Mabomu yaua 12, yajeruhi watu 137
WATU 12 wameuawa na wengine 137 kujeruhiwa katika matukio tisa ya ulipuaji mabomu yaliyotokea katika mikoa ya Arusha, Morogoro, Lindi, Dar es Salaam, Mwanza na Zanzibar.
Aidha, watu 25 wamekamatwa katika tukio la ulipuaji bomu lililofanyika hivi karibuni katika eneo la darajani kisiwani Zanzibar, ambapo mtu mmoja alifariki. Watano kati ya watu hao, wameshafikishwa mahakamani.
Hayo yalisemwa bungeni jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Perreira Ame Silima, alipokuwa akijibu swali...
Uhuru Newspaper
Habari Zinazoendana
9 years ago
Mtanzania17 Sep
Ajali yaua watu watatu, yajeruhi 51
Victor Bariety na Emanuel Ibrahim, Geita
WATU watatu wamefariki dunia na wengine 51 kujeruhiwa mkoani Geita, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupasua gurudumu kisha kupinduka.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alisema watu walifaki dunia katika ajali hiyo majina yao hajatambuliwa kutokana na miili yao kuharibika vibaya.
Alisema ajali hiyo, iliyotokea saa 3;30 asubuhi katika eneo la Nyantorotoro, ilihusisha basi la Sheraton lenye namba...
9 years ago
BBCSwahili14 Sep
Milipuko ya mabomu yaua watu 20 Syria
10 years ago
Habarileo20 Feb
Ajali yaua 2 yajeruhi 45
WATU wawili wamekufa papo hapo huku wengine 45 wakijeruhiwa baada ya basi la abiria lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kugongana uso kwa uso na roli katika kijiji cha Vikonje wilayani Chamwino mkoani hapa.
11 years ago
Habarileo22 Apr
Ajali ya basi yaua 10, yajeruhi 30
WATU 10 wamekufa papo hapo na wengine 30 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya basi la Luhuye Express lililokuwa likitoka wilayani Tarime mkoani Mara kwenda jijini Mwanza jana.
11 years ago
Tanzania Daima22 Jun
Ajali yaua 6, yajeruhi 12 Dar
WATU sita wamefariki dunia papo hapo na zaidi ya 12 kujeruhiwa katika ajali mbaya iliyohusisha magari manne. Akizungumzia tukio hilo lililotokea jana eneo la Makongo, jijini Dar es Salaam, Kamanda...
9 years ago
Mtanzania21 Dec
Ajali ya basi yaua mmoja, yajeruhi 46
NA ABDALLAH AMIRI, IGUNGA
MTU mmoja, amefariki dunia papo hapo na wengine 46 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Kampuni ya ALLY’S lenye namba za usajili T 560 AKW aina ya Scania, kupinduka katika Kijiji cha Igogo, Kata ya Nanga, Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora.
Ajali hiyo ilitokea jana, saa 12 alfajiri wakati basi hilo lilipokuwa likitoka wilayani Igunga kwenda jijini Mwanza.
Wakizungumza na MTANZANIA eneo la tukio baada ya ajali hiyo, mmoja wa abiria aliyenusurika, Emmanuel Julius (32),...
11 years ago
GPL![](http://api.ning.com/files/iC8gEB0kF6mBd7r6*8rSsXekJ*wCwi-bk9AUNlcLhatBnZpnFwCzLv2fq73rgAc5qaguKf20Ho7tClSIM8vg93ZfQThCBOFE/13.gif)
AJALI YAUA 6 TANGA, YAJERUHI ZAIDI YA 12
10 years ago
Habarileo23 Mar
Mvua yaua 5 Dar es Salaam, yajeruhi
HALI ni tete katika jiji la Dar es Salaam, kutokana na mvua ya masika iliyonyeshwa kwa siku tatu na kusababisha vifo vya watu watano, huku nyumba nyingi zikiwa zimezingirwa na maji.
10 years ago
Mwananchi27 Feb
Ajali yaua watatu, nyingine yajeruhi 21