Jobs

Sales Representative

NORTH AMERICA ALIGN WORKERS EMPLOYMENT PROGRAM (NAAWEP)
Deadline: Oct 26, 2105




POPULAR ON YOUTUBE


TANZIA: CHIGWELE CHE MUNDUGWAO AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki Chigwele Che Mundugwao enzi za uhai wake. MWANAMUZIKI maarufu wa nyimbo za asili nchini, Chigwele Che Mundugwao amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na matatizo ya damu. Marehemu Chigwele Che Mundugwao amewahi kulipatia taifa sifa kimataifa katika nchi za Scandinavia ambako alijipatia mialiko mbalimbali ya kuwaburudisha mashabiki wake wa...

GPL

Read more


Habari Zinazoendana

10 years ago

Michuzi

TANZIA: CHE MUNDUGWAO AFARIKI DUNIA LEO

Mwanamuziki Mkongwe wa Nyimbo za Asili hapa nchini, Chigwele Che Mundugwao (pichani) amefariki Dunia mapema leo asubuhi kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es salaam.
Kabla ya kufikwa na mauti, Che Mundugwao aliugua na kulazwa katika hospitali ya Muhimbili kwa muda mrefu. 
Che Mundugwao alikuwa anashikiliwa katika gereza la Segerea kwa kukosa dhamana ya kesi yake,  ya kukutwa na pasi za kusafiria 12 za watu tofauti tofauti bila kuwa na maelezo yake.
Taarifa zaidi zitawajia baadae...

 

10 years ago

Mtanzania

Che Mundugwao afariki dunia

Che MundugwaoNA RHOBI CHACHA
ALIYEWAHI kuwa Mjumbe wa Bodi na Katibu Mkuu wa Chama cha Muziki wa Asili nchini, mwanamuzi Chigwele che Mundugwao, amefariki dunia jana katika Hospitali ya Muhimbili, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Che Mundugwao (48) aliyewahi kutamba na nyimbo mbalimbali za ngoma za asili ikiwemo ya ‘Tumetoka Kwetu Mayenge’, pia alikuwa mtayarishaji wa vipindi vya muziki vya redio.
Rais wa Shiriko la Muziki, Samweli Mbwana (Bratoni),
aliliambia Mtanzania kwamba msanii huyo aliyekuwa...

 

10 years ago

GPL

SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA MSANII CHIGWELE CHE MUNDUGWAO

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa kifo cha Msanii wa muziki wa asili Chigwele Chemundugwao kilichotokea Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam jana mapema Asubuhi ya Alhamisi ya tarehe 16/04/2015 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Che mundugwao ni msanii wa muziki wa asili na mdau wa muda mrefu wa sekta ya Sanaa nchini. Amekuwa na mchango mkubwa katika kukuza muziki wa asili...

 

10 years ago

Michuzi

mazishi ya Chigwele Che Mundugwao kufanyika kwao wilayani masasi, Mtwara, kesho


MAZISHI ya aliyekuwa msanii wa muziki wa asili Chigwele Che Mundugwao, 46, aliyefariki dunia jana asubuhi katika hospitali ya taifa Muhimbili, yanatarajiwa kufanyika kesho Ijumaa  Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara.
Rais  wa Shirikisho la Muziki Tanzania Ado Novemba, alisema marehemu alifikwa na umauti huo baada ya kufikishwa hospitalini akitokea Keko gerezani ambako alikuwa mahabusi.“Marehemu Che Mundugwao alikuwa akisumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu miezi miwili iliyopita, akiwa huko...

 

10 years ago

Dewji Blog

Breaking News!!No More Che Mundugwao! afariki dunia mchana wa leo katika Hospitali ya Muhimbili

4

Che Mundugwao enzi za uhai wake.

Na Andrew Chale wa Modewji blog

Katika masikitiko makubwa na majonzi, Tanzania imeweza kumpoteza msanii mahiri  wa muziki wa asili nchini, Chigwele Che Mundugwao  alifariki mchana wa leo.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka vyanzo vya habari, vilivyoifikia  chumba cha Habari Modewji blog, zilieleza kuwa, CHE MUNDUGWAO amefariki dunia leo Aprili 16, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Hata hivyo taarifa zaidi zitaendelea  kutolewa hapo baadae..ENDELEA...

 

10 years ago

Mtanzania

Dk. Che-Mponda afariki dunia

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MWASISI wa Chama cha Tanzania Peoples (TPP) aliyeandika chapisho la mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi, Dk. Aleck Che-Mponda, amefariki dunia.
Mtoto wa marehemu, Chemi Che-Mponda, alisema jana kwamba baba yake alifariki dunia jana katika Hospitali ya Massana iliyoko Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Enzi za uhai wake, Dk. Che-Mponda alifanya utafiti kuhusu mgogoro wa Malawi na Tanzania kuhusu Ziwa Nyasa mwaka 1971 alipokuwa akisomea shahada ya uzamivu...

 

10 years ago

Habarileo

Che Mponda afariki dunia

Dk Aleck Che-Mponda enzi za uhai wakeMWASISI wa chama cha siasa, Tanzania People’s Party (TPP), Dk Aleck Che-Mponda (80) amefariki dunia katika hospitali ya Massana iliyopo Mbezi Beach, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani ya mifupa.

 

9 years ago

GPL

TANZIA: MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI DUNIA

Mwanasiasa mashuhuri nchini na Mwenyekiti wa Chama Cha DP Mch.Christopher Mtikila amefariki dunia na watu wengine watatu kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichopo Chalinze mkoani Pwani asubuhi ya leo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Jafari Mohamed, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa "Taarifa za mwanzo" zinasema Mtikila amefariki majira ya saa 11:45 asubuhi ya leo katika kijiji...

 

5 years ago

CCM Blog

TANZIA: IDDI SIMBA AFARIKI DUNIA

   Aliyewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika serikali ya awamu ya tatu, Iddi Simba amefariki dunia leo.
Taarifa zilizothibitishwa na mtoto wake, Sauda Simba Kilumanga zinasema Iddi Simba amefariki katika Hospitali ya JKCI alipokuwa akipatiwa matibabu.

 

Share

Magazeti ya Leo

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani