Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


STOP PRESS: WAZIRI CELINA KOMBANI AFARIKI DUNIA NCHINI INDIA LEO

Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka 56.
Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Dewji Blog

Waziri Celina Kombani afariki dunia nchini India leo, mwili wake watarajiwa kuwasili nchini JUMATATU

kombani

Majonzi makubwa  lufuatia taarifa za msiba  jioni ya leo Septemba 24.2015, Aliyekuwa  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeshi Kombani (56),  amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. 

Tayari mamlaka husika ikiwemo Serikali na Bunge  kupitia  ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kubainisha kuwa, mwili wa marehemu unategemewa kuwasili  Tanzania, siku ya Jumatatu, na shughuli zote Bunge na Serikali zitasimamia...

 

9 years ago

Mtanzania

Waziri Celina Kombani afariki dunia

kombani masikini

NA KULWA KAREDIA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani amefariki dunia.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila aliliambia MTANZANIA jana usiku kuwa Waziri Kombani alifikwa na mauti katika Hospitali ya Apollo nchini India ambako alikuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu karibu wiki mbili.

“Ni kweli Waziri Kombani amefariki dunia leo jioni (jana), kwa saa za kwetu..alikuwa India kwa matibabu karibu wiki mbili hivi.

“Mimi kama kiongozi wa Bunge naweza...

 

9 years ago

GPL

TANZIA: MBUNGE WA ULANGA MASHARIKI, CELINA KOMBANI AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Celina Ompeshi Kombani enzi za uhai wake. Aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Celina Ompeshi Kombani amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu huko nchini India. Bi. Celina Kombani alizaliwa Juni 19 mwaka 1959 na kufariki leo Septemba 24...

 

9 years ago

Mwananchi

Waziri Kigoda afariki dunia nchini India

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda amefariki dunia leo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

 

9 years ago

Dewji Blog

News Alert; Waziri Kigoda afariki dunia nchini India

kigoda

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh Abdallah Kigoda (pichani) amefariki dunia jioni hii nchini India alikokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo cha Mh Kigoda ambaye pia alikuwa mbunge wa Handeni mkoani Tanga zimethibitishwa na ofisi ya Bunge jijini Dar es Salaam.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda nchini India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015, kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo. Taarifa zaidi kutolewa baadaye.

Modewji Blog inaungana na Familia ya Marehemu pamoja na Watanzania kwa...

 

9 years ago

Habarileo

Waziri Kombani afariki dunia

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi), Celina Kombani amefariki dunia jana akiwa nchini India alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

9 years ago

Michuzi

STOP PRESS: Mchungaji Mtikila afariki katika ajali alfajiri leo


Mwanasiasa maarufu nchini Tanzania mwenyekiti wa chama cha DP Mchungaji Christopher Mtikila amefariki dunia Majira ya saa 10 alfajiri akitokea mkoani kwake Njombe katika kampeni .
 Taarifa zilizothibitishwa na mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini na mwenyekiti wa DP Mkoa Robart Kisinini wakati akizungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.co.tz amesema ni kweli mwenyekiti wake huyo Taifa amefariki dunia Kamanda wa polisi mkoa wa pwani pia amethibitisha.

 

9 years ago

Vijimambo

MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AONGOZA MAZISHI YA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA TUMISHI WA UMMA MAREHEMU CELINA KOMBANI LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Udongo kwenye kaburi la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma marehemu Celina Kombani wakati wa mazishi yake yaliyofanyika leo shambani kwake katika kijiji cha Lukobe mkoani Morogoro. (Picha na OMR)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Shada la maua kwenye kaburi la Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma...

 

9 years ago

GPL

CELINA KOMBANI KUAGWA LEO DAR

Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM), Bi. Celina Kombani. Mwili wa Marehemu Kombani ulivyoshushwa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Nyerere kutoka India, juzi. Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM), Bi. Celina Kombani utaagwa rasmi leo Jumatatu, kuanzia majira ya saa nne asubuhi katika Viwanja...

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani