Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Nyumba 15 zachomwa moto Isodero Geita

Wakazi wa kijiji cha Idosero na Saragulwa Mkoani Geita wamedai kuvamiwa katika vijiji vyao na Wakala wa Misitu  na kuharibiwa mazao na nyumba kumi na tano kuchomwa moto kwa madai ya kuwa wananchi hao wamejenga na kulima ndani ya Hifadhi.

Wananchi hao wamesema wameshangaa kuvamiwa bila taarifa yoyote na kuharibiwa mali zao na nyingine kuchukuliwa na watu wa Misitu hali iliyorudisha nyuma nguvu kazi kwa kukosa mahala pa kuishi na kuiomba Serikali kuingilika kati na kulishughulikia suala la...

StarTV

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Habarileo

Nyumba 13 zachomwa moto, 35 wakosa makazi

RPC, Valentino MlowolaWATU 35 wakazi wa kitongoji cha Iroba kisiwani Bwiro wilaya ya Ukerewe, Mwanza hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao 13 kuchomwa moto katika tukio linalohusishwa na imani za kishirikina.

 

11 years ago

Mwananchi

Nyumba 24 zachomwa moto wakituhumiwa kuua watu 5

Geita. Zaidi ya nyumba 24 zimevunjwa na kuteketezwa moto Kijiji cha Kilombero, mkoani Geita na wananchi kutokana na mauaji ya Felister Mathias (55), anayedaiwa kuuawa kwa kukatwa mapanga na watu wa ukoo mmoja.

 

9 years ago

Vijimambo

Nyumba tisa zachomwa moto Z'bar Dk. Magufuli akitangazwa mshindi.

Nyumba tisa zimeteketezwa kwa moto katika kisiwa cha Tumbatu Kaskazini Unguja muda mfupi baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kutangaza ushindi wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, baadhi ya wafuasi na wanachama wa CCM kisiwani hapo walianza kushangilia ushindi huo. Hata hivyo, wakati wakiendelea kushangilia ushindi huo huku wakilidhihaki kundi lingine hali iliyosababisha warushiane...

 

10 years ago

Vijimambo

Nyumba za mtuhumiwa ujambazi zachomwa

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Suzana Kaganda
Wananchi wa kata ya Igurubi Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, wameteketeza nyumba tano za mtu wanayemtuhumu kuwa jambazi.

Kufuatia kitendo hicho, wananchi hao sasa wamelazimika kuzikimbia nyumba zao kuhofia kukamatwa na Jeshi la Polisi ili mkono wa sheria uchukue mkondo wake.

AFISA MTENDAJI ANENA
Afisa Mtendaji wa Kata ya Igurubi, Mdeka Said, akizungumza na NIPASHE jana, alisema wananchi hao walichoma nyumba hizo zinazomilikiwa na Mahona Malendeja,...

 

10 years ago

Habarileo

Nyumba 12 zachomwa kwa tuhuma za kufanya vurugu

WAKAZI wa Kijiji cha Mingenyi, Kata ya Gehandu, wilayani Hanang’ mkoani Manyara, wamechoma nyumba 12 zinazoishi kaya 50 wakiwatuhumu kufanya vurugu wakati wa kurudiwa kwa uchaguzi wa Serikali za mitaa katika eneo hilo.

 

10 years ago

Vijimambo

MAGARI TISA YATEKETEZWA KWA MOTO, NYUMBA 16 ZATIWA MOTO MGOGORO WA ENEO LA MALISHO SIHA

Mabaki ya nyumba yaliyoteketezwa kwa moto na wafugaji wa kimasaii wakidai eneo la malisho yao.(picha: Elias Kija, Siha, Kilimanjaro)Jeshi la Polisi likiwa limeimarisha ulinzi katika kijiji cha Miti-Mirefu wilayani Siha. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiliangalia mojawapo la gari la mwekezaji lililochomwa moto katika eneo la Ndarakwai. Mwekezaji wa eneo la Ndarakwai wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Peter Jones akizungumza na wanahabari katika eneo la tukio.Kwa picha na maelezo...

 

9 years ago

GPL

NYUMBA YA BATULI YATEKETEA MOTO

Imelda Mtema POLE sana! Staa mwenye mvuto mkubwa Bongo Movies, Yobunesh Yusuph ‘Batuli’ amepata pigo kufuatia nyumba anayoishi Mbezi Beach jijini Dar kuungua moto na kuteketeza vitu vyote ndani, Risasi Jumatano lina mkasa wote.  ....Soma zaidi===>http://bit.ly/1JljG7Y

 

11 years ago

Habarileo

Moto wateketeza nyumba, maduka Dar

NYUMBA moja imeteketea kwa moto na nyingine vyumba viwili wakati moto huo ulipozuka ghafla kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana. Katika tukio la kwanza, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura alisema moto uliteketeza nyumba moja yenye vyumba 12 eneo la Mwananyamala A juzi saa 5.30 asubuhi.

 

11 years ago

Michuzi

NYUMBA YAWAKA MOTO JIJINI MBEYA

Wakazi wa eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiwa wamesimama nje nyumba iliopo kwenye eneo hilo ambayo imepatwa na dhahma ya kuungua moto na kuteketea kwa mali zote zilizokuwemo ndani ya nyumba hiyo,kutokana na hitilafu ya umeme iliyojitokeza.haijadhibitika mpaka sasa kama kuna mtu yeyote aliedhulia kwenye tukio hilo lililotokea mchana wa leo jijini humo. Sehemu ya mali zilizokuwemo kwenye nyumba hiyo zikiwa zimeteketea zote kwa moto huo. Majirani wakiangali kupitia dirishani kuona namna...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani