Mvua yaua watu watatu, kaya zaidi ya 70 zakosa makazi
Watu watatu wamefariki dunia na familia zaidi ya 70 zimekosa mahala pa kuishi, huku mifugo zaidi ya 150 ikisadikiwa kufa baada ya kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Arumeru mkoani Arusha. Â Â Â
Mwananchi
Habari Zinazoendana
10 years ago
StarTV12 May
Athari ya mvua, Kaya 30 zakosa makazi Bukoba.
Na Mariam Emily,
Bukoba.
Athari za mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini zimezidi kuonekana, baada ya kaya thelathini katika eneo la Nyamkazi Manispaa ya Bukoba, kukosa makazi baada ya mvua kubwa inayonyesha mfululizo mjini humo kuharibu makazi yao pamoja na kupoteza mali kadhaa ikiwemo mazao ya chakula, mifugo pamoja na kuharibu miundombinu ya barabara.
Baadhi ya wananchi wamesema kiini cha mafuriko hayo ni mkondo wa maji kuzibwa na uchafu pamoja na mmea wa gugu maji...
11 years ago
Tanzania Daima01 Jan
Kaya 12 zakosa makazi Mtwara
KAYA 12 za wakazi wa Magomeni A katika Manispaa ya Mtwara-Mikindani mkoani hapa, wamekosa mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kubomolewa na mvua iliyonyesha hivi karibuni. Akizungumza na waandishi...
11 years ago
Habarileo28 Apr
Kaya 235 zakosa makazi Kyela
MBUNGE wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe amesema kaya 235 zenye wakazi 1,087 katika wilaya hiyo, zipo katika hali mbaya. Amesema kaya hizo zimeathiriwa vibaya na mafuriko, yaliyoikumba wilaya hiyo na kwamba sasa zimehamishiwa kwenye makanisa na shule ili kupewa msaada wa karibu.
9 years ago
Dewji Blog07 Dec
Kaya 19 zilizopo katika mpango wa kunusuru kaya maskini zakosa malipo yao Manyoni
Baadhi ya wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini wa Kijiji cha Sukamahela, tarafa ya Kilimatinde waliokosa malipo yao licha ya kuwa na taarifa na fomu za kupokelea malipo hayo, na kujikuta wakikaa kwa muda wa zaidi ya saa tano wakisubiri kuitwa wakapokee malipo hayo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sukamahela, Bwana Stephen Chilewa Mgusi (wa kwanza kutoa kulia), Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Sukamahela, Bwana Ernesti Gyunda Kitundu (wa pili kutoka kulia) na Mwezeshaji wa TASAF wilaya ya...
11 years ago
Habarileo15 Jan
Mvua yaacha watu 400 bila makazi
MVUA kubwa iliyoambatana na mawe na upepo mkali, imewaacha zaidi ya watu 400 katika kijiji cha Mwandoya wilayani Meatu mkoani Simiyu bila kuwa na mahali pa kuishi kutokana na nyumba zao kuezuliwa.
9 years ago
Mtanzania17 Sep
Ajali yaua watu watatu, yajeruhi 51
Victor Bariety na Emanuel Ibrahim, Geita
WATU watatu wamefariki dunia na wengine 51 kujeruhiwa mkoani Geita, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupasua gurudumu kisha kupinduka.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alisema watu walifaki dunia katika ajali hiyo majina yao hajatambuliwa kutokana na miili yao kuharibika vibaya.
Alisema ajali hiyo, iliyotokea saa 3;30 asubuhi katika eneo la Nyantorotoro, ilihusisha basi la Sheraton lenye namba...
10 years ago
Habarileo05 Mar
Mvua yaua watu 38 Kahama
MAAFA makubwa yameikumba Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga baada ya watu 38 kufa papo hapo na wengine 82 kujeruhiwa, kutokana na mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali, iliyonyesha katika Kijiji cha Mwakata Kata ya Isaka.
11 years ago
Habarileo13 Apr
Mvua yaua watu, nyumba zasombwa
MVUA iliyonyesha juzi na jana, ikiambatana na upepo mkali katika mikoa mbalimbali nchini, imeleta madhara na kusababisha vifo vya watu kadhaa. Jijini Dar es Salaam, nyumba nyingi zimebomolewa na kuzingirwa na maji, na miundombinu imekatika, ikiwemo kufunikwa kwa madaraja muhimu na adha za kila aina.
10 years ago
Mwananchi05 Mar
Mvua ya mawe yaua watu 42 Kahama, 91 wajeruhiwa