Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


STOP PRESS: Mchungaji Mtikila afariki katika ajali alfajiri leo


Mwanasiasa maarufu nchini Tanzania mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia Majira ya saa 10 alfajiri akitokea mkoani kwake Njombe katika kampeni .
 Taarifa zilizothibitishwa na mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini na mwenyekiti wa DP Mkoa Robart Kisinini wakati akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz amesema ni kweli mwenyekiti wake huyo Taifa amefariki dunia Kamanda wa polisi mkoa wa pwani pia amethibitisha.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Dewji Blog

Breaking News: Mchungaji Christopher Mtikila afariki dunia leo alfajiri

ChristopherMtikila

Taarifa zilizotufikia hivi punde katika chumba chetu cha habari, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (pichani) amepata ajali na kufariki dunia alfajiri ya leo eneo la Msolwa-Chalinze.

Modewji blog inaungana na wanachama wa DP pamoja na watanzania wote katika kuomboleza kifo cha Mchungaji Mtikila, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Mchungaji Mtikila Amen.

mtikila

Pichani ni gari iliyopinduka na kumuua Mchungaji Mtikila.

Taarifa za kifo chake...

 

9 years ago

Michuzi

STOP PRESS: MBUNGE WA LUDEWA MHE DEO FILIKUNJOMBE AFARIKI KATIKA AJALI YA CHOPA

 










Mbunge wa Ludewa Mhe Deogratias Haule Filikunjombe (chini) amefariki dunia katia ajali ya Chopa katika hifadhi ya wanyama ya Selous, pamoja na rubani Kepteni William Silaa (juu kulia), mfanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa na ndugu yake Marehemu Filikunjombe ambao majina  hayajapatikana mara moja.
Mhe. Deo Filikunjombe, rubani na  na abiria wengine walipata matatizo ya engine ya chopa namba  5Y-DKK jana jioni wakitokea Dar kuelekea Ludewa.

Kwa mujibu wa Meya wa Ilala aliyemaliza muda...

 

9 years ago

Mwananchi

Mchungaji Mtikila afariki kwa ajali ya gari Chalinze

Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia leo alfajiri kwa ajali ya gari katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar Mohamed amethibitisha.

 

9 years ago

Michuzi

STOP PRESS: WAZIRI CELINA KOMBANI AFARIKI DUNIA NCHINI INDIA LEO

Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka 56.
Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa...

 

9 years ago

Michuzi

STOP PRESS: VIJANA SITA WA JKT BULOMBORA MKOANI KIGOMA WAPOTEZA MAISHA 21 WAJERUHIWA KATIKA AJALI JIONI HII

Na Editha Karlo wa Globu ya Jamii, Kigoma VIJANA sita  waliokuwa  katika mafunzo ya kijeshi ya kujitolea katika kikosi cha 821 JKT Bulombora mkoani Kigoma wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya gari iliyotokea jioni hii. Mganga Mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Kigoma Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.  "Ni kweli leo majira ya saa moja jioni tumepokea miili minne ya vijana wa JKT ambao waliketwa hapa tayari wamefariki na majeruhi 21....

 

10 years ago

Michuzi

NEWS ALERT: WATU WANNE WAFARIKI KATIKA AJALI YA BASI NA TRENI MKOANI MOROGORO LEO ALFAJIRI

Watu wanne wamefariki dunia na 21 kujeruhiwa baada ya basi aina ya Isuzu  kugonga treni ya abiria iendayo bara katika  kilomita 276/0 kati ya Stesheni  za Kimamba na Kilosa mkoani Morogoro saa 11:25 asubuhi leo Julai 01, 2015. Wahanga walipakiwa katika  treni hiyo na kukimbizwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kilosa.Basi lilohusika ni lenye namba za usajili T837CTM Isuzu Coaster linalomilikiwa na Feisal  A. Khuwel wa Kilosa.Taarifa kutoka eneo la tukio  limefafanua kuwa waliofariki ni wanaume...

 

9 years ago

GPL

TANZIA: MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI DUNIA

Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha DP Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani asubuhi ya leo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 asubuhi ya leo katika kijiji...

 

5 years ago

CCM Blog

DC MTWARA EVOD MMANDA AFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO

MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Wakili Evod Mmanda, amefariki dunia alfajiri ya leo Jumatatu, Aprili 27, 2020, katika Hospitali ya Ligula, Mtwara kutokana na maradhi ya moyo

Taarifa zinaeleza kuwa aliwahi kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam miezi minne iliyopita akisumbuliwa na matatizo ya presha kisha baadaye akaruhusiwa.

Mmanda aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Mtwara na Rais John  Magufuli, Desemba 19, 2016, akichukua nafasi ya Dkt. Khatib Kazungu ambaye alihamishiwa...

 

9 years ago

Vijimambo

BREAKING NEWS: MCH. CHRISTOPHER MTIKILA AFARIKI KWA AJALI YA GARI MKOANI PWANI

Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama Cha DP Mch Christopher Mtikila amefariki dunia kwa ajali ya gari kijiji iliyotokea cha Msolwa, Chalinze mkoani Pwani asubuhi ya leo na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali.
ENDELEA KUTUFUATILIA KWA TAAARIFA ZAIDI
CHANZO: TBC TV

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani