Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Mitihani kidato cha nne upo palepale

Wakati Rais Jakaya Kikwete akitangaza kuwa leo ni siku ya mapumziko nchi nzima ili kutoa nafasi kwa Watanzania kushiriki na kufuatilia sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule, Dk John Magufuli kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, wanafunzi wa kidato cha nne wataendelea na mitihani yao ya kuhitimu elimu ya sekondari kama kawaida.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Habarileo

'Kidato cha nne msiibe mitihani'

WANAFUNZI wa Kidato cha Nne wanaotarajiwa kufanya mtihani wa taifa wameonywa kujiepusha na vishawishi vya kushiriki kwenye wizi wa mitihani na udanganyifu mwingine utakaowaondolea sifa ya kuendelea kufanya mitihani yao.

 

9 years ago

StarTV

Watahiniwa kidato cha nne waanza mitihani

Wanafunzi wa kidato cha nne nchini wameanza mitihani  ya Taifa ya kuhitimu elimu ya sekondari huku hali ya utulivu ikitawala katika vituo vyote vya kufanyia mitihani hiyo.

Mitihani hiyo imeanza Novemba 2 hadi 27 na jumla ya watahiniwa 4,634 ndiyo wanaofanya mitihani hiyo huku  960 wakiwa ni watahiniwa wa kujitegemea.

 Startv imetembelea katika baadhi ya shule ambapo mitihani hiyo inafanyika na kushuhudia wanafunzi wakiwa wanajisomea kwa ajili ya kujikumbusha kile walichofundishwa.

Monica...

 

10 years ago

Mwananchi

Watahiniwa kidato cha nne kuanza mitihani rasmi

  Wanafunzi 297,488 wa kidato cha nne katika shule mbalimbali nchini, wanaanza mtihani wa kuhitimu utakaokamilika baada ya siku 20 huku watahiniwa wakionywa kujiepusha na vitendo vya udanganyifu.

 

10 years ago

GPL

MITIHANI YA KIDATO CHA NNE YAANZA, GPL YATEMBELEA MANZESE DAR

Wanafunzi  wakijisomea ili kukabiliana na mtihani unaofuata. Mwanafunzi akipitia  daftari lake kabla ya kuingia darasani. Baadhi ya wanafunzi wakiwa mapumziko kusubiri mtihani.…

 

11 years ago

Michuzi

BARAZA LA MITIHANI LAPANGUA MFUMO MZIMA WA KUPANGA MADARAJA YA UFAULU KIDATO CHA NNE NA TANO


Matokeo ya Mtihani wa Majaribio (Mock) kwa mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu na Kidato cha Sita mwakani, yatachangia alama 10 za Alama Edelevu (CA). Kwa utaratibu huu, matokeo ya mwisho ya mtahiniwa, yatatokana na asilimia 30 ya Alama Endelevu na asilimia 70 ni mchango wa Alama za Mtihani wa Taifa.  Asilimia 30 za Alama Endelevu, zitapatikana kutokana na mitihani mbalimbali. Kwa Kidato cha Nne mwaka huu, alama hizo zitatokana na matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha pili ambao...

 

5 years ago

Michuzi

MKURUGENZI KAGURUMJULI APONGEZWA KINONDONI KUONGOZA MARA NNE MFULULIZO MATOKEO KIDATO CHA NNE NA PILI KIMKOA


Mkuu wa shule ya Sekondari ya Canosa sister Irine Nakamanya akipokea cheti cha pongezi kwa shule hiyo kufanya vizuri kwenye matokeo ya kidato cha nne na pili.Wanafunzi na walimu waliokuwa katika hafla ya kupongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne na cha pili mwaka 2019. Hafla hiyo imeandaliwa na Idara ya elimu Sekondari.

 

10 years ago

Mtanzania

Mitihani kidato cha sita yaanza

shukuru-kawambwaGrace Shitundu na Michael Sarungi, Dar es Salaam
MTIHANI wa kidato cha Sita ulioanza jana nchini kote umeendelea licha ya mgomo wa madereva uliofanyika na kusababisha tatizo la usafiri.
Mtanzania ilifanikiwa kuzunguka katika baadhi ya shule zilizopo katikati ya jiji la Dar es Salaam ambazo ni Tambaza, Jangwani na Azania na kukuta wanafunzi wakiendeleea na mitihani yao.
Hata hivyo baadhi ya walimu waliliambia gazeti hili kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wamechelewa kufika katika chumba cha...

 

9 years ago

Mtanzania

Wanafunzi kidato cha pili waanza mitihani

dk-charles-e-msondeNa Jonas Mushi, Dar es Salaam

BARAZA lA Mitihani Tanzania (NECTA) limesema wanafunzi 397, 250 wa kidato cha pili wameanza kufanya Mitihani ya Upimaji wa Kitaifa wa Kidato cha Pili (FTNA) ikijumuisha wavulana 197,452 sawa na asilimia 49.70 na wasichana 199,798 sawa na asilimia 50.30.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema mitihani hiyo ilianza jana katika shule za sekondari 4,764 za Tanzania bara na itamalizika...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani