Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Sakata IPTL lazidi kuwavuruga wabunge

>Sakata la fedha za IPTL limechukua sura mpya baada ya baadhi ya wabunge kudai kurubuniwa na wenzao kwa fedha ili wakwamishe Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini, wakidai balozi mmoja yuko nyuma ya mpango huo.

Mwananchi

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

VYAMA VITANO VYA SIASA VISIVYO NA WABUNGE VYAOMBA SAKATA LA IPTL LIMALIZWE

Na Dotto Mwaibale 
 MAKATIBU wakuu wa vyama vitano vya kisiasa visivyo na wabunge bungeni wameomba suala la utata wa ufisadi zaidi ya sh.bilioni 300 zilizowekwa katika akaunti ya Tegeta Escrow zilizokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) limalizwe ili kuendelea kwa mambo mengine ya kitaifa.
 Katika hatua nyingine makatibu hao wamepinga hatua ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru) kukabidhi ripoti ya uchunguzi kwa Waziri Mkuu na kudai ipelekwe kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini...

 

10 years ago

Mwananchi

Sakata la rufaa ya Ndumbaro sasa laanza kuwavuruga TFF

Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Hammidu Mbwezeleni amesema TFF isipotoshe umma kwa vile bado haijawasilisha rufaa ya Damas Ndumbaro kwenye kamati yao.

 

10 years ago

GPL

SAKATA LA DK. SLAA KUTAKA KUUAWA LAZIDI KUPAMBA MOTO

Na Uwazi Mizengwe
Lile sakata linaloendelea kutingisha katika siasa za Tanzania, la aliyekuwa mlinzi wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Wilbroad Slaa aitwaye Khalid Kangezi, kudaiwa kushirikiana na baadhi ya wanachama wa CCM, akiwemo makamu mwenyekiti wake (Bara), Philip Mangula na maafisa wa usalama wa taifa (TISS) kupanga njama za kumuua kiongozi huyo, linazidi kuchukua sura mpya. Katibu Mkuu wa Chama...

 

11 years ago

Mwananchi

Sakata la kampeni za kuwania urais 2015 lazidi kuibua mapya CCM

Siku nne baada ya Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye kueleza kuwa amekata rufaa Kamati Kuu (CCM) kupinga adhabu ya onyo aliyopewa kwa kuanza mapema kampeni za urais, wenzake watano waliokumbwa pia na adhabu hiyo wamesita kufanya hivyo

 

10 years ago

Mwananchi

Wataka sakata la IPTL bungeni

Bunge limetakiwa kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika na sakata la IPTL, badala ya kupigia kelele jambo linalosababisha masuala muhimu yanayowahusu wananchi kutojadiliwa bungeni.

 

10 years ago

Mwananchi

Sakata la IPTL kutinga bungeni Novemba 27

Ripoti ya ufisadi katika akaunti ya Escrow itawasilishwa bungeni Novemba 27, mwaka huu na kujadiliwa baada ya Kamati ya Uongozi ya Bunge kuridhia kwamba Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) inaweza kushughulikia suala hilo.

 

10 years ago

Mwananchi

Sakata la IPTL, sasa wanasiasa waonywa

Wanasiasa wametakiwa kukaa kimya na kusubiri matokeo ya ripoti ya IPTL itakayotolewa na Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) watakapoendelea kuongea watasababisha kuchakachuliwa.

 

10 years ago

GPL

KAMPUNI YA VIP YAFAFANUA SAKATA LA IPTL‏

 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari pamoja na jopo la wanasheria kutoka Marekani (hawapo pichani kuhusu jambo hilo Dar es Salaam jana.   Mwanasheria maarufu kutoka Amterdam Holand, Dk. Camilo Schutte (kushoto), akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu jambo hilo. Kulia ni Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya VIP na Mabibo Beer Wines and Spirits Limited,… ...

 

10 years ago

Mwananchi

SAKATA LA IPTL: Mabalozi waitaka Serikali kuchukua hatua kali

>Licha ya Rais Jakaya Kikwete kutoa ufafanuzi wa sakata la uchotaji fedha kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa Benki Kuu na kutangaza kuchukua hatua dhidi ya baadhi ya viongozi na watendaji, nchi wahisani wamesema bado suala hilo linawachanganya na wanasubiri tamko la Serikali.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani