Uchaguzi Arusha Mjini kuahirishwa
JIMBO la Arusha Mjini na Chama cha ACT-Wazalendo, wamepata msiba wa aliyekuwa mgombea wa ubunge wa jimbo hilo, Estomih Mallah na kusababisha kuwa jimbo la tatu ambalo kura ya mbunge haitapigwa katika Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa Oktoba 25 mwaka huu.
Majimbo mengine ambayo kura ya kuchagua wabunge haitapigwa ni Lushoto, baada ya kufariki kwa mgombea ubunge wa Chadema, Mohamed Mtoi mwanzoni mwa Septemba mwaka huu.
Lingine ni Ulanga Mashariki, baada ya mgombea ubunge wa jimbo...
Vijimambo
Habari Zinazoendana
9 years ago
Mtanzania10 Oct
Uchaguzi wa ubunge Arusha kuahirishwa
NA ELIYA MBONEA, ARUSHA
CHAMA cha ACT Wazalendo kimepata pigo baada ya mgombea wake wa Ubunge Jimbo la Arusha Mjini, Estomih Mallah kufariki katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Mjini Moshi.
Katika hilo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa mujibu wa sheria italazimika kuusogeza mbele uchaguzi wa ngazi ya ubunge.
Ilidaiwa kuwa Septemba 6, mwaka huu Mallah alianza kujisikia vibaya wakati akiwa katika mkutano wa mgombea urais wa chama chake, Anna Mghwira na kwamba baada ya mkutano alipelekwa...
9 years ago
StarTV10 Oct
Uchaguzi Arusha kuahirishwa kufuatia kifo cha mbunge wa ACT Wazalendo.
Mgombea wa Ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo Estomih Malla, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya rufaa ya KCMC Mjini Moshi, alipokuwa akipatiwa matibabu.
Marehemu Malla alikimbizwa KCMC baada ya hali yake kubadilika ghafla akiwa katika mikutano ya kampeni za chama chake jumatano iliyopita huko Ngaramtoni Arusha.
Katika makao makuu ya chama cha ACT-Wazalendo Arusha Mwenyekiti wake mkoani humo Samwel Kivuyo, amesema wakiwa katika mkutano...
9 years ago
Habarileo02 Nov
Uchaguzi Handeni, Arusha Mjini kufanyika Desemba 12
UCHAGUZI wa ubunge kwa majimbo ya Handeni na Arusha Mjini umepangwa kufanyika Desemba 12, mwaka huu.
9 years ago
MichuziNEC YATAOA TAMKO KUHUSU UCHAGUZI WA WABUNGE ARUSHA MJINI NA HANDENI.
9 years ago
BBCSwahili29 Sep
Uchaguzi mkuu nchini CAR kuahirishwa
10 years ago
Mwananchi15 Apr
Ukawa wahofia Uchaguzi Mkuu kuahirishwa
10 years ago
BBCSwahili19 May
Zuma ataka uchaguzi kuahirishwa Burundi
9 years ago
Dewji Blog28 Oct
Taarifa kamili ya kuahirishwa kwa uchaguzi Zanzibar iko hapa
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
TUME ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) , imefuta na kuhairisha matokeo yote ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu kutokana na kujitokeza kwa kasoro mbali mbali za ukiukaji wa sheria na kanuni za uchaguzi Zanzibar.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa tume hiyo, Jecha Salim Jecha alisema kuwa kutokana na kasoro mbali mbali zilizojitokeza katika uchaguzi huu na kusababisha vikwazo mbali mbali...