Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


Waziri Celina Kombani afariki dunia nchini India leo, mwili wake watarajiwa kuwasili nchini JUMATATU

kombani

Majonzi makubwa  lufuatia taarifa za msiba  jioni ya leo Septemba 24.2015, Aliyekuwa  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeshi Kombani (56),  amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. 

Tayari mamlaka husika ikiwemo Serikali na Bunge  kupitia  ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kubainisha kuwa, mwili wa marehemu unategemewa kuwasili  Tanzania, siku ya Jumatatu, na shughuli zote Bunge na Serikali zitasimamia...

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

9 years ago

Michuzi

STOP PRESS: WAZIRI CELINA KOMBANI AFARIKI DUNIA NCHINI INDIA LEO

Habari zilizotufikia jioni hii zinasema kwamba Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Ompeashi Kombani (pichani), amefariki dunia leo huko India alikokuwa akipata matibabu ya saratani. Alikuwa na umri wa miaka 56.
Taarifa kutoka ofisi za Bunge zimethibitisha kifo hicho na kueleza kwamba mwili wa marehemu unategemewa kuwasili Dar es salaam siku ya Jumatatu, ambapo Bunge na Serikali zitasimamia maandalizi yote ya maziko na kumsafirisha kwa mazishi nyumbani kwa...

 

9 years ago

Mtanzania

Waziri Celina Kombani afariki dunia

kombani masikini

NA KULWA KAREDIA

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), Celina Kombani amefariki dunia.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila aliliambia MTANZANIA jana usiku kuwa Waziri Kombani alifikwa na mauti katika Hospitali ya Apollo nchini India ambako alikuwa amelazwa kwa ajili ya matibabu karibu wiki mbili.

“Ni kweli Waziri Kombani amefariki dunia leo jioni (jana), kwa saa za kwetu..alikuwa India kwa matibabu karibu wiki mbili hivi.

“Mimi kama kiongozi wa Bunge naweza...

 

9 years ago

Mwananchi

Waziri Kigoda afariki dunia nchini India

Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Handeni Tanga na Waziri wa Viwanda na Biashara, Abdalah Kigoda amefariki dunia leo nchini India alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

 

9 years ago

Dewji Blog

News Alert; Waziri Kigoda afariki dunia nchini India

kigoda

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh Abdallah Kigoda (pichani) amefariki dunia jioni hii nchini India alikokuwa anapatiwa matibabu.

Taarifa za kifo cha Mh Kigoda ambaye pia alikuwa mbunge wa Handeni mkoani Tanga zimethibitishwa na ofisi ya Bunge jijini Dar es Salaam.

Mhe. Dkt. Kigoda alikwenda nchini India kwa matibabu tarehe 18 Septemba, 2015, kupata matibabu katika hospitali Hiyo ya Apollo. Taarifa zaidi kutolewa baadaye.

Modewji Blog inaungana na Familia ya Marehemu pamoja na Watanzania kwa...

 

9 years ago

GPL

TANZIA: MBUNGE WA ULANGA MASHARIKI, CELINA KOMBANI AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Celina Ompeshi Kombani enzi za uhai wake. Aliyekuwa Mbunge wa Ulanga Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na  Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Celina Ompeshi Kombani amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu huko nchini India. Bi. Celina Kombani alizaliwa Juni 19 mwaka 1959 na kufariki leo Septemba 24...

 

9 years ago

Vijimambo

MWILI WA MAREHEMU CELINA O. KOMBANI WAWASILI DAR ES SALAAM LEO JIONI

 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani  ukitelemshwa baada ya kuwasili jioni hii Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Mh. Celina Kombani umewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali . Tutaendelea kuwafahamisha ratiba kila tutapopata...

 

9 years ago

Michuzi

MWILI WA DR KIGODA KUWASILI LEO NCHINI

MAREHEMU Dk Abdalala Kigoda enzi za uhai wake(Pichani) 
 Mwili wa aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Dk Abdalala Kigoda aliyefariki  nchini India unatarajia kuwasili leo mchana tayari kwa ajili ya mazishi.
Ofisa habari wa Bunge, Prosper Minja ameiambia Mwananchi kuwa mwili huo utawasili saa nane mchana kwa ndege ya Emirates na kwenda kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya jeshi ya Lugalo.
Minja amefafanua kuwa shughuli za kuaga mwili huo zitafanyika kwenye Ukumbi wa Karimjee kuanzia saa mbili...

 

9 years ago

Habarileo

Mwili wa Kombani kuwasili Dar leo

MWILI wa aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani, unatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo saa 9 alasiri kutoka nchini India, alikofariki wakati akipatiwa matibabu ya saratani.

 

10 years ago

Mwananchi

Mwili wa mtoto Imran kuwasili nchini leo

Mwili wa mtoto Imran Mwerangi aliyefariki dunia katika Hospitali ya Apollo, India alikokuwa amepelekwa kwa matibabu, unatarajiwa kuwasili leo.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani