Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


TANZIA: MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI DUNIA

Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha DP Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani asubuhi ya leo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 asubuhi ya leo katika kijiji...

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Dewji Blog

Breaking News: Mchungaji Christopher Mtikila afariki dunia leo alfajiri

ChristopherMtikila

Taarifa zilizotufikia hivi punde katika chumba chetu cha habari, Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (pichani) amepata ajali na kufariki dunia alfajiri ya leo eneo la Msolwa-Chalinze.

Modewji blog inaungana na wanachama wa DP pamoja na watanzania wote katika kuomboleza kifo cha Mchungaji Mtikila, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Mchungaji Mtikila Amen.

mtikila

Pichani ni gari iliyopinduka na kumuua Mchungaji Mtikila.

Taarifa za kifo chake...

 

9 years ago

Mwananchi

Mchungaji Mtikila afariki kwa ajali ya gari Chalinze

Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia leo alfajiri kwa ajali ya gari katika Kijiji cha Msolwa, Chalinze, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jaffar Mohamed amethibitisha.

 

9 years ago

Michuzi

STOP PRESS: Mchungaji Mtikila afariki katika ajali alfajiri leo


Mwanasiasa maarufu nchini Tanzania mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia Majira ya saa 10 alfajiri akitokea mkoani kwake Njombe katika kampeni .
 Taarifa zilizothibitishwa na mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini na mwenyekiti wa DP Mkoa Robart Kisinini wakati akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz amesema ni kweli mwenyekiti wake huyo Taifa amefariki dunia Kamanda wa polisi mkoa wa pwani pia amethibitisha.

 

5 years ago

CCM Blog

TANZIA: MDOGO LOWASSA AFARIKI DUNIA


  Mdogo wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anayefahamika kwa kwa jina la Bernard Lowassa, amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Aghakhan jijini Dar es salaam.


Mtoto wa Waziri Mkuu huyo Mstaafu Fred Lowassa amethibitisha hayo
"Ni kweli ndugu yetu Bernard lowassa amefariki yeye ni Baba yangu mdogo, na alikuwa amelazwa Aga Khan na hapa familia tunaenda hospitalini kwa ajili ya kukutana."- Amesema

 

5 years ago

CCM Blog

TANZIA: IDDI SIMBA AFARIKI DUNIA

   Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya tatu, Iddi Simba amefariki dunia leo.
Taarifa zilizothibitishwa na mtoto wake, Sauda Simba Kilumanga zinasema Iddi Simba amefariki katika Hospitali ya JKCI alipokuwa akipatiwa matibabu.

 

10 years ago

GPL

TANZIA: ABDUL BONGE AFARIKI DUNIA

Abdul Bonge enzi za uhai wake. ALIYEWAHI kuwa Meneja wa wasanii na mwanzilishi wa Kundi la Tip Top Connection, Abdul Bonge amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo akiwa nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. Chanzo cha kifo cha Abdul Bonge bado hakijafahamika ila msiba upo Manzese Tip Top. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN

 

9 years ago

Mtanzania

Mtikila afariki dunia ajalini

MtikilaChristopherMtikilaNA Waandishi Wetu, Chalinze na Dar
MWANASIASA mkongwe na Mwenyekiti wa Chama Cha Democratic (DP), Mchungaji Christopher Mtikila (62) amefariki dunia kwa ajali ya gari katika Kijiji cha Msolwa,   Jimbo la Chalinze mkoani Pwani, barabara Kuu ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Jafary Ibrahimu alisema ajali hiyo ilitokea saa 11 alfajiri usiku wa kuamkia jana alipokuwa akitoka mkoani Njombe kurejea Dar es Salaam.

 

“Ni kweli Mtikila amefariki dunia saa 11 alfajiri katika eneo la Msolwa...

 

9 years ago

Michuzi

TANZIA: Geoffrey Boardington Gondwe afariki dunia

Ndg.Robert Gondwe wa Dar es Salaam,anasikitika kutangaza kifo cha kaka yake Geoffrey Boardington Gondwe kilichotokea jana(25.08.2015).
Ataangwa kesho(27.08.2015) kwake Kunduchi saa 6 mchana. Mazishi yatafanyika katika   makaburi ya Kinondoni saa kumi jioni.

Sisi tulimpenda, lakini BWANA alipenda zaidi. Jina lake BWANA na lihimidiwe...
AMINA!

 

10 years ago

Michuzi

TANZIA: CHE MUNDUGWAO AFARIKI DUNIA LEO

Mwanamuziki Mkongwe wa Nyimbo za Asili hapa nchini, Chigwele Che Mundugwao (pichani) amefariki Dunia mapema leo asubuhi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es salaam.
Kabla ya kufikwa na mauti, Che Mundugwao aliugua na kulazwa katika hospitali ya Muhimbili kwa muda mrefu. 
Che Mundugwao alikuwa anashikiliwa katika gereza la Segerea kwa kukosa dhamana ya kesi yake,  ya kukutwa na pasi za kusafiria 12 za watu tofauti tofauti bila kuwa na maelezo yake.
Taarifa zaidi zitawajia baadae...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani