima Polisi

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeishtaki polisi Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima kutokana na kuharibu miundombinu ya umeme katika maeneo ya shirika hilo Jumamosi iliyopita na kusababisha umeme kukatika kwa baadhi ya mikoa na Jiji la Dar es Salaam.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani