Vigogo wa TPA kizimbani Dar
Aliyekuwa Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA), Ephraim Mgawe pamoja na aliyekuwa naibu wake anayeshughulikia huduma, Hamad Mussa Koshuma wamefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na shtaka moja la matumizi mabaya ya madaraka.
Mwananchi
Habari Zinazoendana
11 years ago
Habarileo15 Jul
Vigogo wa juu TPA kizimbani
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na Msaidizi wake, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka.
10 years ago
Uhuru Newspaper13 Nov
Kesi ya vigogo TPA kusikilizwa Desemba
NA FURAHA OMARY
KESI ya matumizi mabaya ya madaraka, inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Ephraim Mgawe na Naibu wake, Hamad Koshuma, imepangwa kuanza kusikilizwa Desemba 2, mwaka huu.
Mgawe na mwenzake, wanadaiwa kutoa zabuni ya upanuzi wa gati namba 13 na 14, katika bandari ya Dar es Salaam, kwa Kampuni ya China Communications Contruction, bila ya kutangaza zabuni.
Washitakiwa hao walipanda kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi...
10 years ago
Mwananchi17 Apr
Sitta ‘atimua’ vigogo TRL, amhamisha Kipande TPA
11 years ago
Tanzania Daima15 Jul
Vigogo Bandari kizimbani
ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Ephraim Mgawe na naibu wake, Hamad Koshuma, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam...
10 years ago
Mtanzania15 Jan
Vigogo kizimbani mgawo Escrow
Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam
SAKATA la uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, limeanza kuchukua sura mpya baada ya Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), kuwafikisha mahakamani vigogo wawili wa Serikali.
Vigogo hao, waliofikishwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam jana, ni Mhandisi Mkuu wa Mradi wa Umeme Vijijini (REA), Theophillo Bwakea na Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Rugonzibwa...
11 years ago
Mwananchi05 Jul
Vigogo Uhasibu Arusha kizimbani
9 years ago
Habarileo20 Aug
Vigogo watatu wizara ya afya kizimbani
MAOFISA Utumishi watatu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh milioni 3.7.
11 years ago
Habarileo06 Jul
Vigogo Chuo cha Uhasibu kizimbani
MKUU wa Chuo cha Uhasibu Arusha, Profesa Johannes Monyo na wenzake saba wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha wakituhumiwa kwa makosa manne tofauti yakiwemo ya uhujumu uchumi na kuisababishia hasara serikali kiasi cha Sh 6,258,448.60.
10 years ago
Habarileo31 May
Vigogo 5 TRL kupandishwa kizimbani kashfa ya mabehewa
MAOFISA watano wa Serikali, wanatarajiwa kupandishwa kizimbani hivi karibuni, kutokana na kashfa ya uagizaji wa mabehewa 274 kutoka India, huku wengine wakitarajiwa kuchukuliwa hatua za kiutawala.