Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Maofisa 12 wa TRA mbaroni kwa upotevu wa makontena

Maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wanaotuhumiwa kuitia Serikali hasara ya Sh80 bilioni kutokana na upotevu wa makontena 349, wametiwa mbaroni.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Michuzi

WAFANYAKAZI SABA WA TPA MBARONI KWA UPOTEVU WA MAKONTENA MPYA 11,884 NA MAGARI 2,019... WANANE WATOROKA

Waziri wa Uchukuzi, Ujenzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa. Na Chalila Kibuda,Globu ya JamiiBAADA ya  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  kufanya ziara  katika Mamlaka ya Bandari Nchini (TPA) na kubaini uondoshwaji wa wa kontena 329   bila kulipiwa kodi zaidi ya sh.bilioni 12,  Mawakala wa Forodha walifanya ukaguzi  kuona kama kuna upotevu wa mapato  na kubaini jumla ya kontena 11,884 na magari 2019 yalitolewa bila malipo.Makontena hayo yalitolewa katika bandari kavu ni MOFED 61, DICD 491,...

 

5 years ago

Michuzi

TAKUKURU MANYARA YAWATIA MBARONI MAOFISA WAWILI WA TRA

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini, (TAKUKURU) Mkoani Manyara, inawashikilia maofisa wawili wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) kwa kudaiwa kupokea rushwa ya shilingi milioni 10.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu (Pichani) akizungumza mjini Babati alisema maofisa hao TRA wanadaiwa kufanya kosa hilo kinyume cha kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007. 
Makungu aliwataja majina yao maofisa hao wa TRA wanaodaiwa kupokea rushwa ya...

 

9 years ago

Michuzi

TAARIFA YA UPOTEVU WA MAKONTENA AZAM ICD TOKA SSB Group of Companies

Kumekuwa na taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa kampuni ya Bakhresa inahusika na upotevu wa Makontena 349 yaliyoripotiwa hivi karibuni kuwa yametolewa bandarini bila kulipiwa ushuru. Taarifa hizo zilitolewa na Waziri Mkuu wakati wa ziara yake ya Bandari ya Dar es salaam hivi karibuni.

Uchunguzi wetu umeonyesha kuwa si kweli kuwa kuna makontena yenye bidhaa zilizoingizwa na kampuni hio ama ni miongoni mwa makontena yaliyohusika katika sakata hilo. Isipokuwa kumetokea upotevu...

 

9 years ago

Habarileo

TRA yagomea wamiliki wa makontena

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imewagomea kulipa kodi bila adhabu baadhi ya wamiliki wa makontena, ambayo yalitoroshwa kwenye bandari kavu bila kulipiwa kodi. Badala yake, TRA imewapelekea hati ya malipo inayowataka wafanyabiashara hao, kuhakikisha wanalipa kodi hiyo na adhabu ndani ya siku saba, la sivyo watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

 

9 years ago

Habarileo

Makontena yanaswa sakata TRA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata makontena tisa, yaliyotoroshwa kutoka katika bandari kavu na kuhamishiwa katika eneo la Mbezi Tangi Bovu, Dar es Salaam, hivyo kuwepo na kiashiria cha ukwepaji wa kodi.

 

9 years ago

Mwananchi

Vigogo wa TRA kesi ya makontena nje

Hatimaye vigogo watatu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) wanaokabiliwa na kesi ya uhujujmu uchumi kutokana na sakata la upotevu wa makotena 329 kutoka bandari kavu ya Azam, wamerejea uraiani baada ya kuachiwa kwa dhamana.

 

9 years ago

Mtanzania

TRA yakamata makontena tisa Dar

Pg 1 mbiliNA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imefanikiwa kukamata makontena tisa, mali ya Kampuni ya Heritage Limited yakiwa katika eneo la maficho ya Mbezi Tangi bovu, Dar es Salaam kinyume cha sheria.

Akizungumza kuhusu ukamataji huo akiwa eneo la tukio jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi TRA, Richard Kayombo, alisema taarifa hizo walipewa na msamaria mwema.

“Taarifa za kukamata makontena hayo tulipewa na msamaria mwema aliyetuambia kwamba usafirishaji...

 

11 years ago

Mwananchi

TRA: Hatuna taarifa za makontena ya magogo ya magendo

Mamlaka ya Kodi ya Mapato Tanzania Kanda ya Zanzibar (TRA), imesema haina taarifa kuhusu makontena 95 yenye mzigo wa magendo ya magogo yaliosafirishwa kupitia bandari ya Zanzibar yakielekea mataifa ya Mashariki ya Mbali, gazeti hili limebaini hilo jana.

 

9 years ago

StarTV

Wa Makontena TRA yakamata tisa Mbezi Tangibovu Dar

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA inayashikilia makontena tisa yanayodaiwa kuingizwa na kutolewa bandarini kinyume cha sheria ya ulipaji kodi ikitoa saa ishirini na nne kwa wamiliki wa makontena hayo kujisalimisha.

Makontena hayo yamekatwa kwenye eneo la Mbezi Tangibovu jijini Dar es Salaam, eneo ambalo kwa mujibu wa TRA halina kibali kisheria kuhifadhi makontena kama bandari kavu.

Taarifa za wasamaria wema, zinawafikisha mamlaka ya mapato nchini TRA, mamlaka ya bandari, (TPA) na jeshi la...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani