TSHABALALA AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA WA MWEZI
Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.
MSHINDI wa mwezi wa Oktoba, 2015 ni Mohamed Hussein Tshabalala ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.
Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mwanachama na Shabiki wa Simba Mbunge wa...
Michuzi