MSHAURI WA ULAYA WA TAASISI YAKUDHIBITI MAGONJWA YA MIFUGO AKUTANA NA BALOZI KAMALA
Mshauri wa Ulaya wa taasisi ya kudhibiti magonjwa ya mifugo (GALVmed) Dr. Joris Vandeputte akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania BELUX, Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala ofisini kwake. Dr Joris amemtembelea Balozi Kamala kumweleza mipango ya taasisi ya GALVmend ya kusaidia Tanzania na nchi za ACP kupambana na magonjwa ya mifugo.
Michuzi
Habari Zinazoendana
11 years ago
MichuziBALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI WA MAENDELEO WA JUMUIYA YA ULAYA
Mwenyekiti wa Mabalozi wa Nchi za Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo na Misaada wa Jumuiya ya Ulaya Mhe. Pierre Amilhat ( kushoto), Bi. Camilla Lombard Msaidizi wa Mhe Pierre (kulia) na Afisa wa Ubalozi wa Tanzania Ubelgiji Mhe. Nyamtara Mukome (wa pili kulia). Mhe Pierre amekutana leo na Balozi Kamala ofisini kwake Brussels kumweleza miradi mbalimbali inayotekelezwa na inayopangwa...
10 years ago
MichuziBALOZI KAMALA AKUTANA NA MBUNGE KIJANA WA BUNGE LA ULAYA
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimkabidhi Mhe. Victor Negrescu Mbunge wa Bunge Ulaya vitabu vya kuitangaza Tanzania. Mhe. Negrescu ni kati ya wabunge vijana sabini wa Bunge la Ulaya na leo hii alimtembelea Balozi Kamala ofisini kwake Brussels.
11 years ago
MichuziBALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA USALAMA WA CHAKULA YA UBELGIJI
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Usalama wa Chakula ya Ubelgiji Bwana. Pierre Nassens ( wa pili kutoka kushoto). Balozi Kamala ametembelea taasisi hiyo leo Brussels kushauriana nayo jinsi inavyoweza kushirikiana na Tanzania. Wengine katika picha ni wataalamu katika taasisi hiyo.
11 years ago
MichuziBALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA UWEKEZAJI NA BIASHARA YA BRUSSELS
Balozi wa Tanzania Belux na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uwekezaji na Biashara ya Brussels Bi. Benedicte Wilders (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa wa taasisi hiyo Bwana. Philip Feytons. Balozi Kamala amekutana na viongozi hao leo hii Brussels kuwaomba wahimize makampuni ya Brussels kushiriki ziara ya kibiashara inayoandaliwa kufanyanyika Tanzania mwishoni mwa mwaka huu.
11 years ago
MichuziBALOZI KAMALA AKUTANA NA MENEJA WA UWEKEZAJI WA TAASISI YA UWEKEZAJI YA WALLONIA YA UBELGIJI
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Uwekezaji wa Taasisi ya Uwekezaji ya Wallonia ya Ubelgiji Bi. Dominique Badot baada ya kumaliza kikao cha maandalizi ya Ziara ya Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Ubelgiji inayopangwa kufanyika Tanzania mwaka huu.
10 years ago
Michuzibalozi kamala akutana na katibu mkuu wa taasisi ya kusambaza umeme vijijini na Mkuu Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Jiji la Oestende la Ubelgji
Balozi wa Tanzania Ubelgji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Taasisi ya Kusambaza Umeme Vijijini katika nchi zinazoendelea Bwana. Marcus Wieman (katika). Bwana Wieman alikutana na Balozi Kamala leo Brussels kumweleza mipango ya taasisi yake ya kusambaza umeme vijijini katika nchi zinazoendelea.Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa wa Jiji la...
11 years ago
MichuziBalozi kamala akutana na balozi wa ubelgiji nchini tanzania
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye miwani) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Ubelgiji Tanzania Mhe. Adam Koeler (wa pili kutoka kulia) baada ya kumaliza kikao cha maandalizi ya ziara ya wadau wa sekta za miundombinu ya bandari, reli na kilimo itakayofanyika Ubelgiji kuanzia tarehe 19-23 Mei, 2014. Kikao kimefanyika nyumbani kwa Balozi wa Ubelgiji nchini Tanzania.
9 years ago
MichuziBALOZI KAMALA AAGANA VIONGOZI WA TAASISI YA WAFANYABIASHARA YA UBELIGIJI
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa taasisi ya Wafanyabiara Ubeligiji baada ya kumaliza kikao cha kuagana nao Brussels. Balozi Kamala anarejea Tanzania baada ya kumaliza kipindi chake cha Kuwa Balozi wa Tanzania Ubeligi, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya.
11 years ago
MichuziBALOZI KAMALA AKUTANA NA GAVANA WA HAINAUT UBELGIJI
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza katika tafrija iliyoandaliwa na Gavana wa Hainaut Mhe. Tommy Leclercq kuwashukuru wadau wa reli na bandari kutoka Tanzania kwa kutembelea Ubelgiji. Mhe. Leclercq ameahidi kushiriki ziara ya Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Ubelgiji watakaotembelea Tanzania mwaka huu.
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiweka sahihi Hati ya Mapokezi ya Hainaut huku Gavana wa Hainaut Mhe. Tommy Luclercq akishuhudia....
Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiweka sahihi Hati ya Mapokezi ya Hainaut huku Gavana wa Hainaut Mhe. Tommy Luclercq akishuhudia....
Top 10
Tanzania Today
Today Breaking News,Tanzania World News
13-February-2025 in Tanzania