Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Masha apanda kizimbani, apata dhamana

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrance Masha jana alipandikishwa kizimbani pamoja na viongozi  sita wa Chadema mkoani Katavi, wakishtakiwa kwa tuhuma za kufanya mkutano wa hadhara na kuingia bila kibali kwenye kambi ya wakimbizi ya  Katumba wilayani Mlele.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Mwananchi

Masha apata dhamana

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani nchini, Lawrence Masha (45) baada ya kukamilisha masharti ya dhaman

 

9 years ago

GPL

MASHA AACHIWA KWA DHAMANA

Lawrence Masha akiwa na wanachama wa Ukawa baada ya kuachiwa. Baada ya jana kulala mahabusu ya segerea, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha leo ameachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana. Masha, ambaye anashitakiwa kwa kosa la kuwazuia Polisi wasifanye kazi ikiwa ni pamoja na kuwatolea lugha ya matusi. Jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo alisomewa mashtaka...

 

9 years ago

Mtanzania

Wanasheria wavalia njuga Masha kunyimwa dhamana

Laurence MashaNa Elias Msuya

CHAMA cha Wanasheria cha Tanganyika (TLS), kimelaani kitendo cha mwanachama wake ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Lawrence Masha, kunyimwa dhamana mahakamani.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, TLS imesema mahakama imekuwa na tabia ya kunyima watu haki yao hiyo kwa kisingizio cha kuhakiki nyaraka za dhamana.

Kutokana na hali hiyo, chama hicho kimesema kitaunda tume maalumu ya kuchunguza uvunjwaji wa taratibu za mahakama...

 

10 years ago

Mtanzania

Dk. Slaa apanda kizimbani

Pg 2Na Mwandishi Wetu, Hai
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amepanda kizimbani na kutoa ushahidi katika kesi utapeli dhidi ya mtu aliyetumia jina la Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta.
Katika kesi hiyo namba 117, Dk. Slaa ni shahidi wa nane na alisema kuwa mke wake, Josephine Mushumbuzi, ndiye aliyemsaidia kumgundua mtu aliyejaribu kumtapeli kwa kutumia jina la Jaji Samatta.
Alikuwa akituoa ushahidi jana katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi wa Wilaya...

 

11 years ago

Tanzania Daima

Naibu Meya apanda kizimbani

NAIBU Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe na Diwani wa Kata ya Levelos, Ephata Nanyaro, wote kutoka CHADEMA, wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kumshambulia mgambo wa jiji, William Mollel....

 

10 years ago

Habarileo

Gwajima apanda kizimbani Kisutu

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (45), akiwasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.HATIMAYE Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (45), amepanda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka mawili, ikiwemo la kutumia lugha ya matusi dhidi ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam la Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.

 

11 years ago

Mwananchi

Sheikh Farid apanda kizimbani Kisutu

Kiongozi wa Jumuiya za Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheikh Farid Hadi Ahmed (43) na mwenzake Jamal Nooridin Swalehe (38), wameunganishwa na watu wengine 18 wanaoshtakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwamo la kula njama ya kuingiza watu nchini kushiriki katika vitendo vya ugaidi.

 

10 years ago

Mwananchi

Jaji Mkuu mstaafu ‘apanda kizimbani’

Jaji Mkuu mstaafu, Barnabas Samatta jana alipanda kizimbani kutoa ushahidi katika Mahakama ya Wilaya ya Hai tukio lililovuta hisia za wananchi wengi kwani ni la kwanza na la aina yake kwa kiongozi wa juu wa mhimili huo wa dola.

 

10 years ago

Mwananchi

Lema naye ‘apanda kizimbani’ Hai

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amedai mshtakiwa aliyejifanya Jaji mstaafu, Barnabas Samatta, alimtisha kuwa angehakikisha anashindwa katika rufaa yake ya kupinga kuvuliwa ubunge.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani