Wakazi kata ya Kurasini Dar wagoma kuhama Kupisha mradi wa maegesho
Wakazi wa kata ya Kurasini Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam wamegoma kuhama katika makazi yao kupisha mradi wa ujenzi wa maegesho ya magari makubwa.
Manispaa ya Temeke imetoa amri ya kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuhama ndani ya muda wa saa 12 kuanzia Novemba 13, vinginevyo nyumba zao zitavunjwa.
wakazi wa Kurasini jijini Dar es Salaam, wamepaza kilio chao kupinga amri ya Manispaa ya Temeke kuwataka kuhama eneo hilo kupisha ujenzi wa maegesho ya magari makubwa.
Wakizungumza na Star...
StarTV
Habari Zinazoendana
11 years ago
Tanzania Daima03 Mar
Wagoma kuhama kupisha barabara
WAKAZI wa kaya 30 wa mitaa ya Majanimapana na Nguvumali zinazotarajiwa kubomolewa makazi yao kupisha ujenzi wa barabara zimetangaza mgogoro na serikali kwa kugoma kuhama na kumtaka Rais Jakaya Kikwete...
10 years ago
Tanzania Daima10 Oct
Wagoma kupisha mradi wa bwawa
WAKAZI wa vijiji vya Bwirachini na Kiburungo Kata ya Selembala Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Vijijini wamegoma kuondoka kwenye makazi yao kupisha mradi wa bwawa la kufua umeme la Kidunda...
10 years ago
Habarileo07 Aug
Machinga wagoma kuhama Jangwani
WAFANYABIASHARA ndogo ndogo maarufu kama ‘machinga’, waliohamishia biashara zao katika eneo la Jangwani wanaendelea na ujenzi wa vibanda pamoja na agizo la serikali kusisitiza kuwa wanapaswa kuhama eneo hilo.
5 years ago
Michuzi![](https://1.bp.blogspot.com/-Vovp4T1uHu8/Xt-dmTYiB4I/AAAAAAALtMo/x53f2-IE67E3xD-DYST1WirLxBsKGgTpwCLcBGAsYHQ/s72-c/290.jpg)
UJENZI MRADI MKUBWA ENEO LA MAEGESHO YA NDEGE UWANJA WA NDEGE WAPAMBA MOTO ZANZIBAR
Harakati za umwagaji wa zege katika sehemu za kupakia na kushukia abiria ziko katika hatua nzuri chini ya wahandisi wa kampuni ya kimataifa ya CRJ kutoka nchini China wakisaidiwa na wahandisi na washauri wazalendo waliobobea kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere wa Dar es Salam.
Makamu wa Pili wa...
11 years ago
Dewji Blog07 Jul
Breaking News: Wakazi wa Kurasini wafunga barabara kwa muda!
Baadhi ya wakazi wa Mivinjeni Kurasini wakiwa na mabango katikati ya Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam hivi sasa, zenye ujumbe wa malalamiko ya kudai kulipwa fidia zao ili kupisha mradi wa ujenzi wa bandari kavu kwenye eneo hilo.
HABARI KAMILI ITAKUJIA HAPO BAADAE KIDOGO..!
Baadhi ya magazri na mabasi yakigeuza yalikotoka.
Gari lililokuwa likielekea kwenye maonyesho ya Sabasaba likizuiwa na wakazi wa eneo hilo.
Mabasi yakizuiwa kupita.
Baadhi ya waanawake wa eneo hilo wakimzuia...
11 years ago
Habarileo23 Mar
Wakazi Pugu watakiwa kuhama
WIKI moja baada ya gazeti hili kuandika kuhusu hatari ya kupata magonjwa, ikiwemo kipindupindu inayowakabili wakazi wanaoishi karibu na dampo la Pugu Kinyamwezi na hatua ya kula kwenye chandarua walioianzisha kupunguza kero ya inzi, uongozi wa Jiji la Dar es Salaam umezungumzia hali hiyo.
9 years ago
StarTV23 Dec
Wakazi wa mabondeni wapewa siku 14 kuhama
Serikali imesitisha kazi ya ubomoaji nyumba za wakazi wanaoishi maeneo ya mabondeni katika bonde la Mto Msimbazi jijini Dar Es Salaam kwa muda wa siku 14 ili kuwapatia nafasi ya kuondoka kwenye maeneo hayo kwa hiari.
Kazi hiyo ya kubomoa nyumba na vibanda vilivyojengwa kinyume cha sheria na maeneo oevu yasiyoruhusiwa kwa ajili ya makazi ya binadamu ilianza Novemba 18 mwaka huu.
Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi na Mipangomiji namba 8 ya mwaka 2007 kifungu cha 30 imeleza kuwa hairuhusiwi wananchi...
11 years ago
Habarileo20 Jan
Maegesho ya magari Dar sasa kusimamiwa na Jiji tu
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imezinyang’anya rasmi Manispaa majukumu ya kusimamia maegesho ya magari na imefuta vibali vyote vya maegesho vilivyotolewa na mamlaka hizo. Hatua hiyo imekuja baada ya Kamati ya Ushauri Mkoa wa Dar es Salaam (RCC) kuagiza halmashauri ya Jiji kufanya kazi hiyo baada ya kubaini halmashauri za Ilala, Kinondoni na Temeke, kisheria hazikupaswa kusimamia maegesho ya magari.