Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Kundi hatari laibuka

Godfrey-KamwelaNa Mwandishi Wetu, Kilimanjaro

Kundi hatari la vijana limeibuka wilayani mwanga mkoani Kilimanjaro na kuzua hofu. Kundi hilo la vijana wapatao 40, wanadaiwa kupewa mafunzo ya kijeshi na watu wasiofamika wilayani humo.
Vijana hao kwa muda wa miezi kadhaa inadaiwa wamekuwa wakipewa mafunzo ya kijeshi katika vijiji vya Lang’ata na Kirya kwa lengo la kuandaliwa kufanya matukio ya kihalifu nchini.
Habari za uhakika kutoka wilayani Mwanga zinasema hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa kwa wananchi...

Mtanzania

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Dewji Blog

Wajumbe Kundi la 201 watoa tamko dhidi ya wanaolichafua Bunge Maalum la Katiba na Wajumbe wa kundi hilo

PIX 1

Askofu Amos Muhagachi akitoa tamko juu ya tuhuma mbalimbali dhidi ya kundi la 201 la wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba jana 03 Septemba, 2014 katika Ukumbi wa Spika, Mjini Dodoma.

Na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma.

WAWAKILISHI wa Taasisi za dini wa Bunge Maalum la Katiba toka wajumbe 201 wametoa tamko lao dhidi ya tuhuma mbalimbali zinazoendelea katika kulichafua Bunge hilo ikiwemo baadhi ya wajumbe wa kundi hilo wakituhumiwa kudaiwa kupewa rushwa.

Tamko hilo limetolewa jana 03 Septemba,...

 

11 years ago

Michuzi

BARABARA KIJICHI - MBAGALA KUU NI HATARI ZAIDI YA HATARI!

Barabara ya Kijichi – Mbagala Kuu, ndani ya jiji la Dar es Salaam kama ilivyokutwa jana na Mdau Nathan Mpangala. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Butiama, Bw. Haji Mgaya, alisema, dhahma hiyo ni ya muda mrefu na Manispaa ya Temeke ina taarifa hiyo kwa kupindi chote hivyo,lakini mpaka leo iko kimya tu.  Hapa dereva ‘akilala’ tu, kilio kitongoji kizima zikifuatiwa na salamu za rambirambi nyiiingi toka kwa viongozi. Inawezekana Manispaa ya Temeke haina picha halisi ya hatari...

 

11 years ago

GPL

KANISA LA WALA NYASI LAIBUKA!

Stori: Mwandishi Wetu
KUNA mengi ambayo yamekuwa yakizungumzwa kuhusu huduma za watumishi mbalimbali wa kiroho, moja wapo ni hili la kuanzishwa kanisa la wala nyasi nchini. Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kanisa hilo lipo maeneo ya Upanga jijini Dar na huduma yao inafanywa kwa kutumia jina la Rabboni Centre Ministries yenye makao yake makuu jijini Pretoria, Afrika Kusini. Gazeti hili lilifika Upanga, kwenye nyumba...

 

11 years ago

GPL

GONJWA JINGINE LAIBUKA BONGO

Mbu wa Aedes aegypti anayesambaza gonjwa hatari la Chikungunya pamoja na homa ya Dengue. Majanga! Huku hali ya sintofahamu ikiendelea kuwakumba wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam na nchi nzima kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa homa ya Dengue, gonjwa lingine hatari lisilo na chanjo wala tiba limezuka, Risasi Jumamosi linakuwa la kwanza kukujuza. Gonjwa hilo liitwalo Chikungunya, linasambazwa na virusi wa jamii ya...

 

10 years ago

Mtanzania

Timbwili laibuka mkutano Simba

simbaNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

MKUTANO mkuu wa dharura wa klabu ya Simba ulifanyika jana kwenye Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam, huku ukiibua timbwili baada ya baadhi ya wanachama kutoleana lugha chafu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wanachama 514, lakini sehemu kubwa ya viti ilionekana kuwa tupu tofauti na ilivyotarajiwa, huku ukihusisha ajenda tatu, ya kwanza ambayo ni kubwa ilihusu kujadili mwenendo wa mbaya wa Simba kwenye Ligi Kuu ya Vodacom.

Ajenda ya pili...

 

9 years ago

GPL

GONJWA LA AJABU LAIBUKA JIJINI DAR

Haruni Sanchawa na Makongoro Oging’ Mshituko mkubwa umewakumba wakazi wa Kijitonyama Kwaally Maua B, wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam baada ya Ijumaa kuamkia Jumamosi iliyopita kuibuka kwa ugonjwa wa ajabu ulioua watu wawili ghafla na kuwapa hofu kubwa wakazi wa eneo hilo.  .....Soma zaidi====>http://bit.ly/1IZ0iNF

 

10 years ago

Bongo Movies

Bifu la Wema na Kajala Laibuka Upya!

Bifu la kati ya waigizaji  marafiki wa zamani Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Kajala Masanja ‘Kay’ inadaiwa kuwa limeibuka tena upya mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Madam kuanika ubaya aliotendewa na Kajala aliyewahi kumlipia faini ya shilingi milioni 13 na kumuepusha na kifungo cha miaka 7 jela, Machi 25, 2013, kupitia kipindi chake cha In My Shoes kinachorushwa na  kituo cha televisheni cha EATV.

Wafuasi na mashabiki wa Kajala hawakufurahishwa na maneno ya Wema ambayo walidai yalikuwa...

 

11 years ago

Habarileo

Sakata la misamaha ya kodi laibuka upya

KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeibua upya matatizo ya misamaha ya kodi bungeni na kubainisha wazi kuwa tatizo hilo linazidi kuwa kubwa siku hadi siku, ambapo kwa mwaka wa fedha 2011/2012 misamaha ya kodi iliyotolewa ilikuwa ni asilimia 13 sawa na bajeti ya mwaka huo wa fedha iliyokuwa Sh trilioni 13.5.

 

10 years ago

Mwananchi

Sakata la jengo la ATCL kupigwa mnada laibuka tena

Kampuni tatu zimewasilisha maombi katika Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara zikitaka jengo la Makao Makuu ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) lenye thamani ya Sh12 bilioni lipigwe mnada kufidia madeni yao yanayofikia zaidi ya Sh2 bilioni.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani