Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


KWA NINI GLOBAL PUBLISHERS IMEAMUA KUPAMBANA NA HOMA YA INI?

Mgonjwa mwenye Hepatitis B ngozi na macho yake vikiwa vya njano. Na Mwandishi Wetu
Taifa la Tanzania lipo kwenye hatari kubwa. Hepatitis B (homa ya ini) ni janga la kitaifa na dunia kwa jumla. Nchi yetu (Tanzania) ipo Kusini ya Jangwa la Sahara, eneo ambalo kijiografia ndilo hatari zaidi ulimwenguni kwa maambukizi. Ni ugonjwa hatari ambao hauna tiba ya moja kwa moja lakini kinga ipo. Jambo la kuhuzunisha ni kwamba wananchi...

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

11 years ago

GPL

KAMPENI YA KUPAMBANA NA HOMA YA INI YAZINDULIWA JIJINI DAR

Mganga Mkuu Hospitali ya Amana, Dk. Meshack Shimwela, akielezea madhara ya ugonjwa wa Homa ya Ini. Shigongo akiwaomba wadau mbalimbali kupambana dhidi ya ugonjwa wa Homa ya Ini.…

 

11 years ago

GPL

SAID MECKY SADICK AZINDUA RASMI KAMPENI YA KUPAMBANA NA HOMA YA INI AMANA, DAR

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Said Mecky Sadick akizundua rasmi kampeni ya kupambana na ugonjwa hatari wa Homa ya Ini. Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo akielezea madhara ya ugonjwa wa Homa ya Ini wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupambana na ugonjwa huo.…

 

11 years ago

GPL

GLOBAL KUIPINGA HOMA YA INI NCHI NZIMA

KAMPENI ya kutokomeza homa ya ini (Hepatitis B), iliyoanzishwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, imewekewa wigo mpana wa kufika nchi nzima. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd, Eric Shigongo. Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo, alimweleza mwandishi wetu kuwa kampeni hiyo imeanzishwa kwa nia ya dhati kabisa ya kumkomboa Mtanzania dhidi ya...

 

11 years ago

GPL

MKUU WA MKOA AIPONGEZA GLOBAL KUASISI HARAKATI ZA HOMA YA INI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick (kulia) akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo baada ya kuzindua Kampeni ya Homa ya Ini. Na Mwandishi Wetu
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick ameipongeza Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd kwa kuwaza vizuri kisha kuamua kuanzisha harakati za kupambana na ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B). Said Meck Sadick… ...

 

11 years ago

Habarileo

RC Dar ataka tahadhari homa ya ini kwa watoto

MKOA wa Dar es Salaam umesema watoto waliozaliwa kabla ya mwaka 2008 hawana kinga ya ugonjwa wa homa ya ini, hivyo imeagiza Manispaa zote kuwapima na kuwapatia kinga ili kukabiliana na ugonjwa huo hatari. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki alisema hayo leo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani na kuwasisitiza wanawake kuhakikisha wanapatiwa chanjo ya ugonjwa huo hasa wakati wa ujauzito.

 

11 years ago

GPL

DAMU SALAMA: MAAMBUKIZI YA HOMA YA INI YAZIDI UKIMWI KWA 5.6%

Ofisa Uhusiano Mpango wa Taifa wa Damu Salama,  Rajab Mwenda, akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani).  Kulia ni ofisa kutoka Msalaba Mwekundu, Evelyne Kussaga.
Waandishi wa habari wakisikiliza maelezo kutoka kwa maofisa wa Damu Salama.…

 

11 years ago

GPL

UZINDUZI HOMA YA INI LEO

Shigongo akizungumza kwa masikitiko jinsi watu wengi walivyo kwenye hatari ya kufa kwa ugonjwa wa ini. Stori: RICHARD BUKOS KAMPENI ya ugonjwa wa Homa ya Ini unaosambazwa na Virusi vya Hepatitis B inazinduliwa rasmi leo, Machi 7, mwaka huu katika Hospitali ya Mkoa wa Kitabibu Ilala – Amana, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na Ijumaa, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers ambayo ndiyo inayoendesha kampeni...

 

11 years ago

GPL

WADAU WAONGEZEKA KAMPENI YA HOMA YA INI

Mkurugenzi Mtendaji wa Global Publishers, Eric Shigongo. Stori: Mwandishi Wetu
Kampeni iliyoanzishwa na Kampuni ya Global Publishers & General Enterprises Ltd ya mapambano dhidi ya homa ya Ini (hepatitis B), imepokelewa kwa mikono miwili baada ya wadau muhimu katika sekta ya afya kujitokeza. Taasisi za Damu Salama, SD Afrika na Sanofi Pasteur, wamejitokeza kuungana na Global kuhakikisha kuwa homa hiyo inatokomezwa nchini....

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani